BLOG BADO NI CHACHE MNO…

make-money-online

Habari rafiki,
Siku moja nikiwa naongea na mtu aliyekuwa anaomba ushauri kuhusu blog, aliniauliza huoni kwa sasa blog zimekuwa nyingi sana?
Jibu langu kwake lilikuwa blog bado ni chache mno.
Yaani sisi watanzania bado hatujafikia hatua ya kusema tuna blog nyingi.
Hasa blog zinazotoa maarifa na mafunzo ni chache sana.
Na uchache huu umekuwa unasababishwa na watu kuanza blog kwa hamasa kubwa, lakini baada ya muda wanapotea kabisa.
Unaweza kudhibitisha hili, hesabu blog kumi unazoona zinatoa maarifa na mafunzo leo, halafu njoo ziangalie baada ya mwaka mmoja, utakuta chache ndiyo zimebaki.
Sasa rafiki yangu, kuanzia jumatatu ya wiki ijayo, nitaendesha semina kuhusu blog, na nitakupa mbinu zote za kuweza kuanzisha blog, kuikuza na kutengeneza kipato.
Nafasi bado ni kubwa mno ya kutengeneza kipato kwenye mtandao.
Mwisho wa kujiunga na semina hii ni kesho, hivyo chukua hatua sasa.
Bonyeza link hii kujiunga na semina; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/tengeneza-fedha-kwa-kutu…/
Karibu sana rafiki yangu.
Rafiki yako,
Makirita Amani.

Leave a Reply