Hivi Ndivyo Unavyopaswa Kukuza Huduma Yako Ya Uandishi…

Waandishi wengi wamekuwa hawapigi hatua kubwa kupitia uandishi wao, kwa sababu wamekuwa hawakui. Wanaandika vile vile miaka nenda miaka rudi. Ni kama wanakuwa wamepata maono fulani ya kuandika, wakachagua aina fulani ya uandishi na kuenda na hiyo mara zote. Wengi hawakuzi huduma zao na wasomaji wao wanakua na kuwaacha waandishi bado wakiwa pale walipoanzia.

Kwanza kabisa tambua uandishi ni huduma, na ni huduma nzuri na ya kipekee kwa sababu tangu kuwepo kwa dunia, uandishi ni njia ya pili ya mawasiliano yenye ushawishi mkubwa. Njia ya kwanza ni kuongea. Watu wamekuwa wakiandika tangu enzi na enzi. Na vipo vitabu na falsafa ambazo zimedumu kwa miaka mingi mpaka sasa tunazitumia na zinabadili maisha yetu.

Ili kuweza kukuza huduma yako kama mwandishi, lazima uwe tayari kukua wewe mwenyewe. Huwezi kukuza huduma yako kama wewe hukui. Huwezi kuandika vitu bora zaidi kama wewe huwi bora zaidi. Kwa kifupi huduma yako inaendana na wewe binafsi. Jinsi unavyopiga hatua, ndivyo unavyoweza kuikuza huduma yako zaidi.

Zamani wakati nawasoma wanafalsafa ninaowakubali, nilikuwa nafikiria kwamba yale wanayoandika wanayatoa kwenye mawazo yao wenyewe. Ni mpaka nilipoingia ndani zaidi kwenye maandishi yao, nikagundua kumbe na wao walikuwa wanajifunza kutoka kwa wanafalsafa wengine. Kila mwanafalsafa kuna namna alijifunza kwa wanafalsafa wengine na kisha kuboresha zaidi falsafa yake. Wengine walijifunza kwa kuangalia mazingira yao na watu wanaowazunguka, wakafikiri kwa kina na kujaribu kuja na majibu yatakayowasaidia.

SOMA;Kuwa Halisi, Simamia Kile Unachojua Na Kuamini Kupitia Uandishi Wako.

Hivyo kama mwandishi, lazima uwe na njia ya kukua zaidi, usiandike tu kwa mazoea, badala yake andika kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa. Na hilo linakutaka wewe ukue zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply