Sababu Mbili Kwa Nini Watu Wapo Online Na Jinsi Ya Kuzitumia Kibiashara.

Unapotumia mtandao wa intaneti kama njia yako ya kutengeneza kipato, kupitia kazi zako mbalimbali, lazima uweze kujibu swali hili muhimu sana; kwa nini watu wapo online? Yaani nini kinawapelekea watu kuingia kwenye mtandao wa intaneti?

Na hili unaanza kulijibu kwa kuangalia tabia zako binafsi, kwa kuangalia kinachokufanya wewe uwe kwenye mtandao.

Kwa utafiti niliofanya, kuanzia mimi binafsi na watu wengine, zipo sababu kuu mbili kwa nini watu wapo online.

Sababu ya kwanza ni kupoteza muda.

Ndiyo, pamoja na umuhimu na uhaba wa muda, lakini hebu niambie unapotaka kupoteza muda unafanya nini? Unaingia kwenye mtandao wa intaneti, hasa mitandao ya kijamii, ukipanga kudhurura kwa dakika kadhaa. Labda ni mapumziko mafupi umepata kwenye kazi yako, au umefika wakati unataka kulala, unaweza kusema upitie kidogo mtandaoni kuangalia nini kinaendelea. Kwa kuwa kuangalia nini kinaendelea hakuna matokeo ya maana sana, basi ni kupoteza muda.

Unaweza kutumia hili kuhakikisha watu wanapoingia kupoteza muda basi wanakutana na wewe. Na hapa ni muhimu sana ujue watu wanapoteza zaidi muda kwenye mtandao katika nyakati zipi. Mara nyingi asubuhi kabla kazi hazijaanza, mchana wakati wa chakula na jioni baada ya kazi, watu wengi huwa kwenye mitandao. Hivyo unaweza kutumia muda huo kufanya kitu ambacho unataka kiwafikie wafuasi wako kwenye mitandao ya kijamii. Kama ni makala unaandika na kuwashirikisha watu, basi unapaswa kufanya hivyo wakati ambao watu wengi wanaweza kuiona. Japo hili siyo la uhakika sana, litakusaidia kuwafikia watu wengi zaidi.

SOMA;Usitangaze Biashara Yako Kwenye Blog Za Wengine, Badala Yake Fanya Hivi.

Sababu ya pili ni kutafuta njia ya kutatua tatizo.

Muda wowote unapokuwa na shida ni hatua ipi ya kwanza huwa unachukua? Kama kuna kitu unataka kujua au kujifunza, kwa dunia ya sasa, hatua ya kwanza ni google. Unatafuta taarifa za kitu hicho kwenye mtandao. Hivyo kutafuta njia ya kutatua tatizo fulani, ni sababu nyingine inayowapeleka watu online.

Kwa kujua hili, inakusaidia kujiweka kwenye mfumo ambao kila mwenye tatizo ambalo wewe unatatua, basi anakufikia wewe. Mtu anapoingia google na kutafuta kitu kinachohusiana na kile unafanya wewe, basi moja kwa moja aletwe kwako. Zamani kuna kitu kilikuwa kinaitwa SEARCH ENGINE OPTIMIZATION (SEO), ilikuwa ni njia ya kuweka maneno fulani fulani kwenye blog yako ili watu wakiyatafuta wafike kwenye blog yako. Mpaka sasa bado njia hiyo ipo, ila haina tena nguvu kama zamani. Na nguvu pekee iliyopo sasa, ni wewe kuwa na makala nyingi, na mpya mpya zaidi kuhusiana na kile ambacho mtu anatafuta. Mtandao wa google unapotafuta, unaangalia kwenye yale maeneo ambayo kitu kinachotafutwa kipo kwa wingi, na pia ni cha siku za karibuni. Hivyo unahitaji kuwa na makala nyingi zenye utatuzi wa matatizo ambayo watu wanatafuta suluhisho, na makala hizo ziwe mpya mara kwa mara.

Ukiweza kutumia njia hizi kuu mbili, kila wakati utawafikia watu wengi na wengi wakajua kazi zako na kununua kile ambacho unawauzia kupitia mtandao wa intaneti na blogu yako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply