Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao.

Sasa hivi karibu kila maarifa yanapatikana bure kabisa kwenye mtandao wa intaneti. Na hivyo watu wengi wamekuwa wakinufaika na maarifa hayo yanayopatikana bure, kuanzia vitabu, makala, video, sauti na kadhalika.

Ukiingia kwenye mtandao wa google na kutafuta kitu chochote, chini ya sekunde moja, utaletewa maelfu ya matokeo yanayoendana na kile unachotafuta.

Kwa kifupi yapo maarifa na taarifa nyingi kiasi kwamba ukitaka uzisome zote, basi itabidi uishi maisha yako yote yaliyobakia kuzisoma tu, na hapo hulipi hata senti moja.

Sasa hapa ndipo waandishi wengi, hasa wachanga hujiuliza wanawezaje kuuza maarifa wakati yanapatikana kwa wingi na bure kabisa kwenye mtandao?

Na hata unapojaribu kuuza, kuna baadhi ya wasomaji wako wanaweza kukuambia mbona unachouza tunakipata bure tu?

Hapo wengi hukata tamaa na kuona hawawezi kutengeneza kipato kwenye mtandao kwa kuuza maarifa. Lakini ukweli ni kwamba, hilo linawezekana, na wengi wanafanya hivyo.

Nimekuwa nawashauri watu wanaoniomba ushauri kuhusu kuandika vitabu, na swali langu kwao huwa ni moja, unataka kuandika kitabu, je una blog? Wengi jibu huwa ni hapana. Na huwa nawaambia kitu kimoja, anza na blog kwanza, kabla hujakimbilia kwenye kitabu.

Uandishi wa zama hizi, au biashara yoyote ya kuuza maarifa, kitu cha kwanza kinachomsukuma mtu kununua kwako, ni kama anakujua kwa muda mrefu. Kama ameshafuatilia kazi zako kwa muda mrefu na hivyo kuwa mfuasi na shabiki wako. Mtu huyu ndiye atakayekuwa wa kwanza kununua kwako, bila ya kujiuliza kama maarifa hayo yanapatikana bure mtandaoni au la.

SOMA;Kama Wewe Una Taaluma Au Uzoefu Wowote Ambao Watu Wanauhitaji, Unafanya Kosa Kubwa Sana Kama Huna Blog.

Hivyo basi, ili kuuza maarifa yanayopatikana bure mtandaoni, unahitaji kuwa na watu wanaokukubali na kukufuatilia kwa muda mrefu. Watu ambao umekuwa unawaandikia na kuwashirikisha maarifa yako kwa muda mrefu, wakanufaika nayo sana.

Watu hawa ndiyo watakaohamasika sana pale utakapowaambia, nimekuwa nakuandikia makala hizi kwa muda mrefu, umenishirikisha changamoto zako kwa muda mrefu, hapa kuna kitabu ambacho kitakusaidia sana… watanunua hata kama hujawaambia jina la kitabu. Kwa sababu wanakuamini, kwa sababu wana sababu ya kukusikiliza.

Usikimbilie kuuza kwa sababu unataka kuuza, ila tengeneza kwanza sababu ya watu kununua kwako. Sababu hii unaitengeneza kwa kuwapa watu maarifa ambayo yanawasaidia, kiasi kwamba siku ukija na maarifa unayouza, watakuwa tayari kulipia kwa sababu tayari wameshazoea kupata vitu vizuri.

Wape watu sababu ya kununua kwako, na watakuwa tayari kununua muda wowote na chochote unachouza hata kama wanaweza kukipata bure sehemu nyingine.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

3 thoughts on “Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao.

  1. Pingback: Hata Kama Kila Kitu Kimeshaandikwa, Dunia Bado Haijasikia Sauti Yako. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Watu Huwa Hawathamini Sana Vitu Vya Bure, Jifunze Kuweka Thamani Zaidi Na Kutoza Gharama. | MTAALAMU Network

  3. Pingback: Wanunuaji Wa Mtandaoni Wapo Sehemu Hii Muhimu. | MTAALAMU Network

Leave a Reply