Njia Tano Za Kuanza Kukuza Email List Yako Kupitia Blog Na Mitandao Ya Kijamii.

Kama wewe ni mwandishi ambaye unatumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii na huna email list, yaani orodha ya wasomaji wako ambao wanapokea maandiko yako moja kwa moja kwenye email zao, basi huutendei haki uandishi wako. Kwa sababu kwenye uandishi, email list ndiyo sehemu pekee ya kujenga mahusiano mazuri na wasomaji wako na hatimaye kuwa wafuasi wako wa karibu.

Hivyo ni muhimu sana kwa kila mwandishi kuwa na email list, ambayo ataitumia kujenga ukaribu na wasomaji wake, na hatimaye kuitumia kuuza huduma na bidhaa zake nyingine moja kwa moja kwa wasomaji wake.

Sasa ukishakuwa na email list, kazi muhimu ni kuikuza ili uwe na wasomaji wengi waliojiandikisha kwenye orodha hiyo. Hapa nakupa njia tano za kukuza list yako.

  1. Weka fomu kwenye blog yako.

Hakikisha kwenye blog yako kuna fomu ya watu kuweza kujiunga na email list yako. Kuwa na ukurasa maalumu wenye kichwa cha jiunge na mtandao huu au jiunge na mimi, na hapo mtu anaweza kujaza taarifa zake ili kupokea mafunzo zaidi. Unaweza pia kuwa na fomu ambayo inafunguka kabla mtu hajafungua makala (pop up), japo hii inaweza kuwasumbua na kuwakera watu, ila unaweza kuitumia kwa muda.

  1. Weka fomu kwenye facebook.

Mtandao wa kijamii wa facebook, kupitia ukurasa uliofungua, unaweza kuweka fomu moja kwa moja. Kwa njia hii, msomaji wako anayekujua kupitia mtandao wa facebook anaweza kujiunga moja kwa moja, hata kama hajatembelea blogu yako. Ni rahisi kufanya hivyo na unawafikia watu wengi zaidi. Kama tunavyojua, mtandao wa facebook una wafuatiliaji wengi.

  1. Toa zawadi ambayo watu wanaipata kwa kujiandikisha.

Ili kuwavutia wasomaji wako kujiunga na email list yako, unapaswa kutoa zawadi ambayo wataipata kwa kujiunga na email list yako. Zawadi hiyo inaweza kuwa kijitabu kidogo ulichokiandaa kwa mfumo wa pdf na unawatumia wakishajiunga. Hiyo itawapa sababu ya kujiunga ili kupata kile unachotoa.

SOMA;Makala kwa Email

  1. Wakumbushe mwisho wa makala.

Kila mwisho wa makala unayoandika, wakumbushe wasomaji wako kujiunga na email list yako. Weka link au fomu ya kujiunga mwisho wa makala, ambapo msomaji ataweza kufungua au kujiunga moja kwa moja.

  1. Andaa makala zitakazotolewa kwa email pekee.

Njia nyingine bora ya kukuza email list yako ni kuwa na aina za makala au kipengele ambacho utatuma kwenye email pekee. Unaweza kutenga siku fulani ya wiki na kuwaambia wasomaji wako kwamba wakijiunga kila siku fulani ya wiki watapokea makala kutoka kwako. Na hakikisha unatimiza kile ambacho umekiahidi.

Tumia kila fursa unayoiona kuhakikisha wasomaji wako wanajiunga na email list yako. Na wakishajiunga watumie makala nzuri zenye msaada kwako, zitakazowafanya waendelee kuwa na wewe na kukuamini zaidi.

Kama mpaka sasa huna email list, karibu nikusaidie kuandaa email list nzuri na kukuwekea kwenye blog na mtandao wa facebook. Tuwasiliane kwa wasap namba 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Njia Tano Za Kuanza Kukuza Email List Yako Kupitia Blog Na Mitandao Ya Kijamii.

  1. Pingback: Kama Wewe Una Taaluma Au Uzoefu Wowote Ambao Watu Wanauhitaji, Unafanya Kosa Kubwa Sana Kama Huna Blog. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Chagua Tatizo Unaloweza Kuwasaidia Watu Kutatua Kupitia Maarifa Sahihi. | MTAALAMU Network

Leave a Reply