Unapolalamika Kuhusu Mitandao Ya Kijamii, Umeamua Kupoteza Fursa Ya Kutengeneza Fedha.

mtaalamu 1

Facebook ni mtandao wa kijamii namba moja duniani.

Ni mtandao wenye watumiaji wengi na hata wenye mapato makubwa zaidi.

Kadiri siku zinavyokwenda, mtandao huu mkubwa, unazidi kununua mitandao mingine midogo midogo. Ni kama vile facebook inataka kutawala mitandao yote ya kijamii.

Tukiangalia ni kitu gani kinapoteza muda sana katika zama hizi, mitandao ya kijamii inaongoza. Inaonekana kama watu hawawezi kukaa dakika 30 bila ya kuchungulia kwenye mitandao ya kijamii. facebook, instagram na wasap, ni mitandao inayotumiwa sana, na yote ipo chini ya kampuni ya facebook.

Hivyo pamoja na mitandao hii kuwa inawapotezea watu muda, bado ndivyo watu wanavyozidi kuitumia. Hii ni kwa sababu mitandao hii imetengenezwa makusudi kabisa kuwafanya watu waitegemee kama sehemu ya maisha yao. Mtu aone asipoingia kwenye mtandao wa kijamii, kipo kitu kikubwa sana ambacho anakipoteza. Wakati siyo ukweli.

Kadiri watu wanavyopoteza muda wao kwenye mitandao hii ya kijamii, ndivyo mitandao hii inavyotengeneza faidia kubwa. Kwa sababu biashara kubwa ya mitandao hii ni kuuza matangazo, na bei ya matangazo inakuwa kubwa pale watu wengi wanapoona matangazo hayo.

Ili facebook iendelee kuwa kwenye biashara, lazima iendelee kuufanya mtandao wao kuwa tegemezi kwa wengi zaidi.

Sasa turudi kwako, unapoona watu wanapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii unafanya nini? Labda utakuwa unalalamika na kuona kwa nini watu hao wanafanya hivyo. Na vipi inapokuwa kwamba wewe mwenyewe ndiyo unapoteza muda kwenye mitandao hii?

Kwa nilichojifunza kwa uzoefu, hata uwapigie watu kelele kiasi gani, hawataacha kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii. Na hata ukiwashauri vipi, bado wataendelea kutembelea mitandao hii. Kwa sababu siyo makosa yao, bali nguvu ya mitandao hii ni kubwa sana kuweza kupingana nayo.

Hivyo basi, badala ya kulalamika kuhusu watu kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii, badala ya kulalamika kuhusu wewe mwenyewe kupoteza muda kwenye mitandao hii, kwa nini usianze kunufaika na mitandao hii?

Unajua ya kwamba unaweza kutengeneza kipato kupitia matumizi yako ya mitandao ya kijamii, tena kwa kuendelea kufanya kile ambacho unafanya sasa?

Hicho ndiyo nataka kukushirikisha hapa. Kwamba uache kulalamika kuhusu kupoteza muda, na badala yake utumie hiyo kama fursa ya kutengeneza kipato. Unachohitaji ili kutengeneza fedha kwenye mitandao hii, ni kuwepo kwenye mitandao hii, kitu ambacho tayari umeshafanya, kuwa na blog ambayo itakuwa nyumbani kwako na hatimaye uweze kuwauzia watu huduma na bidhaa zako.

Unahitaji kuwa na blog, na katika blog hiyo utakuwa unaweka maarifa na taarifa mbalimbali unazopenda kufuatilia. Kupitia taarifa na maarifa hayo, unatengeneza watu ambao wanapenda kufuatilia kazi zao, na baadaye unaweza kuwauzia bidhaa na huduma zako nyingine.

Ni kitu ambacho unaweza kukifanya huku unaendelea kufanya kile unachofanya sasa, na baadaye ukanufaika sana.

Anza sasa kubadili matumizi yako ya mitandao ya kijamii. Na kama utapenda ushauri zaidi wa namna ya kutumia mitandao ya kijamii kutengeneza kipato, nitumie ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253 na nitakupa mpango mzuri unaoweza kuutumia kutengeneza kipato.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK.

Makirita Amani,

Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Karibu sana kwenye MTAALAMU NETWORK uweze kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Kujua huduma za blog tunazotoa BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kusoma makala zetu za mbinu na maarifa ya kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Unapolalamika Kuhusu Mitandao Ya Kijamii, Umeamua Kupoteza Fursa Ya Kutengeneza Fedha.

  1. Pingback: Aina Mbili Za Watumiaji Wa Mtandao Wa Intaneti Na Upande Unaopaswa Kuwa Wewe. | MTAALAMU Network

Leave a Reply