Naweza Kumsaidia Nani? Naweza Kumsaidia Nini? Njia Ya Kupata Mawazo Ya Kuandika.

Kuna wakati kama mwandishi unakosa kabisa kitu cha kuandika. Hapo umeshapanga kwamba kila siku lazima uandike, iwe ni kitabu au makala. Lakini siku inafika, upo tayari kuandika, unaishia kuangalia tu pale unapoandika, hakuna kinachokuja kwa ajili ya kuandika. Kwa dunia ya sasa, mwandishi atakimbilia haraka kutafuta usumbufu kwenye mitandao ya kijamii, labda kuangalia facebook, labda atapata kitu cha kaundika. Lakini ni mara chache sana usumbufu huo utamsaidia.

Njia bora kabisa ya kupata wazo la kuandika, pale ambapo huna cha kuandika, ni kujiuliza maswali haya mawili muhimu;

Naweza kumsaidia nani?

Naweza kumsaidia nini?

Kwa mfano leo sikuwa na kitu naweza kuandika hivyo nikajiuliza maswali hayo mawili.

Naweza kumsaidia nani?

Jibu limekuja kwamba naweza kumsaidia mwandishi ambaye amekwama, anataka kuandika lakini mawazo ya kuandika hayamjii haraka. Anakazana lakini anaona hakuna cha kuandika. Anakaribia kukata tamaa na kuacha akafanye mambo mengine.

Naweza kumsaidia nini?

Naweza kumsaidia njia ya kumfanya apate mawazo ya kuandika, pia ninaweza kumsaidia kujenga nidhamu ya kutokimbilia usumbufu kama mitandao ya kijamii. Pale anapojishawishi kwamba bora aache, hapo ndipo nataka awe na nidhamu ya kutokuacha, na aweke akili na mawazo yake pale mpaka atakapopata cha kuandika.

Nina imani hili limekuwa la msaada kwako. Sasa ni zamu yako kuwaangalia wasomaji wako, kuona wamekwama wapi na wewe unaweza kuwasaidia wapi.

SOMA;Jinsi Unavyoweza Kupata Mawazo Ya Kuandika Makala Kila Siku Kwenye Blog Yako.

Ukitaka kukosea hili, fikiria watu wengi, utakwama tena. Ukitaka kupatia hili, fikiria mtu mmoja, lazima utapata unayeweza kumsaidia.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Naweza Kumsaidia Nani? Naweza Kumsaidia Nini? Njia Ya Kupata Mawazo Ya Kuandika.

  1. Pingback: Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuandika. | MTAALAMU Network

Leave a Reply