Soma Maandiko Ya Miaka Mia Tano Iliyopita, Na Utajifunza Kitu Hiki Kikubwa Sana.

Vitu vingi vinavyoandikwa sasa, vilishaandikwa miaka mingi sana ambayo imepita.

Changamoto za watu ni zile zile, fedha, mahusiano, afya, muda, kazi, biashara, mapenzi na imani.

Kinachobadilika ni zama ambapo changamoto hizi zinatokea, na njia zinazopatikana za kutatua changamoto hizi.

Hii inatupa siri moja muhimu, ili kufanikiwa kama mwandishi, lazima uwasome waandishi wengine, tena wa siku za nyuma sana.

Kwa lile eneo unaloandikia, nenda miaka elfu moja nyuma, au hata miaka mia tano nyuma, ukishindwa, basi nenda miaka mia moja nyuma.

Soma kazi ambazo zimeandikwa katika kipindi hicho. Angalia changamoto ambazo watu walikuwa nazo wakati huo. Angalia njia zilizokuwepo za kutatua changamoto hizo kwenye zama hizo.

Ancient Writing

Hili litakupa wigo mpana wa kufikiri kwa kina, litakuwezesha kuja na majibu na suluhisho ambalo wengi kwa sasa hawalifikirii.

Tatizo kubwa sana kwenye kila eneo la maisha yetu ni kwamba zipo njia fulani ambazo zinaonekana ndiyo sahihi na watu ndiyo wamezoea, na wanazifuata hizo hizo, kwa sababu ndicho wamezoea kuona.

Kwa wewe kwenda miaka mia moja nyuma, na kuangalia mambo yalivyofanywa, itakuwezesha kufikiri tofauti na hapo utakuja na majibu ambayo wengi hawajayazoea. Yatakuwa majibu bora ambayo yatawasaidia wengi.

SOMA; Kuwa Halisi, Simamia Kile Unachojua Na Kuamini Kupitia Uandishi Wako.

Unaposoma kazi za miaka mingi iliyopita, angalia ni kwa namna gani zinaweza kuwasaidia watu katika zama za sasa. Kwa mfano, miaka mia moja iliyopita, hakukuwa na mtandao wa intaneti, hivyo watu waliandika kwa njia za kawaida, vitabu na magazeti au majarida. Lakini sasa hivi mtandao wa intaneti unatoa fursa ya mtu kaundika bila ya kuchapa vitabu au magazeti na majarida. Hapa unaweza kuchanganya njia ya zamani na njia mpya na kuweza kufanya kazi bora kabisa.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maeneo mengi, kuna njia ambazo zilizoeleka kwa zama hizo, ambazo kwa sasa wengi hawazipi uzito. Angalia namna gani unaweza kuchanganya njia hizo na zilizopo sasa ili kuboresha zaidi kile ambacho watu wanafanya.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Soma Maandiko Ya Miaka Mia Tano Iliyopita, Na Utajifunza Kitu Hiki Kikubwa Sana.

  1. Pingback: Kama Huandiki Hukitendei Haki Kizazi Kinachokuja. | MTAALAMU Network

Leave a Reply