Chini Kumejaa, Lakini Juu Zipo Nafasi Za Kutosha Sana.

Kwenye kila kitu ambacho watu wanafanya, kwenye ngazi ya chini kabisa wapo wengi ambao wanafanya kwa kawaida. Ukiwaangalia watu hao, unaweza kukata tamaa ya kufanya kitu, kwa kuamini hakuna tena nafasi ya wewe kuweza kufanya.

Hilo pia lipo kwenye uandishi. Ukiangalia jinsi ambavyo watu wengi wanaandika, unaweza kufikiri huna nafasi ya kuandika na wewe. Unaweza kuona kila kitu kimeshaandikwa.

Ukiangalia kwenye upande wa blog pia, zipo blog nyingi sana, unaweza kuona hakuna tena nafasi ya wewe kuwa na blog yako, au blog yako haitapata wasomaji.

Ukweli ni kwamba, wapo wengi wanaoandika, lakini wanaandika kawaida, wanaandika kwa ngazi ya chini mno, na hivyo kujikuta wakiwa katikati ya ushindani mkubwa.

Ni kweli blog zipo nyingi, lakini nyingi zinaandika vitu vya kawaida, zinanakili vitu vile vile ambavyo kila mtu anaandika.

Hii inatoa nafasi kubwa kwa wale ambao wanaweza kuandika kwa utofauti, na wala siyo kuandika vitu tofauti sana.

Wale ambao wanaweza kuandika kitu ambacho kinamsaidia mtu kuchukua hatua, ambacho mtu hawezi kukipata sehemu nyingine, wanayo nafasi kubwa ya kuweza kupata wasomaji wengi.

Wale ambao wanajali hasa, na kuweka utu kwenye kile wanachoandika, kujali wasomaji wao na changamoto au matatizo ambayo wanapitia, wana nafasi kubwa ya kupata wasomaji wengi na wanaojali pia.

SOMA; Makundi Matatu Ya Wasomaji Wa Kazi Zako Ambayo Unapaswa Kuyajua Ili Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Hivyo basi rafiki, tatizo siyo uwepo wa watu wengi wanaofanya kile ambacho unataka kufanya, tatizo ni je kuna kitu unajali sana kufanya au kuandika, ambacho kitawasaidia watu kupiga hatua fulani kwenye maisha yao?

Kama ndiyo, je upo tayari kukifanya kwa utofauti? Kuweka juhudi kubwa na kuongeza thamani kubwa?

Kama majibu yote ni ndiyo, basi fanya, usiangalie wangapi wanafanya, bali angalia ni mchango upi ambao wewe unatoa.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply