Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya kosa kubwa sana wanapotangaza biashara zao kwenye mitandao ya kijamii. Wanachofanya ni kuwasukumia watu picha za bidhaa zao. Wanakazana kutuma picha nyingi kupitia mitandao ya kijamii na wakati mwingine hata kuwatumia watu moja kwa moja kwenye mitandao kama wasap.

Njia hii inaweza kuonekana kuleta matokeo kiasi mwanzoni, lakini baadaye inakuwa usumbufu na haileti matokeo. Kwa sababu ni usumbufu na wengi wanaokuwa wanatumiwa picha zile hawajali kabisa kuhusu hizo picha wanazotumiwa.

Kama wewe ni mfanyabiashara, ambaye unatumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako, basi acha mara moja kuwasukumia watu picha kila wakati. Watu watajifunza kupuuza picha zako na haijalishi utatuma nyingi kiasi gani, haitakuongezea mauzo.

kutangaza mitandaoni

Njia bora kabisa ya kutangaza bidhaa zako kwenye mitandao ya kijamii ni kuwafikia wale ambao wanajali. Badala ya kumsukumia kila mtu picha nyingi, unachagua wale wanaojali, ambao wao wenyewe watakutafuta wakitaka bidhaa zako ambazo zitawasaidia.

Kwa njia hii, kwanza unahitaji kuwajua wateja wa biashara yako ni watu wa aina gani. Ukishawajua, jua changamoto zao kwenye kile unachouza ni nini? Vitu hivi viwili vitakuwezesha wewe kuwatengenezea sababu ya kukutafuta na kununua kwako.

Baada ya kujua vitu hivyo viwili, unahitaji kutengeneza maudhui ambayo yanawasaidia wateja wako kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye eneo la maisha yao linalohusisha biashara yako. Hapa unawaandalia taarifa na maarifa muhimu kwao, ambayo yatawawezesha kufanya maamuzi sahihi kwao.

SOMA; Chagua Tatizo Unaloweza Kuwasaidia Watu Kutatua Kupitia Maarifa Sahihi.

Kwa njia hii, utatengeneza watu wanaokuamini wewe kama mshauri na mwalimu wao, na hivyo utakapowaambia kuna bidhaa unauza, hawatasita kununua. Hii inawafanya wao wakuulize kama kuna bidhaa unayouza, kabla hata hujawaambia kama unauza. Huwezi kuwachosha watu kwenye hili, kwa sababu wao ndiyo wanakutafuta wewe kupata maarifa na taarifa badala ya wewe kuwasukumia matangazo.

Swali ni je unawezaje kufanya hivyo?

Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwaelimisha watu kuhusiana na biashara unayofanya. Pia unaweza kuwa na blogu ambayo itakuwa inatoa elimu inayohusiana na biashara yako. Hapo utaweza kuwapa watu maarifa na taarifa na pia kuwaeleza juu ya kile unachouza.

Watu wanathamini sana elimu yoyote wanayoipata, na kadiri unavyowapa elimu, ndivyo wanavyojenga imani kwako na kuwa tayari kukusikiliza. Pia hutatumia nguvu nyingi kuuza, kwa sababu tayari wateja wako wanakujua.

ANGALIZO; Njia hii inahitaji muda mpaka uanze kuona matokeo yake. Wafanyabiashara wengi wanakosa subira, wanataka wafanye kitu leo na majibu yawe kesho, kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Lakini uzuri wa njia hii ni kwamba ikishaanza kukupa matokeo mazuri, matokeo hayo yanaendelea kukua kwa kasi kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Watu wakishakuelewa na kukuamini, wakishaanza kuwa tayari kununua kwako, wanaendelea kununua kwako na hao watakusaidia kuwapata wateja wengi zaidi.

Kwa ushauri zaidi jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii na blogu katika kutangaza biashara yako tuwasiliane kwa wasap namba 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

  1. Pingback: Matokeo Ya Kutangaza Biashara Kwenye Intaneti Hutayaona Haraka Kama Unavyotaka. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Dunia Ya Sasa, Kila Kitu Kinaanza Na Maudhui, Kisha Kuwafikia Wengi Zaidi. | MTAALAMU Network

Leave a Reply