MBAKIZE MSOMAJI KWENYE BLOG YAKO KWA MUDA MREFU.

Kuna wasomaji wa aina mbili wa blog yako.

Aina ya kwanza ni wale wasomaji wako wa kila siku, wale ambao tayari ni wafuasi wako na wanajua wakija kwenye blog yako wanajifunza. Hawa ni wasomaji wazuri na unahitaji kuwapa makala nzuri kila siku.

Aina ya pili ni wale wasomaji ambao ndiyo wanaijua blog yako kwa mara ya kwanza. Labda wamekutana na link ya blog yako kwenye mitandao ya kijamii, au walikuwa wanatafuta kitu google na wakafikia kwenye blog yako.
Wasomaji hawa hawakujui, hivyo hawajui vizuri kazi zako. Wanaweza kusema kile ambacho kimewafikisha kwenye blog yako na wakamaliza na kuondoka zao. Ikitokea hivi kwa nafasi kubwa unakuwa umewakosa.

Ipi njia ya kuwabadili hawa watembeleaji wa mara moja kuwa wasomaji wako wa kudumu. Njia hii ni kuhakikisha kila makala ina viungo vya makala nyingine nzuri. Kwa namna hiyo, mtu anaposoma makala, anakutana na kiungo kinachompa makala nyingine ya kusoma. Akifungua makala hiyo anakuta tena mambo mazuri. Huko pia anaweza kufungua nyingine na nyingine na nyingine tena.
Kwa njia hii unamfanya msomaji aliyefika mara moja, kujifunza mengi mno na hatimaye kuanza kukufuatilia zaidi.

SOMA; Umuhimu Na Matumizi Ya Email List Kwenye Blog Yako.

Unawekaje viungo vya watu kusoma zaidi?
Ndani ya makala yako, weka kiungo cha makala ya nyuma. Ninaposema kiungo namaanisha link. Weka maneno SOMA; halafu mbele yake weka kichwa cha makala anayotakiwa kufungua ili kusoma.
Pia unaweza kutumia maneno kama;
INAYOFANANA NA HII;
SOMA MAKALA NZURI;
Kwa njia hii utawapa wasomaji wako maarifa mengi zaidi.
Pia ni njia ya kuwapa wasomaji wapya nafasi ya kusoma makala zako za zamani.

Anza kufanyia kazi hili sasa.
Kwenye kila makala yako, usiache kuweka kiungo cha makala za nyuma. Weka kiungo angalau kimoja na visizidi vitatu kwenye makala yenye maneno mpaka 1000.

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
www.makirita.info

tengeneza-fedha-kwa-blog

Leave a Reply