Kama Wewe Una Taaluma Au Uzoefu Wowote Ambao Watu Wanauhitaji, Unafanya Kosa Kubwa Sana Kama Huna Blog.

Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa ndiyo sarafu ya zama hizi. Watu wanathamini taarifa kuliko kitu kingine chochote. Kwa sababu taarifa sahihi zinawawezesha watu kufanya maamuzi sahihi na maamuzi sahihi yanawapelekea watu kupata mafanikio.

Katika zama hizi, mtu anapotaka kujua jambo lolote, kwanza anaingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake. Kupitia mtandao anakutana na wale wanaotoa taarifa kisha kutaka kujifunza zaidi kutoka kwao. Na pale unapobidi, wanakuwa tayari kugharamia ili kupata taarifa sahihi zinazowawezesha wao kufanya maamuzi sahihi.

Hivyo basi, kama wewe una taaluma au uzoefu wowote, ambao unaweza kuwasaidia watu kufanya maamuzi, iwapo huna njia ya kuweka taaluma na uzoefu wako kwenye mtandao wa intaneti, unafanya makosa makubwa. Hii ni kwa sababu unawakosa wale ambao wana shida na uhitaji wa taaluma au uzoefu ulionao wewe.

Chochote kile ambacho unajua, kinaweza kumsaidia mtu mwingine. Unaweza kuona unachojua ni cha kawaida sana, lakini nataka kukuambia kuna mtu amekwama mahali kwa sababu hajui unachojua wewe. Anaingia kwenye mtandao na kutafuta hatua zipi achukue, na huenda hajakutana na ushauri unaoweza kumsaidia.

Unahitaji kuwa na njia ya kuwafikia watu kwenye mtandao wa intaneti. Pale mtu anapoingia kwenye mtandao wa google na kutafuta kitu kinachoendana na unachojua wewe, basi waletwe kwako moja kwa moja.

SOMA;Njia Tano Za Kuanza Kukuza Email List Yako Kupitia Blog Na Mitandao Ya Kijamii.

Zipo njia nyingi za kufanya hivyo, rahisi kabisa na inayopendwa na wengi ni MITANDAO YA KIJAMII. Hii wengi huitumia kwa kuweka taarifa fupi fupi na hata matangazo ya kile ambacho wanafanya.

Njia nzuri kabisa ambayo nimekuwa nawashauri watu waitumie ni kuwa na blog. Hii inakuwa kama nyumba yako kwenye mtandao wa intaneti. Ni kona ambayo unakuwa umejitengenezea, ambapo mtu akitaka kitu fulani kutoka kwako, basi anajua akija pale atakipata.

Unapokuwa na blog kwa sehemu kubwa unakuwa unaimiliki mwenyewe na hivyo kuweza kuitumia kutunza kazi zako, kujenga wafuasi wako na kuuza huduma au bidhaa ambazo unazo.

Blog ni njia bora kabisa ya watu kukufikia, hasa pale wanapotafuta kitu kinachoendana na kazi zako kupitia mitandao kama google.

Ndiyo maana napenda kukushauri, kama utaalamu wako au uzoefu wako ni wa kufanya kazi na watu moja kwa moja, basi anzisha blog yako.

Na wala huhitaji kuwa na gharama kubwa ili kuanzisha blog, huhitaji hata kuwa na utaalamu mkubwa. Unachohitaji ni kuwa tayari kuwapa watu maarifa na taarifa sahihi, ili waweze kufanya maamuzi sahihi.

Kama mimi ninavyokupa taarifa sahihi hapa kuhusu kuwafikia watu kupitia mtandao wa intaneti kwa kuwa na blog. Na kama mpaka sasa huna blog, naweza kukusaidia ukawa na blog bora kabisa ya kuanzia kufikisha taarifa zako kwa watu ambao wana uhitaji nazo. Tuwasiliane kwa wasap 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Kama Wewe Una Taaluma Au Uzoefu Wowote Ambao Watu Wanauhitaji, Unafanya Kosa Kubwa Sana Kama Huna Blog.

  1. Pingback: Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao. | MTAALAMU Network

Leave a Reply