Taarifa Nyingi Haziwaelimishi Watu, Bali Zinawachanganya….

Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa zinazotuzunguka ni nyingi kuliko uwezo wetu wa kuzitumia. Kwa chochote unachotaka kujifunza, taarifa zinazopatikana ni nyingi kiasi kwamba ukisema uchukue muda wa kuzipitia zote, basi hutaanza hata kufanya.

Tunategemea kwa wingi huu wa taarifa basi watu wawe wameelimika na kuweza kuchukua hatua sahihi kwa maisha yao. Lakini huo siyo ukweli. Ukweli ni kwamba, kadiri taarifa zinavyokuwa nyingi, zinawachanganya watu.

Na watu wanapochanganywa na taarifa, wanaacha kabisa kuchukua hatua.

Hili limewahi kudhibitishwa kwa tafiti mbalimbali. Na ikaonekana wazi machaguo yanapokuwa mengi, watu wanaacha kabisa kuchukua hatua.

Swali ni je, kujua hili kunakusaidiaje wewe kama mwandishi na mtu unayeuza maarifa?

Ni muhimu sana kujua hili, ili lile eneo ambalo umechagua kuuza maarifa yake, uweze kulifanyia kazi vizuri.

SOMA;Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Kwa kujua hili, angalia ni matatizo au changamoto zipi ambazo unaweza kumsaidia mtu kuzitatua, kisha toa maarifa ya msingi kabisa na hatua za mtu kuchukua ili kuweza kuondoka kwenye matatizo au changamoto hizo.

Hakikisha kwenye maarifa unayotoa, unawapa watu hatua za kuchukua, ambazo zitawawezesha kutoka pale walipo sasa na kwenda mbele zaidi.

Usiishie tu kuwajaza watu taarifa ambazo watazifurahia lakini wabaki bila ya kuchukua hatua.

Ndiyo maana kwenye kila unachoandika, mwisho weka hatua za mtu kuchukua. Mpe mtu kitu cha kufanya, ambacho kitamwezesha kubadili hali yake na kupiga hatua.

Kwa njia hii utaacha kuwachanganya watu na utakuwa umewasaidia. Najua unajua kwamba kwenye mtandao wa intaneti, faida yako inakuja pale unapoweza kuwasaidia wengine.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply