Monthly Archives: August 2017

Usiandike Kitabu Kama Hakuna Anayekujua, Itakukatisha Tamaa.

Watu wengi wamekuwa wakiniandikia kuomba ushauri kuhusu uandishi wa vitabu. Wapo ambao tayari wanakuwa na vitabu wakati wengine ndiyo wanafikiria kuandika kitabu kwa mara ya kwanza.

Swali langu la kwanza kwa watu hawa huwa ni nani anayekufahamu? Kwa sababu kama hakuna anayekufahamu, kitabu unamwandikia nani?

Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi mno, kuna maarifa na taarifa za kila aina. Wapo waandishi wengi wanaotoa vitabu kila siku. Kipi kitamfanya mtu ajue kitabu chako na kukinunua?

abc

Unahitaji kuwa na watu wanaokujua tayari, ambao watakuwa wateja wa kwanza wa vitabu vyako. Na ninaposema kujua simaanishi kukujua wewe kwa jina na unapoishi, bali wanaokujua kupitia kazi zako za uandishi.

Mtu anapokujua wewe, kwa kujua kazi zako za uandishi, ambazo kwa kiasi fulani zinakuwa zimemsaidia, inakuwa rahisi kwake kununua kitabu chako. Hata unapotoa kitabu na kumwambia hapa nina kitabu kinaweza kukufaa, atachukua hatua mara moja.

Tofauti na mtu ambaye hajawahi kukusikia kabisa, anaweza kukutana na kitabu chako, lakini asiwe na msukumo wa kukinunua.

Swali muhimu ni je watu wanakujuaje?
Na hili ni swali muhimu na rahisi sana kujibu kwa zama hizi tunazoishi. Watu wanakujua kupitia intaneti na mitandao ya kijamii.

Kwa intaneti unahitaji kuwa na blog ambayo inaandika mambo yanayoendana na kile kitabu ulichoandika au unachopanga kuandika. Kupitia blog yako utatengeneza wasomaji ambao watakuwa wanakutegemea na kusikiliza kile unachosema. Hawa wanakuwa rahisi sana kununua kutoka kwako.

SOMA; Vitu Viwili Unavyohitaji Ili Uweze Kutengeneza Fedha Kupitia FACEBOOK.

Kupitia mitandao ya kijamii unahitaji kuwa na kurasa ambazo unazitumia kuwaelimisha watu kwa kile ambacho unaandika au umeandikia kitabu. Kupitia kurasa hizi watu wanakufuatilia na kujifunza, unapokuwa na kitabu na kuwaambia hichi hapa ni kitabu kinachoweza kukusaidia, watakuwa tayari kununua kutoka kwako.

Haya mawili ni muhimu sana kwako katika uandishi na uuzaji wa vitabu kwa zama tunazoishi sasa. Hata kama vitabu vyako unapeleka kwenye maduka ya vitabu, kukaa pale haimaanishi vitanunuliwa. Lakini unapowaambia wanaokufahamu kupitia kazi zako kwamba kitabu kipo duka fulani, wataenda pale na kununua.

Ni muhimu sana uwe na wasomaji kabla hata hujaandika kitabu, hili litakusaidia kuwafikia watu wengi kupitia kitabu ulichoandika au unachopanga kuandika.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Huhitaji Kuwa Sahihi Wakati Wote Na Kwa Kila Mtu.

Mitandao ya kijamii imetoa fursa sawa kwa wote kutoa maoni waliyonayo na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi. Kwa fursa hii, kila mtu anapenda kuona maoni yake ni ya muhimu zaidi kuliko ya wengine. Pia kuona maoni yake ndiyo sahihi zaidi.

Inapokuja kwenye maoni, huwezi kuwa sahihi wakati wote na kwa kila mtu. Hata kama kitu umejifunza na una uhakika nacho, wapo watu ambao watakupinga na kuja na maoni yao mbadala.

Hapa waandishi wengi huwa wanataharuki, na kuingia kwenye mabishano, ambayo huchochea ushindani zaidi na mara zote mabishano hayo huishia kwenye kudhalilishana na kutukanana.

Kuondokana na hali hiyo, jipe ruhusa ya kutokuwa sahihi wakati wote na kwa watu wote. Toa nafasi ya wengine kuona maoni yao ni muhimu na ya kweli zaidi, hata kama siyo uhalisia. Hii itakusaidia kujifunza hata kama watu wanakosea, unaona wapi hasa wanapokosea. Pia inakuokolea muda, badala ya kukazana kumwonesha mtu ukweli, ambaye wala hatakuelewa, unaweza kutumia muda huo kujifunza zaidi.

Ni vigumu sana kumbadili mtu ambaye anaamini maoni yake ndiyo sahihi na muhimu zaidi. Usijaribu hilo, utapoteza muda na nguvu.

Kama ambavyo nimewahi kukushirikisha kwenye makala za nyuma, kuna watu watakupinga tu hata kama hakuna kibaya unachofanya. Ni furaha yao kukushambulia wewe, sasa unapojibu mashambulizi, unawapa nafasi ya kuendelea. Ila unapoachana nao, kwa kutokushindana nao, wanakosa hamasa ya kuendelea na wewe na kwenda kutafuta mwingine ambaye ataingia kwenye ushindani.

SOMA; Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Hakuna sehemu yoyote ambayo utaadhibiwa kwa sababu umekubali maoni yako siyo sahihi au muhimu kuliko ya wengine. Hata hivyo ni maoni, na maoni yanatofautiana baina ya mtu na mtu. Hivyo usitake kuwa sahihi kwa kila mtu na kwa kila wakati, wakati mwingine wakubalie wengine wanaoona wana maoni sahihi na muhimu zaidi, ili upate nafasi ya kufanya mengine muhimu zaidi kwako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Wewe Ndiyo Bidhaa, Hivyo Hakikisha Na Wewe Una Bidhaa Pia.

Wakati kampuni ya Facebook inanunua mtandao wa wasap kwa dola bilioni 19 (zaidi ya trilioni 40 za Tanzania), watu wengi walistushwa sana. wakati huo inanunuliwa, wasap ilikuwa na jengo moja la ofisi na wafanyakazi wasiozidi 20.

Swali kwa wengi lilikuwa mtandao huo ulikuwa na kipi kikubwa cha kuufanya uuzwe ghali kiasi hicho? Na jibu lilikuwa wazi, ulikuwa na watumiaji wengi, zaidi ya watu milioni 200 kwa kipindi hicho.

Hii inatuonesha wazi kwamba, kama unatumia mitandao ya kijamii, basi wewe ni bidhaa. Mitandao ile inakuuza wewe kwa watu mbalimbali ili kuweza kupata faida na kuendelea kujiendesha. Huwezi kulikwepa hilo, kama upo kwenye mtandao, jua wewe ni bidhaa.

Unauzwa kwa wanaotangaza biashara zao, unauzwa kwa wanaofanya tafiti na yeyote mwenye uhitaji wa watu kwenye mtandao, anaweza kuuziwa uwepo wako kwenye mtandao.

Kwa kuwa hatuwezi kukwepa hili, hatua pekee ya kufanya ni kuhakikisha na sisi kuna vitu tunauza kupitia mitandao hii. Kama wewe ni bidhaa, basi hakikisha pia una bidhaa ambayo inakuingizia wewe faida kupitia mitandao hii.

Kuwa na kitu, iwe ni huduma au bidhaa, ambayo unauza kupitia mitandao ya kijamii. Unawauzia watu moja kwa moja kwenye mtandao, kwa kutumia mtandao kama duka lako au njia yako ya kutangaza biashara yako.

Kila unapotumia mitandao ya kijamii, hakikisha kipo kitu ambacho unauza hata kama ni kidogo kiasi gani. Hii itakufanya wewe unufaike na mitandao hii na kuacha kuwa tu mteja au mtumiaji wa mwisho, ambaye unauzwa kwa wengine.

Uzuri ni kwamba, chochote ulichonacho, au unachopenda kufanya, unaweza kuwauzia wengine kwenye mitandao ya kijamii. Ujuzi wowote ulionao, uzoefu uliojijengea, vyote hivyo kuna watu wanavihitaji ili kuweza kuboresha maisha yao zaidi.

SOMA; Hichi Ndiyo Kitu Kinachowavutia Watu Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Na Jinsi Ya Kukitumia Kutengeneza Kipato.

Angalia njia bora ya kuwasaidia kwenye hilo, iwe ni kupitia ushauri, vitabu na hata bidhaa nyingine zinazoweza kuwa za manufaa kwao.

Kama ungependa kujua njia bora kabisa kwako ya kutumia mitandao ya kijamii kwa faida, tuwasiliane kwa njia ya wasap namba 0717396253. Karibu sana.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Chini Kumejaa, Lakini Juu Zipo Nafasi Za Kutosha Sana.

Kwenye kila kitu ambacho watu wanafanya, kwenye ngazi ya chini kabisa wapo wengi ambao wanafanya kwa kawaida. Ukiwaangalia watu hao, unaweza kukata tamaa ya kufanya kitu, kwa kuamini hakuna tena nafasi ya wewe kuweza kufanya.

Hilo pia lipo kwenye uandishi. Ukiangalia jinsi ambavyo watu wengi wanaandika, unaweza kufikiri huna nafasi ya kuandika na wewe. Unaweza kuona kila kitu kimeshaandikwa.

Ukiangalia kwenye upande wa blog pia, zipo blog nyingi sana, unaweza kuona hakuna tena nafasi ya wewe kuwa na blog yako, au blog yako haitapata wasomaji.

Ukweli ni kwamba, wapo wengi wanaoandika, lakini wanaandika kawaida, wanaandika kwa ngazi ya chini mno, na hivyo kujikuta wakiwa katikati ya ushindani mkubwa.

Ni kweli blog zipo nyingi, lakini nyingi zinaandika vitu vya kawaida, zinanakili vitu vile vile ambavyo kila mtu anaandika.

Hii inatoa nafasi kubwa kwa wale ambao wanaweza kuandika kwa utofauti, na wala siyo kuandika vitu tofauti sana.

Wale ambao wanaweza kuandika kitu ambacho kinamsaidia mtu kuchukua hatua, ambacho mtu hawezi kukipata sehemu nyingine, wanayo nafasi kubwa ya kuweza kupata wasomaji wengi.

Wale ambao wanajali hasa, na kuweka utu kwenye kile wanachoandika, kujali wasomaji wao na changamoto au matatizo ambayo wanapitia, wana nafasi kubwa ya kupata wasomaji wengi na wanaojali pia.

SOMA; Makundi Matatu Ya Wasomaji Wa Kazi Zako Ambayo Unapaswa Kuyajua Ili Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Hivyo basi rafiki, tatizo siyo uwepo wa watu wengi wanaofanya kile ambacho unataka kufanya, tatizo ni je kuna kitu unajali sana kufanya au kuandika, ambacho kitawasaidia watu kupiga hatua fulani kwenye maisha yao?

Kama ndiyo, je upo tayari kukifanya kwa utofauti? Kuweka juhudi kubwa na kuongeza thamani kubwa?

Kama majibu yote ni ndiyo, basi fanya, usiangalie wangapi wanafanya, bali angalia ni mchango upi ambao wewe unatoa.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Taarifa Nyingi Haziwaelimishi Watu, Bali Zinawachanganya….

Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa zinazotuzunguka ni nyingi kuliko uwezo wetu wa kuzitumia. Kwa chochote unachotaka kujifunza, taarifa zinazopatikana ni nyingi kiasi kwamba ukisema uchukue muda wa kuzipitia zote, basi hutaanza hata kufanya.

Tunategemea kwa wingi huu wa taarifa basi watu wawe wameelimika na kuweza kuchukua hatua sahihi kwa maisha yao. Lakini huo siyo ukweli. Ukweli ni kwamba, kadiri taarifa zinavyokuwa nyingi, zinawachanganya watu.

Na watu wanapochanganywa na taarifa, wanaacha kabisa kuchukua hatua.

Hili limewahi kudhibitishwa kwa tafiti mbalimbali. Na ikaonekana wazi machaguo yanapokuwa mengi, watu wanaacha kabisa kuchukua hatua.

Swali ni je, kujua hili kunakusaidiaje wewe kama mwandishi na mtu unayeuza maarifa?

Ni muhimu sana kujua hili, ili lile eneo ambalo umechagua kuuza maarifa yake, uweze kulifanyia kazi vizuri.

SOMA;Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Kwa kujua hili, angalia ni matatizo au changamoto zipi ambazo unaweza kumsaidia mtu kuzitatua, kisha toa maarifa ya msingi kabisa na hatua za mtu kuchukua ili kuweza kuondoka kwenye matatizo au changamoto hizo.

Hakikisha kwenye maarifa unayotoa, unawapa watu hatua za kuchukua, ambazo zitawawezesha kutoka pale walipo sasa na kwenda mbele zaidi.

Usiishie tu kuwajaza watu taarifa ambazo watazifurahia lakini wabaki bila ya kuchukua hatua.

Ndiyo maana kwenye kila unachoandika, mwisho weka hatua za mtu kuchukua. Mpe mtu kitu cha kufanya, ambacho kitamwezesha kubadili hali yake na kupiga hatua.

Kwa njia hii utaacha kuwachanganya watu na utakuwa umewasaidia. Najua unajua kwamba kwenye mtandao wa intaneti, faida yako inakuja pale unapoweza kuwasaidia wengine.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Pamoja na kuishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa ndiyo mtaji mkuu na upatikanaji wake ni rahisi kuliko kipindi kingine chochote, bado sehemu kubwa ya watu hawana taarifa sahihi na za kweli.

Kwenye kila jambo ambalo watu wanafanya, kuna uongo mwingi sana ambao watu wamekuwa wanaaminishwa.

Kuanzia kwenye kazi, biashara, elimu, mahusiano, afya, fedha, uwekezaji, kilimo na mengine mengi.

Wapo watu ambao hawana taarifa sahihi, na wanasambaza sana zile ambazo wanazo, ambazo siyo sahihi.

Wapo watu ambao wana hofu na hivyo wanataka wengine nao wawe na hofu kama zao, hivyo wanasambaza hofu hizo.

Wapo watu ambao wanaujua ukweli, lakini wanauficha ukweli huo na kusambaza uongo ili waweze kunufaika.

Na wapo wengi ambao hawajui ukweli lakini hawajui kwamba hawajui, hivyo wanasambaza kitu ambacho wao wana uhakika ni kweli lakini kwa uhalisia siyo kweli.

Hivyo kama hujui uandike nini, au unajiuliza kipi unaweza kuandikia na ukasaidia watu, angalia kitu gani unajua, au unapenda kufuatilia, kisha wape watu ukweli wote ambao wamekuwa wananyimwa. Weka wazi kabisa kile ambacho mtu anapaswa kujua ili kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yake.

SOMA;Pamoja Na Kuandika Kile Unachopenda, Angalia Pia Idadi Ya Wanaokipenda Pia.

Fungua kila aina ya uongo na waoneshe watu wazi wazi ukweli uko wapi na kwa namna gani utawasaidia. Kwa njia hii utakuwa na mchango mkubwa kwa wengine na kuweza kuwasaidia.

Tahadhari; katika kufanya hivi, utaibua maadui wengi, kwa sababu utakapoanza kuwaambia watu ukweli, utawazuia watu kunufaika na uongo waliokuwa wanasambaza. Hivyo watakushambulia kwa namna moja au nyingine, jipange kwa hilo.

Pia utakutana na changamoto ya watu ambao wamedanganyika mpaka wanaona ukweli ndiyo uongo. Hawa huwa nasema wanaishi kwenye moshi wa uongo, kiasi kwamba hawawezi kuona mbele, uongo unakuwa umeshawaingia kiasi cha kuamini kwamba ni ukweli.

Tafuta mahali ambapo ukweli haujawafikia watu, na wape ukweli huo. Wape maarifa sahihi ya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi. Na muhimu zaidi, toa maarifa sahihi, usiweke nguvu zako kusema nani hayupo sahihi, wewe sema kipi sahihi watu wafanye.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Siri Kuu Ya Mawasiliano Ya Binadamu Ambayo Unaweza Kuitumia Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Nakumbuka nilipojiunga na masomo ya kidato cha kwanza, somo la kwanza kabisa kwenye Kiswahili lilikuwa somo la fasihi. Na tulifundishwa kwamba kuna aina kuu mbili za fasihi, fasihi simulizi na fasihi andishi. Na kwenye kila aina ya fasihi tulipewa mifano ya namna fasihi hizo zinatumika kufikisha ujumbe.

Ukiangalia fasihi hizi mbili, fasihi simulizi ni kongwe ukilinganisha na fasihi andishi. Hii ipo wazi kabisa, kwa sababu watu wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya masimulizi tangu enzi na enzi. Lakini maandiko yamekuja kuchukua nafasi kubwa miaka ambayo siyo mingi, hasa ukilinganisha na muda ambao binadamu tumekuwepo duniani.

Hivyo basi, tunaweza kusema ya kwamba, binadamu tupo vizuri kwenye masimulizi kuliko maandishi. Na hii ndiyo siri kubwa sana ambayo ukiweza kuifanyia kazi, uandishi wako utafanikiwa sana.

Siri hii ni kutumia masimulizi kwenye uandishi wako. Kama upo ujumbe wowote unaotaka kuwafikishia watu, basi tengeneza au tumia simulizi zilizotengenezwa, ambazo zinafikisha ujumbe husika.

Watu wanapenda masimulizi, watu wanapenda hadithi. Unakumbuka enzi za kukaa jioni na kusimuliana hadithi? Sasa hivi imebadilika tu, badala ya watu kukaa na kusimuliana hadithi, wanakaa kuangalia hadithi hizo kupitia tv au kusikiliza kwenye redio.

Watu wanakumbuka zaidi hadithi kuliko maandiko ambayo yanatoa maelezo pekee. Na pale hadithi inapokuwa ina mvuto kihisia, basi wasomaji huvutiwa zaidi kuisoma na kuifanyia kazi.

SOMA;Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani.

Tumia zaidi masimulizi, na popote unapoweza kupata hadithi inayoendana na ule ujumbe ambao unataka uwafikie watu, itumie. Itakusaidia sana kuwashikilia wasomaji wako na kuweza kujifunza na kuchukua hatua.

Binadamu ni viumbe wa hadithi na masimulizi, tumia hilo katika uandishi wako ili kuweza kuwafikia wengi zaidi.