Sema Kitu Kimoja Kwa Wakati, Kusema Mengi Kunawachanganya Watu.

Changamoto kubwa kwenye uandishi wa aina yoyote ile, hasa kwa wale wanaoanza, ni kwenye kupangilia vizuri mtiririko wa mawazo ambayo mtu anaandikia.

Watu wengi ni kama wanatapika kwenye ukurasa wanaoandika. Wao kila kinachokuja kwenye mawazo yao wanakiweka pale.

Wengine wanakuwa na vitu vingi vya kusema, na hivyo kutaka vyote vionekane pale wanapoandika. Hii ipo sana kwenye uandishi wa matangazo na nakala za kuuza kitu. Mtu anakuwa na mengi ambayo anataka yote yaonekane.

Sasa iko hivi, kadiri unavyokazana kusema vitu vingi kwa wakati mmoja, ndivyo inavyokuwa vigumu kwa watu kukusikia na kukufuatilia. Unapokazana kusema mengi kwa wakati mmoja, watu wanashindwa kujua wafuatilie lipi na hivyo kukata tamaa moja kwa moja.

abc

Unapokuwa na mengi ya kusema au kuandika, angalia lipi lenye umuhimu kwa wakati huo, kisha sema hilo. Lieleze kwa kina na hakikisha anayesoma au kukusikiliza anakuelewa vizuri. Hayo mengine yaseme kwa wakati wake.

Andika makala inayobeba wazo kuu moja, ambalo utalielezea vizuri na kumpa mtu hatua ambazo atachukua. Kwa njia hii wengi wataweza kukufuatilia na kujifunza na hatimaye kuchukua hatua. Lakini unapokazana kuandika mambo mengi kwa pamoja, mtu anachanganyikiwa, asijue afanye lipi na kuacha lipi.

Kama unatoa tangazo, basi elezea kitu kikuu kimoja, ambacho kitakuwa na ushawishi kwa wale ambao unawalenga. Eleza kile muhimu kabisa na hatua za mtu kuchukua ili kupata kile ambacho unataka apate. Na kama yapo mengine mengi anayapata, angalia namna ya kumwambia mtu yapo bila ya kuharibu na kuchafua tangazo lako.

SOMA; Jinsi Unavyoweza Kupata Mawazo Ya Kuandika Makala Kila Siku Kwenye Blog Yako.

Unaweza pia kufikiria kwenye maelekezo, kitu chochote ambacho unakitolea maelekezo, kadiri unavyokazana kueleza mambo mengi kwa wakati mmoja, ndivyo unavyowachanganya zaidi watu badala ya kuwaelekeza. Kama unatoa maelekezo, angalia mwisho mtu anapaswa kufika wapi, kisha angalia njia moja rahisi ya kumfikisha pale na mpe hiyo.

Uandishi wa makala, matangazo, maelekezo, mchakato na vingine vingi, kadiri unavyokazana kuweka mambo machache, ndivyo watu wanakuelewa na kuweza kuchukua hatua.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply