Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Pamoja na kuishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa ndiyo mtaji mkuu na upatikanaji wake ni rahisi kuliko kipindi kingine chochote, bado sehemu kubwa ya watu hawana taarifa sahihi na za kweli.

Kwenye kila jambo ambalo watu wanafanya, kuna uongo mwingi sana ambao watu wamekuwa wanaaminishwa.

Kuanzia kwenye kazi, biashara, elimu, mahusiano, afya, fedha, uwekezaji, kilimo na mengine mengi.

Wapo watu ambao hawana taarifa sahihi, na wanasambaza sana zile ambazo wanazo, ambazo siyo sahihi.

Wapo watu ambao wana hofu na hivyo wanataka wengine nao wawe na hofu kama zao, hivyo wanasambaza hofu hizo.

Wapo watu ambao wanaujua ukweli, lakini wanauficha ukweli huo na kusambaza uongo ili waweze kunufaika.

Na wapo wengi ambao hawajui ukweli lakini hawajui kwamba hawajui, hivyo wanasambaza kitu ambacho wao wana uhakika ni kweli lakini kwa uhalisia siyo kweli.

Hivyo kama hujui uandike nini, au unajiuliza kipi unaweza kuandikia na ukasaidia watu, angalia kitu gani unajua, au unapenda kufuatilia, kisha wape watu ukweli wote ambao wamekuwa wananyimwa. Weka wazi kabisa kile ambacho mtu anapaswa kujua ili kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yake.

SOMA;Pamoja Na Kuandika Kile Unachopenda, Angalia Pia Idadi Ya Wanaokipenda Pia.

Fungua kila aina ya uongo na waoneshe watu wazi wazi ukweli uko wapi na kwa namna gani utawasaidia. Kwa njia hii utakuwa na mchango mkubwa kwa wengine na kuweza kuwasaidia.

Tahadhari; katika kufanya hivi, utaibua maadui wengi, kwa sababu utakapoanza kuwaambia watu ukweli, utawazuia watu kunufaika na uongo waliokuwa wanasambaza. Hivyo watakushambulia kwa namna moja au nyingine, jipange kwa hilo.

Pia utakutana na changamoto ya watu ambao wamedanganyika mpaka wanaona ukweli ndiyo uongo. Hawa huwa nasema wanaishi kwenye moshi wa uongo, kiasi kwamba hawawezi kuona mbele, uongo unakuwa umeshawaingia kiasi cha kuamini kwamba ni ukweli.

Tafuta mahali ambapo ukweli haujawafikia watu, na wape ukweli huo. Wape maarifa sahihi ya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi. Na muhimu zaidi, toa maarifa sahihi, usiweke nguvu zako kusema nani hayupo sahihi, wewe sema kipi sahihi watu wafanye.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

  1. Pingback: Taarifa Nyingi Haziwaelimishi Watu, Bali Zinawachanganya…. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Huhitaji Kuwa Sahihi Wakati Wote Na Kwa Kila Mtu. | MTAALAMU Network

Leave a Reply