Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kiuandishi Kabla Ya Kuandika Kitabu.

Waandishi wengi ambao wamekuwa wanaandika vitabu vyao vya kwanza, yapo makosa mengi ambayo wamekuwa wanayafanya, ambayo yanapelekea vitabu wanavyotoa visiwe bora sana.

Japokuwa ni kawaida kukosea kwenye kitu cha kwanza, lakini vipo vitu ambavyo unapaswa kuepuka kuvikosea kwa sababu ni vya kawaida sana katika uandishi.

Uandishi wa vitabu una mambo mengi, kuanzia kuja na wazo, uandishi wenyewe, upangaji wa bei, usambazaji na uuzaji. Leo nataka nikushirikishe machache kwenye hatua ya uandishi, ili uweze kuandika kitabu kizuri, kinachosomekana na chenye mwonekano mzuri.

q

Kwanza kabisa ni ukubwa au urefu wa kitabu.

Wapo watu ambao wanaandika maneno elfu tano au elfu kumi na kusema wameandika kitabu. Hicho siyo kitabu, bali ni makala ndefu au ripoti kama unaweza kuiita hivyo.

Kitabu hasa kinapaswa kuwa na maneno elfu sitini na kijitabu kinakuwa na maneno elfu thelathini.

Hivyo unapopanga kuandika kitabu, hakikisha unaandika siyo chini ya maneno elfu 30.

Elewa hapo nimetumia idadi ya maneno na siyo idadi ya kurasa. Kwa sababu wengi huangalia kurasa ngapi za kitabu, sasa kurasa zinadanganya kwa sababu ukiweka maandishi makubwa, kurasa zinaweza kuonekana nyingi. Tumia idadi ya maneno, haidanganyi.

Jambo la pili ni uchaguzi wa aina ya maneno (fonts) unayopaswa kutumia. Zipo aina nyingi za maneno unaweza kutumia kwenye uandishi, lakini kwa mwonekano mzuri na kwa kila mtu kwa kila kifaa anachotumia, TIMES NEW ROMAN au CALIBRI (BODY) Ni nzuri katika uandishi wa vitabu.

SOMA; Makundi Matatu Ya Wasomaji Wa Kazi Zako Ambayo Unapaswa Kuyajua Ili Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Jambo la tatu ni ukubwa wa maneno unayotumia. Na huu huwa ni kwa namba. Wapo ambao wamekuwa wanatumia maneno makubwa ili kuonekana vizuri, lakini wakati mwingine hayo huharibu mwonekano wa kitabu. Hivyo namba nzuri kutumia ni namba 12 kwa aya za kawaida, 16 kwa kichwa cha habari na namba 14 kwa kichwa kidogo cha habari au kipengele.

Jambo la nne ni idadi ya sura za kitabu. Hata kama kitabu ni kirefu kiasi gani, jitahidi kisiwe na sura nyingi, kuwa na kitabu chenye sura 30 inaweza kumfanya msomaji aone ni kirefu sana na hatamaliza. Badala yake jitahidi kuweka pamoja vile vinavyoendana. Kuwa na sura zisizozidi kumi na kwenye kila sura kuwa na vipengele viwili mpaka vitatu. Kwa mpango huu unampa msomaji mtiririko mzuri.

Zingatia mambo hayo katika hatua ya uandishi wa kitabu na utaweza kuandika kitabu kizuri, kinachovutia kusoma na hata kueleweka na wasomaji wako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply