Umuhimu Na Matumizi Ya Email List Kwenye Blog Yako.

Mara zote nimekuwa nasema kwamba ili kutengeneza kipato kwenye mtandao basi unahitaji vitu vitatu.

Kitu cha kwanza ni blog, hapa ndiyo nyumbani kwako kwenye mtandao, hapa ndipo watu wakikutafuta wanakupata. Ndipo unapoweka kazi zako kwenye mtandao.

Kitu cha pili ni mfumo wa email (EMAIL LIST) kupitia mfumo huu unakusanya taarifa za wasomaji wa blog yako, hasa majina email na namba za simu, kisha unakuwa unawatumia maarifa kwenye email zao moja kwa moja. Hii ni njia nzuri ya kujenga uhusiano bora na wasomaji wako ambao utakuwezesha kufanya biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Kitu cha tatu ni mitandao ya kijamii, ambapo unahitaji kuwa na kurasa za blog yako kwenye mitandao ya kijamii unayotumia. Mitandao kama facebook, instagram, twitter na linked in ina watumiaji wengi. Unahitaji kuwa kwenye mitandao hii ili kupata wasomaji wa blog yako.

tengeneza-fedha-kwa-blog

Aina za email list.

Kuna aina nyingi za kuweza kutengeneza email list yako. Mimi nashauri utengeneze kwa aina moja kati ya hizi mbili.

Mailchimp ni moja ya aina unazoweza kutumia kutengeneza email list. Mailchimp unakuwezesha kuwa na watu 2000 bure na kuweza kutuma email mpaka 12,000 kwa mwezi. Ni rahisi kutumia na inakubali hata kwa blog za bure ambapo huna jina lako kamili (domain name).

Kutengeneza email list yako kwenye mailchimp tembelea www.mailchimp.com

Mailerlite ni aina nyingine ya kutengeneza email list, hii haina tofauti sana na mailchimp ila ni rahisi zaidi. Unapata nafasi ya kuwa na watu 1000 bure na hakuna ukomo wa email unazoweza kutuma kwa mwezi.

Mailerlite huwezi kutumia kama unatumia blog ya bure, unahitaji kuwa na jina la blog yako (domain name) na email inayoendana na jina hilo. Hivyo unahitaji uwe umehifadhi blog yako mwenyewe (Hosting).

Kutumia mailerlite tembelea www.mailerlite.com

Matumizi ya email list kwenye blog yako.

Ukishakuwa na email list yako kwanza unahitaji kuwashawishi wasomaji wako kujiunga na list hiyo. Unafanya hivyo kwa kuwaahidi kuwatumia maarifa zaidi kwenye email zao. Pia unaweza kuwapa kitabu pale wanapojiunga kwenye email list yako. Unafanya hivi kwa kuweka fomu ya kujiunga na email list yako kwenye blog yako. Weka fomu maeneo ambapo msomaji anaweza kuiona kwa urahisi. Mfano kila mwisho wa makala unaweka fomu. Au unaweka fomu inayotokea juu ya makala kabla msomaji hajasoma au anapomaliza kusoma.

Ukishapata watu kwenye email list yako sasa unaweza kuitumia ifuatavyo;

  1. Tengeneza utaratibu wa kuwa unawatumia maarifa zaidi watu kwenye email zao. Unafanya hivyo kwa kuingia kwenye list yako kisha kutengeneza na kutuma kampeni ya email (email campaign).
  2. Waulize wasomaji iwapo wana changamoto zozote kwa maswali unayoweza kuwa unawatumia kwenye email zao, na hapo unaweza kuwashauri moja kwa moja au kupata makala za kuandika.
  3. Wapatie wasomaji wako ofa mbalimbali kwa kuwatumia taarifa kwenye email zao, hili fanya baada ya muda na wasomaji wako kuwa wameshakuzoea.
  4. Unganisha email list yako na blog yako kiasi kwamba unapoweka makala mpya kwenye blog inakwenda mara moja kwenye email za wasomaji wako. Hii haiji moja kwa moja, badala yake ni lazima utengeneze hivyo. Kutengeneza hili unahitaji kwenda kwenye email list yako, nenda kwneye kuandaa email campaign na chagua RSS feed au campaign, utafuata maelekezo baada ya hapo.
  5. Endesha mafunzo au semina kupitia email list yako, hii pia ni njia nzuri ya kukuza list yako.

Hivyo ndivyo unavyoweza kuwa na email list na jinsi unavyoweza kuitumia.

Kupokea maarifa zaidi kuhusu kutengeneza fedha kwenye mtandao weka taarifa zako kwenye email hapo chini.

[mailerlite_form form_id=1]

Kama una swali lolote kuhusu kutengeneza fedha kwenye mtandao au blog uliza kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Makirita Amani,

Kocha, Mwandishi na Mjasiriamali,

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kupata blog ya kitaalamu kwa tsh elfu kumi (10,000/=) bonyeza maandishi haya.

Kupata kitabu cha kutengeneza blog yako mwenyewe bonyeza maandishi haya.

Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Leave a Reply