Siri Kuu Ya Mawasiliano Ya Binadamu Ambayo Unaweza Kuitumia Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Nakumbuka nilipojiunga na masomo ya kidato cha kwanza, somo la kwanza kabisa kwenye Kiswahili lilikuwa somo la fasihi. Na tulifundishwa kwamba kuna aina kuu mbili za fasihi, fasihi simulizi na fasihi andishi. Na kwenye kila aina ya fasihi tulipewa mifano ya namna fasihi hizo zinatumika kufikisha ujumbe.

Ukiangalia fasihi hizi mbili, fasihi simulizi ni kongwe ukilinganisha na fasihi andishi. Hii ipo wazi kabisa, kwa sababu watu wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya masimulizi tangu enzi na enzi. Lakini maandiko yamekuja kuchukua nafasi kubwa miaka ambayo siyo mingi, hasa ukilinganisha na muda ambao binadamu tumekuwepo duniani.

Hivyo basi, tunaweza kusema ya kwamba, binadamu tupo vizuri kwenye masimulizi kuliko maandishi. Na hii ndiyo siri kubwa sana ambayo ukiweza kuifanyia kazi, uandishi wako utafanikiwa sana.

Siri hii ni kutumia masimulizi kwenye uandishi wako. Kama upo ujumbe wowote unaotaka kuwafikishia watu, basi tengeneza au tumia simulizi zilizotengenezwa, ambazo zinafikisha ujumbe husika.

Watu wanapenda masimulizi, watu wanapenda hadithi. Unakumbuka enzi za kukaa jioni na kusimuliana hadithi? Sasa hivi imebadilika tu, badala ya watu kukaa na kusimuliana hadithi, wanakaa kuangalia hadithi hizo kupitia tv au kusikiliza kwenye redio.

Watu wanakumbuka zaidi hadithi kuliko maandiko ambayo yanatoa maelezo pekee. Na pale hadithi inapokuwa ina mvuto kihisia, basi wasomaji huvutiwa zaidi kuisoma na kuifanyia kazi.

SOMA;Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani.

Tumia zaidi masimulizi, na popote unapoweza kupata hadithi inayoendana na ule ujumbe ambao unataka uwafikie watu, itumie. Itakusaidia sana kuwashikilia wasomaji wako na kuweza kujifunza na kuchukua hatua.

Binadamu ni viumbe wa hadithi na masimulizi, tumia hilo katika uandishi wako ili kuweza kuwafikia wengi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply