Unataka Fedha Au Unataka Likes? Makosa Unayofanya Kwenye Facebook Yanayokuzuia Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao.

Unapoweka ujumbe au picha kwenye facebook, na hakuna mtu hata mmoja anakuwa amebonyeza like unajisikiaje?

Na je pale unapoweka ujumbe au picha na waka like watu 100 na zaidi, unajisikiaje?

Kama umeweka jumbe mbili siku moja, mmoja haujapata likes, mwingine umepata likes nyingi, kesho unaweka ujumbe unaoendana na upi? Wenye likes au usio na likes?

Kwa hali ya kawaida kabisa ya ubinadamu, utaweka ujumbe unaoendana na ule wenye likes nyingi. Hii ndiyo maana ukiangalia jumbe na picha za wadada wengi kwenye mtandao wa facebook, ni zinazowaonesha katika mazingira ya urembo, lakini siyo kwamba maisha yao kila wakati yako kwenye hali hiyo.

facebook likes

Hivyo umekuwa unapenda sana likes, na kadiri unavyopata likes nyingi ndivyo unavyoweka jumbe za aina ile inayokuletea likes. Na wengine wamekwenda mbali zaidi, wanawaambia marafiki zao kama hulike au kucoment kwenye jumbe zangu nitakufuta urafiki!

Sawa, tuachane na hayo, nataka nikupe ujumbe wa leo, ambao ni huu LIKES KWENYE FACEBOOK HAZINA MAANA YOYOTE. Sijui kama umenielewa sawasawa, wacha nirudie kusisitiza, yaani zile likes unaona watu wanakupa kwenye jumbe na picha zako, hazina maana yoyote, kwako au hata kwao. Wamejikuta wakibonyeza tu wakati wa kupita. Kama unabisha hili, niambie tarehe kama ya leo ya mwezi uliopita uli like jumbe gani, au waulize wale ambao wamelike jumbe zako kwa nini wali like. Utaona ukweli ulivyo.

Ujumbe mkubwa ninaotaka kukupa leo ni kwamba, unapofanya biashara kwenye mtandao, kwa kutumia blog na mitandao ya kijamii, likes siyo kitu. Unapotaka kupima kukubali kwa watu kwenye chochote unachouza kwa njia ya mtandao, usiangalie likes. Watu wengi husahau dakika chache baada ya kulike.

Hivyo unachohitaji kufanya wewe, siyo kuandika vitu ambavyo watu watalike, bali kuandika vitu ambavyo vitawafanya watu wachukue hatua. Wakutafute kwa ajili ya kupata zaidi au kujua zaidi. Wawaambie wengine, na watafute kujifunza zaidi kupitia wewe. Sasa kama vitu hivyo vitakuwezesha kuwa na likes nyingi, hapo upo vizuri sana. Lakini kama watu wanalike halafu hawakutafuti au kununua vile unavyouza, kuna tatizo mahali, na siyo tatizo la watu hao, bali tatizo lako.

Sehemu kubwa ya tatizo huwa ni mtu kuwa amechagua watu ambao siyo sahihi kwake. Mtu anachagua kuwafurahisha wengi na kusahau kuchagua wateja wachache ambao atawahudumia vizuri kwa kuwapa maarifa na taarifa sahihi.

Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakiandika vizuri kwenye mitandao ya kijamii, na kupata likes na coments nyingi. Huwa nawashauri wawe na blog na waweke maandishi yao kwenye blog zao pia, au zaidi kuliko hata kwenye facebook. Sasa wanapojaribu hilo, wanagundua likes zinapungua. Sasa kwa kuwa wanachotaka ni likes, wanaachana na blog na kuweka muda wao wote kwenye facebook. Wanazipata likes, ila wanakosa fedha kwa sababu sehemu nzuri ya kutengeneza fedha kwenye mtandao ni kwenye blog na email, na siyo kwenye mitandao ya kijamii kama facebook.

Hivyo unapoandika kwenye blog na kuwashirikisha watu facebook, ukapata likes chache, usikate tamaa na kuacha, badala yake chagua watu gani unaoweza kuwasaidia na maarifa na taarifa zako na endelea kuwapa kile wanachohitaji. Weka ubora kwenye kazi yako na utawavutia wale muhimu kwako.

Usilewe likes na kusahau kuwabadili wafuasi wako kwenye mitandao kuwa wateja wako. Na hatua ya kwanza ya kuwabadili wafuasi hao ni kuwa na blog ambayo utawakaribisha, na baadaye ukajenga nao mahusiano bora zaidi na baadaye kuwazuia huduma na bidhaa zaidi.

Lakini je blog unayo? Kama unayo vizuri, weka juhudi huko. Kama blog huna, basi karibu sana upate blog itakayounganishwa na mitandao yako ya kijamii na uanze kuzigeuza likes kuwa fedha. Tuwasiliane kwa simu 0717396253 kupata blog bora kabisa kwako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply