Kwa Nini Watu Wakusome Wewe, Kwa Nini Wakusikilize Wewe?

Urahisi wa kuingia kwenye fani yoyote ile, hasa kwenye zama hizi za maendeleo ya teknolojia, yamepelekea kila mtu kuweza kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.

Kwa mfano, urahisi wa kirekodi sauti na kutuma kwa watu wengi, inampa kila mtu nafasi ya kuweza kuwa mtangazaji, hata kama hana redio.

Urahisi wa kuandika kupitia mitandao ya kijamii, unamfanya kila mtu aweze kuwa mwandishi, hata kama hajasomea uandishi.

Urahisi wa kurekodi video kwa kutumia simu na kuweza kusambaza kwenye mitandao, unamfanya kila mtu kuwa na kipindi cha tv, hata kama hana tv.

Hivyo changamoto kubwa ya zama hizi ni kwa nini watu wakusikilize wewe, wakusome wewe na hata kukuangalia wewe, ikiwa wapo wengine wengi ambao wanafanya kama wewe?

Hili ni swali ambalo wewe unapaswa kujiuliza kila mara, na upate majibu, ili kuhakikisha unatengeneza kitu ambacho kinawafanya watu wakufuatilie.

Kwanza kabisa, sahau kuhusu kumpata kila mtu, kwa sababu watu wengi wamekuwa wakijaribu kuandika au kutoa kitu ambacho kitamfaa kila mtu. Kwa ulimwengu tunaoishi sasa, hilo ni zoezi gumu na ambalo halina faida yoyote kwa anayelifanya.

SOMA;Andika Kitabu Ambacho Ungependa Kukisoma, Lakini Bado Hujakipata.

Pili, chagua watu ambao unajua unaweza kuwatatulia changamoto zao, tofauti kabisa na wengine wanavyozitatua. Hapa ndipo unahitaji kuchagua kitu ambacho utakiandikia au kukisemea kwa undani kabisa kiasi kwamba mtu akikusoma, au akikusikiliza, anaona matumaini mapya na makubwa kwake. Anaona suluhisho la changamoto zake, na anaweza kuchukua hatua bora kwake.

Kwa njia hii, ndiyo unaweza kuwatengeneza watu ambao wanakuwa wafuasi wako, ambao utawahudumia vizuri na hata kuwa wateja wa bidhaa na huduma zako nyingine.

Usijaribu kuiga kile ambacho wengine wanafanya, utateseka na hakuna atakayejali. Wapo wengi wanaofanya mambo yale yale, na hakuna anayesumbuka kuangalia yale yanayofanywa na kila mtu.

Jiweke tofauti, chagua kundi la watu ambao unaweza kusema nao vizuri, kisha weka kazi kubwa kuhakikisha unawapa kile ambacho kitawasaidia.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Kwa Nini Watu Wakusome Wewe, Kwa Nini Wakusikilize Wewe?

  1. Pingback: Kazi Ambayo Haijakamilika Haivutii, Hivyo Jipe Ruhusa Ya Kuandika Kitu Kibovu. | MTAALAMU Network

Leave a Reply