Hicho Unachofikiri Ni Kidogo Na Cha Kawaida, Wapo Wengine Kitawasaidia Mno, Usiache Kuwashirikisha.

Rafiki, nimegundua naweza kuandika makala za kuwasaidia waandishi na waendeshaji wa blogu kupitia maswali mbalimbali wanayoyauliza. Hivyo nakusihi sana, kama makala hizi ninazoandika kupitia blog hii ya MTAALAMU zinakusaidia, basi weka maoni hapo chini yenye swali unalotaka kupata ufafanuzi na nitaandaa makala yake. Pia unaweza kunitumia swali kwa njia ya wasap 0717396253 na nitaandaa makala ya kufafanua kwa kina.

Mmoja wa wasomaji na mtu niliyemshauri kuanza kutoa maarifa ya taaluma yake kupita blog, aliniambia kuna kitu cha kawaida sana alikuwa ameandika, lakini akashangaa namna gani watu wanakichukulia kwa umuhimu mkubwa. Na hata watu walipomuuliza maswali, alishangaa inakuwaje watu hawajui vitu vya kawaida kama hivyo?

Hapo ndipo nilimwambia watu wengi wamekuwa wanafanya makosa. Watu, hasa wale ambao wana taaluma fulani, huwa wanafikiria mambo makubwa sana yanayohusu taaluma zao. Lakini yapo mambo madogo na ya kawaida kabisa, ambayo wao wanayadharau, lakini watu wengine wanayaheshimu sana.

Kuna vitu wewe unaona ni vya kawaida kwa sababu umezoea kufanya kila siku, lakini yupo mtu amekwama mahali hajui achukue hatua gani. Ambapo kama wewe ungechukua muda na kumshirikisha kile unachojua wewe, kingemsaidia na angekushukuru na kukufuatilia zaidi.

SOMA;Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani.

Ndiyo maana nimekuwa nasisitiza kila mtu anapaswa kuwa na blog, kila mtu. Kwa sababu kila mtu ana safari yake ya maisha inayotofautiana na wengine. Kila mtu kuna kitu anakifanya ambacho mwingine hajui kwa uhakika. Iwapo utakuwa na blog na ukawasaidia watu kupitia kile unachojua, kwa kuwasaidia kupata maarifa sahihi yatakayowawezesha kufanya maamuzi sahihi, watakuamini na kuwa wafuasi wako zaidi.

Chochote kile ambacho unakijua, iwe ni kwa kusomea au kwa mazoea, kinaweza kumsaidia mtu mwingine. Chochote ambacho umewahi kufanya kwenye maisha yako, wapo wengine wanaoweza kujifunza kwako.

Kwa mfano kama umeweza kusoma na kufaulu vizuri masomo yako, licha ya kuishi mazingira magumu, wapo wengine wanaopitia hali kama hizo. Ukiweza kuwashirikisha umewezaje kufanya hivyo, watanufaika sana.

Usidharau elimu au uzoefu ambao unao kwa kuona ni mdogo na hauwezi kumsaidia mtu yeyote, una msaada mkubwa kwa wengi, uweke kwenye njia ambayo mtu anaweza kujifunza na kuchukua hatua, utakuwa umewasaidia wengi na hata kutengeneza mazingira ya kuwa na kipato baadaye.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply