Usitangaze Biashara Yako Kwenye Blog Za Wengine, Badala Yake Fanya Hivi.

Watu wengi wamekuwa wakiniandikia wakitaka kutangaza biashara zao mbalimbali kupitia blog ninazoendesha mimi. Nimekuwa nawajibu kwamba sitoi huduma hiyo ya matangazo kwa biashara za watu. Wapo ambao wamekuwa wanashangaa kwa nini nikatae fedha za watu walio tayari kutangaza biashara zao.

Jibu langu limekuwa ni moja, watu wanapotembelea blog zangu, hawafanyi hivyo ili kuja kukutana na matangazo ya vitu. Bali wanatembelea ili kupata maarifa fulani ambayo wanayahitaji kwenye maisha yao, kazi zao na hata biashara zao. Hivyo kipaumbele chao cha kwanza siyo matangazo wala kununua, kwanza ni kupata maarifa, halafu wakiona wanahitaji zaidi, wanaweza kununua huduma nyingine ninazotoa mimi, kama vitabu, ushauri na kadhalika.

Hivyo mtu yeyote kuja kutangaza biashara yake kwenye blog zangu, atakuwa anapoteza fedha zake. Hatapata sawasawa na alichowekeza. Kwa sababu watu hawaweki kipaumbele kwenye matangazo yanayowekwa, bali kwenye kile wanachotaka wao.

Kama umewahi kutembelea baadhi ya blog zenye matangazo mengi, hebu niambie ulichofanya wewe ni nini? Ulianza kupitia tangazo moja moja mpaka umalize yote au uliyavuka yote na kwenda kusoma kile kilichokupeleka? Jibu unalo, maana unajua huwa unafanya nini. Sasa kwa nini unafikiri mtu mwingine ataacha shughuli zake na kuanza kuangalia matangazo yako uliyoweka kwenye blog za wengine?

Badala ya kupoteza fedha na muda wako kutangaza biashara yako kwenye blog za wengine, nakushauri uwe na blog yako mwenyewe, inayohusu biashara yako, kama upo makini na biashara yako.

SOMA;Kila Biashara Sasa Inahusisha Intaneti, Kama Bado Biashara Yako Haipo Kwenye Intaneti, Umechagua Kupoteza Wateja.

Kupitia blog hii utakuwa unatoa taarifa, maarifa na mafunzo mbalimbali yanayohusiana na biashara yako kwa wasomaji wako, na kupitia njia hiyo wasomaji wako wanakuamini na kukuchukulia wewe ni mtaalamu wa eneo hilo unaloandikia. Kupitia blogu yako, wasomaji watahitaji ushauri zaidi kuhusiana na vitu vinahusiana na biashara yako, na hapo ndipo unapata nafasi ya kuwaeleza huduma na bidhaa wanazoweza kuzipata kupitia biashara yako.

Ukiwa na blog yako usiitumie kama sehemu ya kutangaza tu biashara yako, bali itumie kama sehemu ya kuwasiliana na wateja wako. Sehemu ya kuwapa maarifa zaidi, sehemu ya kujenga mahusiano na sehemu ya kuwashauri zaidi kuhusiana na bidhaa au huduma unazotoa.

Kwa kuwa na blogu na kuikuza, utatengeneza wasomaji waaminifu kwako, na ambao watakuwa tayari kununua kwako, kwa sababu wanajali na wanakuamini.

Anzisha blog yako sasa siyo vigumu kama unavyofikiri, na wala huhitaji kuweka gharama kubwa au nguvu kubwa kwenye kuianzisha. Ni kutenga kiasi cha muda kila siku, kuwashirikisha wasomaji wako maarifa muhimu na kuendelea kuwaeleza kuhusu bidhaa na huduma unazotoa. Kama ungependa kuwa na blog yako leo wasiliana na mimi kwa njia ya wasap 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Usitangaze Biashara Yako Kwenye Blog Za Wengine, Badala Yake Fanya Hivi.

  1. Pingback: Sababu Mbili Kwa Nini Watu Wapo Online Na Jinsi Ya Kuzitumia Kibiashara. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Zingatia Mambo Haya Matatu Unapoandaa Tangazo La Chochote Unachouza. | MTAALAMU Network

Leave a Reply