Dunia Ya Sasa, Kila Kitu Kinaanza Na Maudhui, Kisha Kuwafikia Wengi Zaidi.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, kama unataka kuwafikia watu wengi, unahitaji kutengeneza maudhui na kuyasambaza kwa njia ambayo yatawafikia wale ambao unawalenga.

Iwe ni kiongozi, mfanyabiashara au msanii, kitakachokufikisha kwa watu ni aina ya maudhui ambayo unayatengeneza na kuyatoa.

Dunia ya sasa, ambapo mitandao ya kujamii ni sehemu kubwa ya maisha ya watu wengi, kitakachowafanya watu waanze kukuangalia na hata wakufikirie ni aina ya maudhui unayoyatoa na kuwashirikisha.

toa maudhui

Unapotoa maudhui yoyote, wapo watu ambao watakubaliana nayo, watu hao wana watu wanaowajua ambao watakubaliana nayo hivyo wanawasambazia. Inakwenda hivyo mpaka unawafikia wengi zaidi.

Kabla hata hujafikiria kuwaambiwa watu wanunue unachotaka kuwauzia, wape maudhui kwanza.

Kabla hujawaomba watu wafanye kile unachotaka wafanye, hata kama ni kukupigia kura, wape maudhui.

Maudhui haya yanaweza kuwa ya mafunzo fulani, maarifa na hata hadithi ambayo ina funzo kubwa kwa mtu.

Maudhui unaweza kuyatoa kwa njia ya maandishi, kama makala, ripoti au maoni. Unaweza kuyatoa kwa njia ya sauti kama hotuba, maongezi, mahojiano au kuimba. Na pia unaweza kuyatoa kwa njia ya picha na video.

Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Chochote unachoweza kufanya, ambacho kitafikisha ujumbe ulionao kwa wale ambao wanauhitaji, kitumie. Lengo lako kuu ni watu wajue uwepo wako, wajue kwa namna gani unaweza kuwasaidia na wahitaji zaidi kile unachofanya.

Ni baada ya kutoa maudhui, ndipo sasa unaweza kuwauliza watu wakusaidie au wafanye kile ambacho unataka wafanye.

Lakini cha kwanza maudhui, hata kama biashara unayofanya ni ya kawaida. Maudhui ndiyo yanawafanya watu wajue uwepo wako, waone kama unawafaa au la.

Weka jitihada kwenye kutengeneza maudhui mazuri, ambayo yataendana na aina ya watu unaowalenga.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply