Kama Unataka Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao, Jukumu Lako Kubwa Ni Hili.

Swali siyo kama inawezekana au la kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, hilo linafahamika kwamba mtandao wa intaneti ni njia moja na ambayo ipo wazi kwa kila mtu kuweza kutengeneza kipato.

Swali ni unawezaje kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti kwa kuanzia pale ulipo sasa, kwa utaalamu, ujuzi, uzoefu au chochote ambacho wewe binafsi unapenda kufanya.

Na hapa ndipo mimi nimekuwa nakupa maarifa mbalimbali ya kufanya hivyo kuputia mtandao wa www.mtaalamu.net/pesablog Kusudi langu ni wewe uweze kutumia mtandao wa intaneti kwa faida, uache kushabikia tu wengine na wewe unufaike. Uache kushangilia wamiliki wa mitandao hii kuwa mabilionea wakiwa vijana wadogo, na wewe uanze kunufaika na sehemu ya mabilioni hayo ya mtandao wa intaneti.

Ambacho nimekuwa nakuambia mara zote, huhitaji kitu kikubwa sana ambacho huna sasa ili kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti. Unahitaji kuanzia hapo ulipo sasa, ukiwa unafanya kile ambacho umekuwa unafanya, ila sasa ukiwa na mtazamo tofauti kidogo.

Iwapo unataka kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, basi jukumu lako kubwa ni hili; KUFANYA MAISHA YA WENGINE KUWA BORA ZAIDI. Tunaweza kuishia hapo na ukaanze kuweka kazi, kwa sababu hakuna la ziada zaidi ya hilo. Fanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi. Mara zote kuwa wa msaada kwa wengine, kupitia kile ambacho unafanya sasa.

Sasa hizi maisha ya watu yamehamia kwenye mtandao wa intaneti. Watu wengi wanatumia mtandao kwa muda mwingi zaidi kwenye maisha yao. Sasa hivi mtu kukaa nusu saa hajashika simu yake na kuingia kwenye mtandao, ni vita kubwa sana ambayo wachache ndiyo wanaweza kuishinda.

Kwa maisha kuhamia kwenye mtandao, hii ina maana hata mahitaji ya watu wanayatafuta kwenye mtandao, chochote wanachotaka kujifunza wanaanzia kwenye mtandao. Na hapo ndipo wewe una nafasi ya kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kwa kuwapa maarifa na taarifa zinazowawezesha kufanya maamuzi bora kwa maisha yao.

Unahitaji kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuwa shirikisha watu maarifa yanayoendana na kile ambacho unafanya au unafuatilia, yatakayowawezesha kufanya maamuzi bora zaidi. Ukishafanya hivyo, unahitaji kujua namna ya kuwafikia wale wanaojali kile unachofanya.

Writing Message On Smartphone

Ili kufanya hili, unahitaji kuiweka vizuri mitandao yako ya kijamii unayotumia, ili watu wanapotembelea wajue pale wanapata kitu fulani. Na muhimu zaidi unahitaji kuwa na BLOG ambayo hii ndiyo itakuwa nyumbani kwako kwenye mtandao wa intaneti. Watu wanapokuwa wanatafuta kitu chochote kinachohusiana na yale unayowashirikisha watu wewe, ataletwa moja kwa moja kwenye blog yako. Kwenye blog atajifunza zaidi na atapenda kupata mengi kutoka kwako, ikiwa ni pamoja na kupata huduma muhimu unazotoa.

Hivyo rafiki yangu, chochote unachofanya kwenye mitandao ya kijamii na mtandao wa intaneti kwa ujumla, hakikisha unakuwa wa msaada kwa wengine. Unafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi na wao watakuwa tayari kukufuatilia na pia kununua kutoka kwako chochote unachouza.

Usisahau kuweka vizuri mitandao yako ya kijamii na pia kuwa na blog itakayokuwa nyumba yako. Kama unahitaji ushauri wa kina kwenye hili, pamoja na kupata blog, tuwasiliane kwa simu 0717396253, wasap itakuwa njia bora zaidi.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Kama Unataka Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao, Jukumu Lako Kubwa Ni Hili.

  1. Pingback: Zingatia Misingi Hii Mitatu(03) Ya Kutengeneza Kipato Kwenye Mtandao Wa Intaneti. | MTAALAMU Network

Leave a Reply