Usiandike Kwa Sababu Hizi, Utajipoteza Wewe Mwenyewe…

Usiandike kwa sababu tu inabidi uandike..

Usiandike ili tu upate cha kupost…

Usiandike ili uonekane umeandika..

Usiandike ili uonekane na watu watakaotaka uwaandikie zaidi…

Usiandike ili upewe nafasi ya kuandika kwenye magazeti.

Usiandike ili kumfurahisha mtu fulani na akupe fursa fulani unayotaka..

Bali;

Andika kile ambacho unakiamini kweli..

Andika kile ambacho una msukumo mkubwa ndani yako kuandika…

Andika kile ambacho kina msaada kwa watu, kinawapa maarifa ya kufanya maamuzi bora..

Andika kile ambacho kinawafanya watu kuhoji na kudadisi zaidi.

Andika kile kinachowafanya watu kuona makosa ambayo wamekuwa wanafanya na umuhimu wa kubadilika.

SOMA;Naweza Kumsaidia Nani? Naweza Kumsaidia Nini? Njia Ya Kupata Mawazo Ya Kuandika.

Chagua sababu sahihi za kuandika, na uandishi wako utadumu. Lakini kama utaandika kwa sababu ambazo siyo sahihi, uandishi wako utapotea pale utakapopata kile unachotaka kupata kupitia uandishi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Usiandike Kwa Sababu Hizi, Utajipoteza Wewe Mwenyewe…

  1. Pingback: Usiangalie Washindani Wako, Angalia Hadhira Yako Pale Unapotoa Ujumbe. | MTAALAMU Network

Leave a Reply