Kazi Ambayo Haijakamilika Haivutii, Hivyo Jipe Ruhusa Ya Kuandika Kitu Kibovu.

Kama umesoma somo la sayansi shule ya msingi na baiolojia shule ya sekondari, utakuwa umesoma uzazi kwa wanadamu. Utakuwa umejifunza kuhusu kutungwa kwa mimba mpaka mtoto anapozaliwa. Na kama utakuwa unakumbuka vizuri, katika hatua mbalimbali za mimba, sura ya mtoto unaweza usiijue kabisa, kina kuwa kitu cha ajabu ambacho huwezi kukipenda. Lakini miezi tisa inapofika, anakuwa amekamilika mtoto, ambaye ana sura nzuri na unaweza kumbeba na kufurahia.

Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye kazi zetu za uandishi. Kazi yoyote ambayo haijakamilika, huwa haivutii, huwa ni mbovu na inayokatisha tamaa. Lakini kazi inapokamilika, inakuwa nzuri na watu wanaifurahia.

Ni muhimu kujua hili kwa sababu linatusaidia sana kwenye uandishi, linakupa ruhusa ya kuanza kuandika kitu kibovu, kitu kibaya ambacho hakimvutii mtu yeyote. Kadiri unavyokwenda unaendelea kuboresha, unaongeza na kupunguza vitu. Mpaka kufika mwisho, unakuwa na kitu kizuri ambacho mtu akisoma anafurahia.

Mara nyingi huwa nasema tapia kila kilichopo kwenye mawazo yako kwenye kurasa unazoandika. Andika bila ya kuwa na wasiwasi wowote wala kujihukumu. Andika kila unachofikiria, iwe ni makala au kitabu. Kisha hifadhi kile ulichoandika kwa muda, baadaye rudi sasa kuanza kusoma, ukiongeza na kupunguza kadiri utakavyoona inafaa.

SOMA;Kwa Nini Watu Wakusome Wewe, Kwa Nini Wakusikilize Wewe?

Zoezi hili linahitaji muda, kama ambavyo ukuaji wa mimba unahitaji muda. Lakini muda huo unapowekwa, mwishoni tunapata kitu kizuri.

Usijizuie kuandika kwa sababu huna kitu kizuri cha kuandika, mwaga mawazo yako yote kwenye kurasa unazoandika, kisha anza kuboresha hatua kwa hatua.

Unasubiri nini usianze kuandika sasa hivi hiyo makala ambayo umekuwa unafikiria kuandika? Kwa nini usianze kuandika leo kitabu unachotembea nacho kwenye mawazo yako? Hakuna atakayeona ubovu wa mwanzo, kama ambavyo mimba inafichwa kwenye tumbo la uzazi mpaka mtoto anapokamilika.

Anza sasa, weka kila ulichonacho na endelea kuboresha kadiri muda unavyokwenda. Mwisho wa siku utakuwa na kazi bora na inayowasaidia wengi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Kazi Ambayo Haijakamilika Haivutii, Hivyo Jipe Ruhusa Ya Kuandika Kitu Kibovu.

  1. Pingback: Andika Hichi Pale Ambapo Huna Kabisa Kitu Cha Kuandika. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Unachoandika kitasomwa miaka mingapi kutoka sasa? | MTAALAMU Network

Leave a Reply