Aina Mbili Za Watumiaji Wa Mtandao Wa Intaneti Na Upande Unaopaswa Kuwa Wewe.

Kuna aina mbili za watumiaji wa mtandao wa intaneti, na aina moja kati ya hizo ndiyo inanufaika sana na mtandao huu.

Aina ya kwanza ni ya watazamaji, hawa ni walaji wa kila kinachozalishwa kwenye mtandao wa intaneti. Wanachofanya wao ni kufuatilia kila kinachoendelea, na wanachoweza kufanya ni kupenda, kuchukia au kuchangia kwenye kile ambacho wanaona. Kundi hili hawanufaiki chochote kifedha, zaidi ya raha ya muda mfupi, na wakati mwingine chuki na wivu hasa pale wanapoona maisha ya wengine ni mazuri kuliko yao.

Aina ya pili ni wafanyabiashara, hawa ni wazalishaji wa kile ambacho watu wanafuatilia kwenye mtandao wa intaneti. Wanachofanya hawa ni kuzalisha taarifa na maarifa ambayo wengine watayafuatilia na hatimaye kuweza kuwauzia vitu ambavyo wanauza. Kundi hili linanufaika sana kifedhakwenye mtandao wa intaneti.

Katika makundi haya mawili, unapaswa kuwa kwenye kundi la wafanyabiashara, wale wanaozalisha maarifa na taarifa ambazo zinafuatiliwa na wengine, na baadaye kuweza kutengeneza kipato.

Huhitaji kuwa na kitu kikubwa ili kuwa kwenye kundi la wafanyabiashara kwenye mtandao, unachohitaji ni kuchagua eneo ambalo unaweza kuwapa watu taarifa na maarifa yanayowawezesha kufanya maamuzi bora kabisa kwenye maisha yako. Baada ya hapo unahitaji kuandaa bidhaa au huduma ambayo unaweza kuwauzia watu na wakanufaika zaidi.

SOMA;Unapolalamika Kuhusu Mitandao Ya Kijamii, Umeamua Kupoteza Fursa Ya Kutengeneza Fedha.

Sasa kazi yako kubwa inakuwa kutumia mtandao wa intaneti kutoa maarifa na taarifa zako kwa watu. Kutengeneza wasomaji na wafuatiliaji wa taarifa zako. Kuwa na blogu ambayo ina taarifa zote unazotoa, na zaidi. Kuwa na mfumo wa email ambapo unawasiliana kwa karibu zaidi na wasomaji wako. Kwa njia hii unakuwa umejenga biashara yako kwenye mtandao wa intaneti. Kitu ambacho kila anayeamua kufanya, anaweza kufanya.

Unachagua kuwa kwenye kundi lipi? Kama unataka kuwa kwenye kundi la wafanyabiashara, basi anza kuchukua hatua sasa. kama huna blogu ya kuanzia, tuwasiliane kwa wasap 0717396253. Karibu sana.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply