Jinsi Ya Kutengeneza Email List Ya MAIL CHIMP, Hatua Kwa Hatua.

Email list ni sehemu muhimu ya blog yako ambayo unaweza kuitumia kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Kwenye email list yako, unawashawishi wasomaji wako kujiunga na kisha unakuwa unawatumia makala na mafunzo kupitia email zao.

Mwanzoni utakuwa unawatumia bure ili kujenga uaminifu na kuonesha thamani yako. Baadaye utaweza kuwapatia huduma nyingine za kulipia.

Watu ambao wamejiunga na email list yako, ni watu ambao wapo tayari kununua kutoka kwako kuliko wale wanaotembelea blog yako kwa mara ya kwanza.

Hivyo unahitaji kufanya vitu viwili muhimu;

 1. Kuwa na email list.
 2. Kuikuza email list yako ili kuwa na wasomaji wengi, utakaoweza kuwauzia huduma zako baadaye.

Kwenye makala hii ya leo tutaangalia jinsi ya kutengeneza email list yako. Kwenye makala zijazo tutajifunza mbinu za kukuza email list yako.

Jinsi ya kutengeneza email list ya MAIL CHIMP.

Mail chimp ni moja ya mifumo rahisi ya kutengeneza email list yako. Hapa nakuwekea hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kutengeneza email list yako kwenye mail chimp.

 1. Ingia kwenye mail chimp, www.mailchimp.com utaona kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Bonyeza SIGN UP FREE.

1

2. Jaza taarifa zako kama nilivyoonesha kwenye picha hapo chini. Weka email yako, username na password unayotaka kutumia. Password iwe na HERUFI KUBWA, herufi ndogo, namba na alama kama @#$% ukimaliza bonyeza GET STARTED2

3. Nenda kwenye email yako uliyoandikisha, utakuta umetumiwa email ya kuactivate akaunti yako ya mailchimp3

4. Ukiingia kwenye email yako utaona email kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.4

5. Fungua hiyo email, na bonyeza sehemu iliyoandikwa ACTIVATE ACCOUNT.5

6. Itakupeleka eneo la kujaza taarifa zako, weka majina yako, jina la blog na taarifa nyingine kama watakavyouliza. jaza taarifa zote, hata kama siyo sahihi. mfano sanduku la posta, jaza namba yoyote na mji.7 8 9

7. Kwenye swali la kuuza jaza no.10

8. Kama unataka kuunganisha fomu yako na mitandao ya kijamii, bonyeza facebook au twitter, unaweza kuruka kwa sasa kw akubonyeza continue.11

 

9. Ukishamaliza hivyo acount yako inakuwa tayari. Kama unataka kupokea email zao za matangazo na mafunzo, kubali hapo kama inavyoonekana hapo chini.12

10. Ukishamaliza ingia kwenye email list yako, utaona kama inavyoonekana hapo chini. Bonyeza CREATE A LIST.13

11. Jaza jina la blog yako na email yako. Watakuletea angalizo kwamba email ya gmail siyo nzuri, bonyeza ACKNOWLEDGE THE RISK14

12. Hapo kwenye remainder weka ujumbe ambao watu watakumbuka wanapopokea email yako.15

13. Ukishajaza maelezo yote, bonyeza sehemu ya SAVE.16

14. Hapo umeshatengeneza list yako. Kinachofuata sasa ni kutengeneza fomu ya wasomaji kujiunga. Bonyeza CREATE SIGNUP FORM.17

15. Hapa unaweza kuanza kuchagua GENERAL FORMS, bonyeza sehemu ya select kisha fanya marekebisho. Marekebisho unayoweza kufanya ni kuongeza taarifa ambazo mtu anapaswa kulaza au kuitafsiri fomu kwa kiswahili. Sehemu ya NAME unaweka JINA, pia ongeza sehemu ya kujaza namba ya simu.

Ukimaliza kufanya marekebisho save kisha rudi tena kwenye fomu, safari hii chagua Embeded fomu, hii ndiyo fomu utakayoweka kwenye blog yako ili watu wajiandikishe kwenye list yako.18

16. Hapo chini kuna maelekezo ya EMBEDED FORM, unaweza kufanya marekebisho ya namna unavyotaka ionekane. Kama ulishafanya marekebisho kwenye GENERAL FOEM utayaona huku.

Angalia picha ya chini, kuna sehemu imeandikwa ENABLE RECAPTURE, imewekwa tiki, bonyeza hapo kuondoa hiyo tiki.

Ukishamaliza kopi hiyo code, angalia nilipozungushia alama nyekundu pameandikwa COPY/PASTE, chagua hayo maelezo na kopi, kisha utaneda kupaste kwenye blog yako kama nitakavyoelekeza hapo chini (namba 23).19 20 21

17. Sasa unapaswa kujua namna ya kuwatumia wasomaji wako waliojiunga email za makala na mafunzo. Nenda sehemu iliyoandikwa CAMPAIGN, ibonyeze. Bonyeza sehemu ya CREATE NEW CAMPAIGN22 23

18. Select sehemu ya REGULAE CAMPAIGN24

19. Chagua watu unaotaka wafikiwe na hiyo kampeni, kwa sasa chagua entire list. Ukishachagua angalia chini kuna sehemu imeandikwa next, bonyeza hapo.25

19. Hapo inakuja sehemu ya kuandika maelezo kuhusu kampeni yako. Kampeni name weka neno lolote utakalokumbuka wewe,labda namba ya kampeni.

Email subject weka kichwa cha habari, hii ndiyo msomaji atakayopokea kwenye email yake.

Weka jina unalotaka lionekane kwa msomaji kwamba email imetoka kwa nani.

Kisha weka email ambayo unataka msomaji aone imetoka kwa nani. ukiweka gmail au yahoo watakuletea maelezo ya risk bonyeza ACKNOWLEDGE THE RISK. Baada ya hapo bonyeza NEXT.26

20. Hapa unachagua template ambayo utaitumia kutuma email yako. huu ni muonekano wa email kama atakavyopokea msomaji. Kwa sasa chagua yoyote, chagua hata ile ya kwanza.27

21. Hayo maeneo niliyozungushia alama nyekundu, yabonyeze na utaona option ya kufuta au kurekebisha, futa hayo maelekezo yaliyopo. kisha andika au paste yale maelezo unayotaka kumtumia msomaji wako. kama ni makala basi hapo ndipo pa kuiweka, kwenye hilo eneo la chini lenye maandishi mengi.

Unaweza kufanya marekebisho mbalimbali, angalia upande wako wa kulia. Ukimaliza bonyeza next.28

22. Sasa umeletewa muhtasari wa kampeni unayotaka kutuma, jina la email, jina lako, na email uliyoandikisha. Kama kuna kitu hakipo sawa, unaweza kubadili. Kama kila kitu kipo sawa unaweza kutuma papo hapo kw akubonyeza SEND au kutuma baadaye kw akubonyeza SCHEDULE.

N;B Hiyo ya kwangu imeshindwa kwenda kwa sababu list haina mtu hata mmoja.29

23. Sasa tunarudi kwenye kukopi na kupaste fomu yako kwenye blog yako. Select hayo maneno (codes) kama nilivyofanya hapo chini, ksiha kopi.30

24. Kama unatumia BLOGGER, nenda kwenye makala ambapo unataka kuweka fomu, weka nafasi kisha bonyeza sehemu ya HTML.31

25. Paste ile code yako ambayo ulikopi kutoka kwenye email list. ukishamaliza bonyeza sehemu ya COMPOSE, utarudi kwenye uandishi wa kawaida na utaiona fomu yako.32

26. Fomu inaweza kuonekana kama mistari pekee, lakini makala ikienda hewani itaonekana vizuri.33

27. Kama unatumia WORDPRESS, nenda kwenye makala ambapo unataka fomu itokee, weka cursor, kisha rudi juu na bonyeza sehemu imeandikwa TEXT.34

28. Baada ya hapo paste code yako na bonyeza sehemu ya VISUAL utaona fomu yako. Makala ikienda hewano fomu itaonekana vizuri zaidi.35 36

Ukishamaliza kuweka fomu endelea kupost makala yako kama kawaida.

Hivyo ndivyo unavyoweza kutengeneza email list, kutengeneza kampeni na kuweka fomu ya email list kwenye makala zako.

MUHIMU;

Kwenye blog yako, tengeneza ukurasa (PAGE) ambapo utaiweka fomu hiyo pekee. fuata hatua nilizoelekeza hapo juu. nenda kwenye pages, add new page, ikifunguka andika maelezo ya kumashawishi msomaji kujiunga, kisha bonyeza HTML kwa blogger au TEXT kwa wordpress, paste ile code yako ksiha rudi kawaid ana post.

Kwa hatua hii utakuw ana ukurasa maalumu wa watu kujiunga, na unaweza kuweka link ya ukuraha huo kwenye makala zako kwa kuwaambia watu BONYEZA HAPA kujiunga na mtandao huu.

Fanyia kazi hayo, na kama utakwama popote uliza swali kwenye sehemu ya maoni hapo chini, nitakuelekeza vizuri.

Kila la kheri.

Makirita Amani,

Kocha, Mwandishi na Mjasiriamali,

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kupata blog ya kitaalamu kwa tsh elfu kumi (10,000/=) bonyeza maandishi haya.

Kupata kitabu cha kutengeneza blog yako mwenyewe bonyeza maandishi haya.

Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

6 thoughts on “Jinsi Ya Kutengeneza Email List Ya MAIL CHIMP, Hatua Kwa Hatua.

 1. Thomas Malale

  Habari Mkuu, nimesoma Post yako na jinsi ulivyoelekeza kutengeneza email list na kutengeneza page yenye form kwenye blog. Nimefanya kama ulivyoelekeza kwenye email list nimefanikiwa lakini kwenye page nimefanya kama hatua zako lakini nimejaribu kuifungua hiyo page kwa kutumia simu lakini bado imeleta maneno tu bila viboksi vyakujaza! naomba msaada wako….

  Reply
     1. Thomas Malale

      Sehemu ya kujaza taarifa vibox havitokei vizuri kuruhusu mtu kujaza taarifa zake yaani hapo vilipo mtu hawezi kujaza taarifa kwa sababu akiclick havifunguki!

     2. mtaalamu Post author

      Ondoa hiyo fomu na tengeneza fomu nyingine.
      Inaonekana hiyo ina shida, au ulicopy code vibaya.

Leave a Reply