Kuwa Halisi, Simamia Kile Unachojua Na Kuamini Kupitia Uandishi Wako.

Dunia inataka uwe kondoo, ufanye kile ambacho kila mtu anafanya, na hapo hakuna atakayekuhoji. Ila pale unapochukua hatua ya kusimamia kile unachoamini, ambacho kipo tofauti na wengi wanavyoamini, jiandae kupingwa, kudhihakiwa, kukatishwa tamaa na hata kukataliwa.

Hilo limekuwa linawafanya waandishi wengi kuishi maisha ya maigizo, kuandika vitu ambavyo hawaviamini wala kusimamia, ili tu wapate kukubalika na wengine. Au hata waweze kuuza na kupata wateja kwa huduma zao nyingine. Japokuwa njia hiyo inaweza kuwa na matokeo mazuri ndani ya muda mfupi, matokeo yake kwa muda mrefu ni mabaya.

Kwa kuandika kile ambacho hukiamini, bali tu unataka kukubalika, inafika hatua na kujiona huna thamani. Kwa sababu ukishaanza kuigiza, inabidi uendelee kuigiza ili usiwachanganye watu. Na hapo ndipo unapokuwa na maisha yenye sura mbili, ambayo ni magumu sana kuishi.

Amua kuwa halisi, amua kuandika kile unachoamini, na unachokijua kweli, hata kama wengine hawakubaliani nacho. Kuwa tayari kupingwa, kukosolewa na kukataliwa. Lakini kumbuka, wapo watu wanaoamini kama unavyoamini wewe. Na hao watakuchukulia wewe kama shujaa wao, kwa kuweza kuwasemea. Watu hawa wataungana na wewe, na watakuwa wafuasi wako.

SOMA;Tengeneza Sauti Yako Na Mtiririko Wako Wa Uandishi.

Kuchagua kuwa mkweli na kuishi maisha yako, hakutakupa mashabiki wengi haraka, lakini kutakuwezesha wewe kuwa na mashabiki wa ukweli ambao utaenda nao muda mrefu. Pia utakuwa na maisha halisi popote unapokuwa, hivyo hutokuwa na haja ya kufanya maigizo ya aina yoyote ile.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

3 thoughts on “Kuwa Halisi, Simamia Kile Unachojua Na Kuamini Kupitia Uandishi Wako.

  1. Pingback: Hivi Ndivyo Unavyopaswa Kukuza Huduma Yako Ya Uandishi… | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Tenga Muda Wa Kutosha Kutangaza Kazi Yako Ya Uandishi, Hakuna Atakayekufanyia Hilo. | MTAALAMU Network

  3. Pingback: Soma Maandiko Ya Miaka Mia Tano Iliyopita, Na Utajifunza Kitu Hiki Kikubwa Sana. | MTAALAMU Network

Leave a Reply