Itumie Blogu Yako Kama Jukwaa Lako.

Moja ya vitu ambavyo kila mtu anahitaji kwenye zama hizi za taarifa ni jukwaa. Jukwaa ni ile nafasi ambayo mtu anakuwa nayo, ambapo watu wanamsikiliza na kumfuatilia. Yapo majukwaa mbalimbali, majukwaa ya utaalamu, majukwaa ya sanaa, majukwaa ya kisiasa na hata majukwaa ya kibiashara.

Katika ulimwengu huu wa zama za taarifa, majukwaa yameongezeka zaidi. Mtandao wa intaneti umeleta urahisi wa kila mtu kuweza kuwa na jukwaa lake mwenyewe, kwa namna anavyochagua yeye mwenyewe.

Kwa majukwaa ya zamani, ilibidi mtu awe ameidhinishwa kuweza kufuatiliwa na kusikilizwa na wengine. Kwa mfano kwa jukwaa la utaalamu, ilibidi uwe umesomea na kupata vyeti fulani ndiyo uweze kuwa na jukwaa la utaalamu fulani. Au kama ni jukwaa la sanaa, ilibidi msanii awe amekubalika na wale wanaorekodi na kukuza sanaa.

Lakini kwenye ulimwengu wa sasa, huhitaji tena mtu wa kukupa jukwaa, husubiri tena mpaka mtu akuchague na kukudhibitisha. Sasa unaweza kujichagua wewe mwenyewe, kujipa jukwaa na ukapata watu wa kukusikiliza.

Zipo njia nyingi za kujipa jukwaa kwenye mtandao wa intaneti. Unaweza kuwa na tovuti, kuwa na blogu au kutumia mitandao ya kijamii kama jukwaa lako. Ni wewe mwenyewe unachagua kulingana na uhitaji wako.

Katika njia hizi nyingi za kuwa na jukwaa kwenye zama hizi, blogu ni njia bora zaidi ya kufanyia kazi. Hii ni kwa sababu blog ni rahisi kuendesha, huhitaji kuwa na utaalamu mkubwa kufanya hivyo. Na pia blogu inatunza kazi zako vizuri, mtu yeyote anaweza kuzikuta kazi zako zote mahali pamoja, tofauti na mitandao ya kijamii ambayo siyo rahisi mtu kukuta kazi zako kwa pamoja.

Tumia nafasi uliyonayo sasa kujenga jukwaa lako, kwa kuandika kile ambacho ungependa wengine wakijue ili waweze kuboresha maisha yako. Usisubiri mtu akuchague, jichague wewe mwenyewe sasa, na tumia blogu kuwa jukwaa lako. Toa taarifa na maarifa yanayoongeza thamani kwenye maisha ya wengine.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK.

Makirita Amani,

Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Karibu sana kwenye MTAALAMU NETWORK uweze kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Kujua huduma za blog tunazotoa BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kusoma makala zetu za mbinu na maarifa ya kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Itumie Blogu Yako Kama Jukwaa Lako.

  1. Pingback: Mitandao Ya Kijamii Siyo Jukwaa, Tengeneza Jukwaa Lako Kwa Njia Hizi Mbili. | MTAALAMU Network

Leave a Reply