Andika Kitabu Ambacho Ungependa Kukisoma, Lakini Bado Hujakipata.

Hakuna kitu ambacho nimekuwa nasisitiza kama kujitofautisha katika uandishi. Kwa sababu hakuna kifo cha haraka kwenye uandishi kama kuiga kile ambacho wengine wanaandika. Na kama ambavyo nimekuwa nasema, kama unamwiga mtu mwingine, kwa nini watu wakusome wewe na kuacha yule ambaye unaiga kwake? Hili ni swali ambalo ukilifikiria kila wakati, utafanya kitu tofauti.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye uandishi wa vitabu. Unapoandika kitabu, ambacho kinafanana na kilichopo sokoni tayari, unafikiri kwa nini watu waache kusoma kitabu kingine na kusoma ulichoandika wewe? Au kwa nini watu wanunue kitabu kingine wakati tayari wana kitabu kinachofanana na hicho unachotoa wewe? Swali muhimu mno kujiuliza kabla hujaandika kitabu.

Hivyo basi, ili uandike kitabu ambacho watu watakisoma na kunufaika nacho, kwanza soma vitabu vingi kwenye lile eneo unaloandikia. Jifunze kwa kina na ona ni kitu gani ulitaka kujifunza lakini hujapata kwenye vitabu vingi. Labda kuna kitu ulitaka sana kupata kukijua kwa undani, lakini kwenye kila kitabu ulichosoma hakijaelezwa vizuri. Hapo sasa ni pazuri wewe kuandikia kitabu.

Hivyo unaweza kukaa chini na kufanya utafiti wa kina, na kuja na majibu ambayo uliyakosa kwenye vitabu ulivyosoma. Hapo sasa unakuwa na kitabu ambacho wengi wakikisoma watapata kitu cha tofauti. Watapata kitu ambacho hawawezi kukipata kwenye kitabu kingine.

SOMA;Sababu Moja Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuwa Na Blog, Hata Kama Hutaki Kipato Mtandaoni (NA ZAWADI YA KITABU BURE.)

Ukitumia njia hii ya kuandika kitabu ambacho unataka kukisoma, haitakuwa kazi kwako kujua uandike kitabu gani. Na muhimu zaidi, utaandika kitabu kinachoendana na wasomaji ulionao.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Andika Kitabu Ambacho Ungependa Kukisoma, Lakini Bado Hujakipata.

  1. Pingback: Kwa Nini Watu Wakusome Wewe, Kwa Nini Wakusikilize Wewe? | MTAALAMU Network

Leave a Reply