Andika Hichi Pale Ambapo Huna Kabisa Kitu Cha Kuandika.

Msisitizo wangu ni mmoja, kama umeamua kuwa mwandishi, basi andika kila siku. Najua unajua ninaposema mwandishi namaanisha mtu anayetumia maandishi kuwapa wengine maarifa na taarifa za kuwawezesha kufanya maamuzi bora kwenye maisha yake.

Hakuna maana ya kujiita mwandishi kama huandiki. Tunaita mti ni mwembe kwa sababu unatoa maembe, kadhalika kwenye mchungwa ambao unatoa machungwa. Mwembe na mchungwa vitaendelea kutoa matunda yake kadiri msimu unavyokwenda.

Hivyo wewe mwandishi andika, andika kila siku, hata kama huchapishi kile unachoandika kila siku.

Sasa kuandika kila siku siyo zoezi rahisi hata kidogo. Zipo siku utakuwa hujisikii vizuri, zipo siku utafikiria na ukose kabisa kitu cha kuandika. Lakini bado unahitaji upate kitu cha kuandika, na lazima uandike kila siku.

Unapofika kwenye siku kama hizi, basi unaweza kuandika kwa njia hii; andika sentensi moja ya kweli kabisa kuhusiana na kile unachoandikia, kisha endelea kutetea sentensi hiyo, endelea kuielezea kwa kina sentensi hiyo, endelea kwenda nayo kadiri mawazo zaidi yanavyokujia kuhusiana na kile ambacho unakiandika.

SOMA;Kazi Ambayo Haijakamilika Haivutii, Hivyo Jipe Ruhusa Ya Kuandika Kitu Kibovu.

Kwa namna hii utajikuta umeandika kitu kikubwa cha kuweza kuwashirikisha watu, wakajifunza na kuchukua hatua.

Unapoanza zoezi hili usijihukumu au kuanza kuangalia kama unachoandika ni kizuri au kibaya. Wewe fuata mawazo yako kadiri yanavyokupeleka, kwa namna unavyotaka kumwonesha mtu ule ukweli ambao anapaswa kuujua.

Usikubali kupitisha siku hujaandika kwa sababu unaona huna cha kuandika, yapo mambo mengi ya kuandika, ni vile tu wewe kwa sasa huangalii mambo hayo na hivyo huyaoni. Unaangalia kwamba huna cha kuandika na hivyo unachoona ni huna cha kuandika.

Unapovunja ukuta huo uliojijengea kwenye akili, na kuanza kufikiria ile sentensi moja ya kweli kabisa na unayotaka watu waielewe, akili yako inaanza kukukusanyia ushahidi wa kutosha kutetea sentensi uliyoanza nayo. Utajikuta unapata mifano ya kuelezea, utajikuta unafikiria njia bora zaidi za kumwelezea yeyote.

Yote hayo ni kwa sababu umechagua sehemu ya kuanzia na kufikiria kwenda mbele zaidi kutokea hapo ulipoanzia.

Anza na sentensi moja ya kweli kabisa, kisha itetee na kuitolea ufafanuzi zaidi, utakuwa na mengi ya kuandika na kufundisha.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Andika Hichi Pale Ambapo Huna Kabisa Kitu Cha Kuandika.

  1. Pingback: Siri Moja Ya Kubobea Kwenye Jambo Lolote Unaloandikia. | MTAALAMU Network

Leave a Reply