Hivi Ndivyo Unavyoamua Kuwapoteza Wateja Wa Biashara Yako.

Siku za nyuma, mtu alipotaka ushauri juu ya jambo lolote, hasa pale anapokuwa anahitaji kununua bidhaa fulani, basi alianza kwa kuwauliza watu wengine. Aliuliza watu na baadaye kupata maoni na kuamua kuchukua hatua.

Lakini zama hizi, watu wanapotaka ushauri juu ya kitu, au kujua kitu kinapatikana wapi wanafanya nini? Unaweza kuanza kwa kujiuliza wewe mwenyewe, unapokuwa unataka kitu unaanza kutafutia wapi?

Jibu ni GOOGLE.

tafuta google

Google ndiyo imekuwa sehemu ya kwanza kabisa ya kujua chochote unachotaka kujua. Huhitaji kutumia muda mrefu, bali unachohitaji ni kwenda kwenye google na kutafuta kile unachotaka kupata.

Hii ina maana kwamba, wateja wa biashara yako, kabla hawajafanya maamuzi ya kununua, wanaingia kwanza google na kutafuta namna gani wanaweza kutatua matatizo yao, au kupata mahitaji yao. Ni kupitia google ndipo wanapata maelezo na kujua hatua zipi za kuchukua.

Hivyo basi, biashara yako pia inaweza kunufaika na kuwafikia wateja wengi zaidi, iwapo itakuwa kwenye mtandao wa intaneti. Iwapo watu wakitafuta kwenye google wanakutana na taarifa za biashara yako, inakuwa rahisi kwao kujua kuhusu wewe na kuweza kufanya biashara na wewe.

Njia bora kabisa ya biashara yako kuwa kwenye mtandao wa intaneti ni kwa wewe mfanyabiashara kuwa na blog inayoandika kuhusu biashara unayofanya. Hapa unakuwa na blog inayotoa maarifa na taarifa kuhusiana na biashara unayofanya, na hapo unalenga kutatua matatizo ambayo wateja wako wanakutana nayo yanayohusiana na biashara unayofanya.

Kwa mfano kama wewe ni mfugaji na hivyo unauza mazao ya ufugaji au huduma nyingine, unaweza kuwa na blog ambayo utaandika kuhusu ufugaji unaofanya, namna unavyopambana na changamoto unazokutana nazo na hata kuelezea bidhaa na huduma unazotoa na namna watu wanavyoweza kukufikia. Kama unafuga kuku, unaweza kuwa unaandika kuhusu ufugaji wa kuku, kuhusu vyakula vya kuku, magonjwa ya kuku na pia kuhusu mazao unayouza, kama mayai, vifaranga, kuku wenyewe na kadhalika. Sasa mtu anapokuwa na shida yoyote kuhusu kuku, anapoingia google na kutafuta, ataletwa kwenye blog yako na kusoma kile alichokuwa anatafuta. Ila hataishia hapo, ataendelea kuangalia mengine na atakutana na bidhaa na huduma zako nyingine.

Huo ni mfano mmoja wa ufugaji wa kuku, lakini kila aina ya biashara au kazi, ipo namna unavyoweza kuwafikia wateja wengi zaidi kwa kutumia blog yako.

Mfanyabiashara yeyote makini ni muhimu sana uwe na blog inayoelezea kuhusu biashara yako. Kukosa blog maana yake umeamua kuwapoteza wateja ambao wanatafuta suluhisho la matatizo yao kwenye mtandao wa intaneti.

Huhitaji uelewa mkubwa kuwa na blog, na wala huhitaji gharama kubwa ili kuwa na blog. Kama unahitaji blog bora kwa biashara yako, na ushauri zaidi wa namna ya kuiweka biashara yako kwenye mtandao tuwasiliane kwa simu 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Hivi Ndivyo Unavyoamua Kuwapoteza Wateja Wa Biashara Yako.

  1. Pingback: Kila Biashara Sasa Inahusisha Intaneti, Kama Bado Biashara Yako Haipo Kwenye Intaneti, Umechagua Kupoteza Wateja. | MTAALAMU Network

Leave a Reply