Unachoandika kitasomwa miaka mingapi kutoka sasa?

Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba ili usisahaulike hapa duniani, basi unahitaji kufanya moja kati ya vitu hivi viwili;

Moja; ishi maisha ambayo ni makubwa sana kiasi cha watu kuandika kuhusu maisha yako. Unalielewa hili kupitia vitabu mbalimbali ulivyowahi kusoma kuhusu watu waliowahi kufanya makubwa hapa duniani.

Mbili; andika kitabu ambacho watu watakiishi, hichi kinakuwa kitabu ambacho kina maarifa muhimu sana na ya kuwasaidia watu kiasi cha wao kukifanya mwongozo wa maisha yao. Hapa pia utakuwa unavijua vitabu ambavyo watu wamekuwa wakiviishi, hasa vya falsafa na imani mbalimbali.

Swali langu kwako ni je kile unachoandika leo kitasomwa miaka mingapi kutoka leo? Je wapo watu ambao wataishi kile unachoandika? Watakitumia kama rejea pale wanapokutana na changamoto mbalimbali? Je watu watawaambia wengine wasome kile ambacho umeandika?

SOMA;Kazi Ambayo Haijakamilika Haivutii, Hivyo Jipe Ruhusa Ya Kuandika Kitu Kibovu.

Hili ni swali ambalo sisi waandishi lazima tujiulize kila mara kabla hatujafanya kazi yetu. Kwa kujiuliza hivi, tutakazana kuandika kitu ambacho kitawasaidia wengi.

Siyo mara zote utaweza kaundika kitu kinachodumu miaka mingi, lakini unapojiuliza kila mara, kuna wakati utaweza kuandika kitu kitakachodumu.

Hili ni muhimu sana inapokuja kwenye vitabu, kwa sababu unaweka nguvu nyingi kwenye kuandika kitabu, basi jitahidi kiwe kitabu ambacho hakipitwi na wakati. Kiwe kitabu ambacho kwenye zama zozote zile, kinaendelea kuishi na kuwapa watu mwongozo sahihi.

Leo hii vipo vitabu vingi tunavisoma, ambavyo vimeandikwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita. Watu walioviandika na walioishi zama hizo, wakirudi duniani leo hawawezi kutambua kinachoendelea kabisa, lakini mawazo yao yameendelea kutusaidia mpaka leo hii.

Tuna fursa kila mmoja wetu ya kuweka kazi kubwa na kuweza kutoa maarifa ambayo yatadumu na kusaidia vizazi vingi vinavyokuja baadaye. Ni wajibu wengi kuandika tukifikiri hili, ili tuweze kuwasaidia wengi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply