Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Huhitaji Kuwa Sahihi Wakati Wote Na Kwa Kila Mtu.

Mitandao ya kijamii imetoa fursa sawa kwa wote kutoa maoni waliyonayo na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi. Kwa fursa hii, kila mtu anapenda kuona maoni yake ni ya muhimu zaidi kuliko ya wengine. Pia kuona maoni yake ndiyo sahihi zaidi.

Inapokuja kwenye maoni, huwezi kuwa sahihi wakati wote na kwa kila mtu. Hata kama kitu umejifunza na una uhakika nacho, wapo watu ambao watakupinga na kuja na maoni yao mbadala.

Hapa waandishi wengi huwa wanataharuki, na kuingia kwenye mabishano, ambayo huchochea ushindani zaidi na mara zote mabishano hayo huishia kwenye kudhalilishana na kutukanana.

Kuondokana na hali hiyo, jipe ruhusa ya kutokuwa sahihi wakati wote na kwa watu wote. Toa nafasi ya wengine kuona maoni yao ni muhimu na ya kweli zaidi, hata kama siyo uhalisia. Hii itakusaidia kujifunza hata kama watu wanakosea, unaona wapi hasa wanapokosea. Pia inakuokolea muda, badala ya kukazana kumwonesha mtu ukweli, ambaye wala hatakuelewa, unaweza kutumia muda huo kujifunza zaidi.

Ni vigumu sana kumbadili mtu ambaye anaamini maoni yake ndiyo sahihi na muhimu zaidi. Usijaribu hilo, utapoteza muda na nguvu.

Kama ambavyo nimewahi kukushirikisha kwenye makala za nyuma, kuna watu watakupinga tu hata kama hakuna kibaya unachofanya. Ni furaha yao kukushambulia wewe, sasa unapojibu mashambulizi, unawapa nafasi ya kuendelea. Ila unapoachana nao, kwa kutokushindana nao, wanakosa hamasa ya kuendelea na wewe na kwenda kutafuta mwingine ambaye ataingia kwenye ushindani.

SOMA; Ni Ukweli Upi Ambao Bado Haujasemwa Au Watu Wanauficha? Andikia Hilo Na Utaweza Kuwasaidia Wengi.

Hakuna sehemu yoyote ambayo utaadhibiwa kwa sababu umekubali maoni yako siyo sahihi au muhimu kuliko ya wengine. Hata hivyo ni maoni, na maoni yanatofautiana baina ya mtu na mtu. Hivyo usitake kuwa sahihi kwa kila mtu na kwa kila wakati, wakati mwingine wakubalie wengine wanaoona wana maoni sahihi na muhimu zaidi, ili upate nafasi ya kufanya mengine muhimu zaidi kwako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply