Kuna Watu Kamwe Hawatanunua Unachouza, Elewa Hilo Na Songa Mbele.

Ujasiriamali wa taarifa ni moja ya aina ngumu sana za ujasiriamali kuliko wengi wanavyofikiri.

Hii ni kwa sababu, kabla hujamuuzia mtu maarifa na taarifa ulizonazo, unahitaji kwanza kumpa maarifa na taarifa nyingi za bure. Hata kama wewe ni mwandishi wa vitabu, na unategemea kuchapa na kuweka kwenye maduka ya vitabu, kama unataka wanunuzi wengi, basi unahitaji njia ya kuwafikia wengi zaidi kwa kutoa maarifa ya bure.

Sasa hapo ndipo mtego ulipo, kwa sababu wengi wanapotoa maarifa hayo ya bure, na watu wakayapokea vizuri na kuyafurahia, hufikiri kwamba watu wote hao lazima watanunua kile ambacho mtu anauza. Hii siyo kweli.

Wapo watu watafurahia maarifa ya bure unayotoa, lakini kamwe hawatanunua chochote unachouza. Tena wengine watakuwa wa kwanza kulalamika pale wanapokosa maarifa unayotoa bure, lakini ukiwaambia wanunue, hawatanunua.

buy books

Lazima uelewe hili ili uweze kusonga mbele. Lazima ujue wapo watu hawatanunua, hata kama ungeamua kuwapa unachouza kwa bei ndogo sawa na bure kabisa.

Unakuta wengi ndivyo tu walivyo, hawana mpango wowote wa kununua. Wengine wanaona hawana haja ya kulipia kwa kuwa tayari wanapata bure.

SOMA; Unachojua Wewe, Wapo Wengi Hawakijui, Washirikishe Utengeneze Kipato.

Ni muhimu sana ukawajua wale wanaonunua ni wapi, na hao kuwapatia thamani kubwa sana kulingana na gharama wanazolipa.

Lakini pia usiwatelekeze wale ambao hawanunui, ni sehemu ya wafuasi na wasomaji wako, endelea kuwapa maarifa na taarifa zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply