Monthly Archives: September 2017

Matokeo Ya Kutangaza Biashara Kwenye Intaneti Hutayaona Haraka Kama Unavyotaka.

Kutangaza biashara kwa njia ya intaneti  ni kitu ambacho sasa kimeshaeleweka karibu na kila anayefanya biashara au kutoa huduma mbalimbali. Watumiaji wa intaneti ni wengi kutokana na simu zenye uwezo wa kuingia kwenye intaneti kuwa nyingi.

Pamoja na watu kuelewa na kutumia intaneti katika kutangaza biashara zao, wengi wamekuwa wakipata matokeo ambayo yanawakatisha tamaa.

Wengi wamekuwa wakiingia gharama kubwa kulipia matangazo kwenye mitandao mbalimbali mikubwa ambayo inatembelewa na watu wengi. Lakini matokeo ambayo wamekuwa wanayapata siyo kama walivyotegemea.

Huwa ni matokeo madogo sana ukilinganisha na matarajio yao.

mlm

Ukweli ambao kila mtu anapaswa kuuelewa ni kwamba, kutangaza biashara kwa njia ya intaneti hua hautoi majibu haraka kama wengi wanavyotegemea. Hivyo mtu anapaswa kuwa na uvumilivu mkubwa na kuendelea kutangaza hata kama mwanzoni haoni matokeo yoyote.

Mara nyingi watu wanaona tangazo, lakini hawachukui hatua kwa wakati huo, wanaliona tena wakati mwingine wanaweka kwenye kumbukumbu kwamba mtu huyu huwa anajihusisha na kitu fulani. Siku wakiwa na shida inayohusisha kitu kile, wanakutafuta moja kwa moja.

SOMA; Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Wafanyabiashara na watoa huduma wengi, wamekuwa wanataka wakitoa tangazo hapo hapo watu wengi wawatafute na kununua. Kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa namna yoyote ile. Kuna mtu anaweza kuona matangazo yako mwaka mzima na asinunue chochote, lakini siku akiwa na shida inayohusiana na biashara yako atakutafuta.

Usikate tamaa pale unapotangaza lakini huoni matokeo mazuri. Wewe kazana kuboresha matangazo yako zaidi, yawe yanawalenga watu, kuwasaidia changamoto zao na kuwapa mahitaji yao.

Kazana pia kutengeneza hadithi ambazo zinawafanya watu kufikiria kuhusu wewe. Na inapofika siku wana uhitaji wa kile unachofanya, hawatasita kukutafuta wewe mara moja.

Matangazo ya kwenye intaneti hayatofautiani sana na matangazo ya kawaida, kama vile unavyoweza kuwa unaona bango fulani kwa muda mrefu, au tangazo fulani kwenye tv au redio kwa muda mrefu, hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye intaneti.

Ila kwenye intaneti unaweza kufanya hilo kwa ubora zaidi, kwa kuendelea kubadili na kuboresha tangazo kadiri muda unavyokwenda na namna wateja wanavyoulizia na kueleza changamoto au mahitaji yao.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Jinsi Ya Kutengeneza Uaminifu Kwa Wasomaji Wa Kazi Zako Ili Waweze Kununua Kwako.

Kuna kitu kimoja pekee kinachowapa watu uhakika wa kununua kitu chochote kinachouzwa. Kitu hicho ni uaminifu kwamba kitu kile kitawasaidia kweli kulingana na uhitaji au changamoto zao.

Hili lipo kwenye kila aina ya biashara, na lipo pia kwenye uandishi.

Kama mwandishi, kabla mtu hajawa tayari kununua kwako, anahitaji kupata kwanza uhakika kupitia kazi zako unazompatia bure kabisa. Anataka kuwa na uhakika kama atatoa fedha kununua kitabu au kuhudhuria semina basi ipo thamani kubwa ambayo anakwenda kuipata.

Sasa uaminifu huu huwa hautokei tu, bali unatengenezwa. Na unatengenezwa kulingana na namna unavyofanya kazi zako za uandishi.

Tumekuwa na changamoto kubwa katika zama hizi za ‘likes’ na ‘comments’ ambapo waandishi wamekuwa wakivutiwa kuandika vitu vya kuvutia ‘likes’ na ‘comments’ kwenye mitandao ya kijamii. Hili limekuwa linawafanya kuandika vitu ambavyo vinawavunjia uaminifu wao kwa wasomaji wao.

Angalia kipindi hichi cha leo cha MTAALAMU NETWORK ambapo nimekushirikisha njia bora ya wewe kujenga uaminifu kwa wasomaji wako na wakawa wateja wazuri sana kwako.

Kwa kuangalia kipindi hichi utaepuka kufanya makosa ambayo yanawapoteza wengi, kwa kutaka wasomaji wengi wa haraka, ambapo siyo wanunuaji.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya au kuangalia moja kwa moja hapo chini iwapo kifaa chako kinaruhusu.

Fanyia kazi haya uliyojifunza ili uweze kuwa mwandishi bora na kuwasaidia watu kutatua changamoto zao huku nao wakiwa tayari kukulipa kulingana na chochote unachouza.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Hapo Ulipo Tayari Umekamilika Kama Mwandishi, Anza Kuandika Utaendelea Kuwa Bora Zaidi.

Mwandishi mmoja aliwahi kuandika kwamba iwapo utasoma kitu ulichoandika siku zilizopita na usijishangae, basi wewe siyo mwandishi. Anachomaanisha ni kwamba, kwenye uandishi hakuna ukamilifu. Unachojua na kuamini leo, kinaweza kuwa tofauti kabisa unachojua na unachoamini miaka inayokuja.

Wapo watu wengi ambao wamekuwa wanapenda kuandika, lakini wanaona bado hawajakamilika. Mwingine atakwenda hatua mpaka ya kuwa na blog au ukurasa wa kuandika, lakini haandiki.

Writing4

Anachojiambia ni kwamba bado hajawa tayari, akiamini kuna hatua akifikia basi anakuwa mwandishi aliyekamilika na kuweza kaundika vizuri.

Ukweli ni kwamba, kama unapenda kuandika, unachopaswa kufanya ni kuandika. Kwa sababu hapo ulipo, tayari umekamilika. Tayari una kila unachohitaji ili kuwa mwandishi bora, unachopaswa kufanya ni kutumia kile ambacho kipo ndani yako.

Ndiyo utahitaji kuendelea kuwa bora zaidi, utaendelea kujifunza zaidi na kuendelea kubadilika kadiri muda unavyokwenda. Lakini hilo halipaswi kukuzuia wewe usianze kuandika.

SOMA; Unawezaje Kuandika Pale Unapokuwa Hujisikii Kuandika?

Hata ungesubiri muda mrefu kiasi gani, bado utakapoanza kuandika, utahitajika kujiboresha zaidi, utahitaji kujifunza zaidi.

Hivyo kama ilishawahi kukutokea kwenye mawazo yako kwamba unapenda kuandika, au unaweza kuandika na wengine wakanufaika na unachoandika, basi ishia hapa na nenda kaandike. Kaandike kwenye ukurasa wako kwenye mitandao ya kijamii na muhimu zaidi andika kwenye blogu yako. Kama huna blog basi tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 na nitakupa njia bora na rahisi ya wewe kuwa na blog na kuweza kaundika kila siku.

Anza kuandika sasa, usisubiri kesho au mpaka uwe tayari, upo tayari, unachohitaji ni kuanza.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Wanunuaji Wa Mtandaoni Wapo Sehemu Hii Muhimu.

Watu wengi wanaouza bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, huwa wanapata changamoto pale wanapojaribu kuuza moja kwa moja.

Wengi hufikiri kwa sababu wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii basi wanaweza kuuza kitu chochote kwa wafuasi hao na wakanunua. Hili huwa wanalidhibitisha pale wanapojaribu kuuza moja kwa moja kwa njia ya mtandao na ndiyo wanagundua hata wengi wanasema wanahitaji, siyo wanunuaji.

uza mtandaoni

Kama unapanga kuuza bidhaa au huduma zako kwa njia ya mtandao wa intaneti, unapaswa kuelewa wapi walipo wanunuaji wako. Wengi sana hawapo kwenye mitandao ya kijamii, bali wapo kwenye mtandao wako ambao unapaswa kuwa umeutengeneza.

Hapa ninachomaanisha ni kwamba, licha ya kuwa na wafuasi kwenye mitandao ya kijamii, unapaswa kutengeneza wafuasi wengine ambao watakuwa kwenye mtandao wako binafsi.

Hawa ni watu ambao watakuwa wanakufuatilia kwa karibu, wanakusikiliza na wanachukua hatua kwenye yale ambayo unawashauri. Hawa wanakuwa wafuasi wako wa ukweli na pale unapokuwa na huduma au bidhaa inayoweza kuwasaidia, ni rahisi wao kununua kutoka kwako.

Mtandao wako binafsi unahusisha vitu viwili, blog na email list.

Blog ndipo unapoweka maarifa ambayo mtu yeyote anayekutafuta kwenye mtandao anapelekwa kwenye blog yako. Hapo ndipo mtu anaweza kukuta kazi zako zote iwapo umekuwa unaziweka hapo. Katika blog yako, mtu hakutani na kelele na usumbufu mwingine anaokutana nao kwenye mitandao ya kijamii.

Email list ni mfumo wa kuwa na mawasiliano ya wasomaji na wafuatiliaji wako, ambao mara kwa mara unaendelea kuwasiliana nao kwa kuwatumia maarifa na taarifa moja kwa moja kwenye email zao. Pia unaweza kuwa na makundi maalumu ya wasomaji na wafuatiliaji wako kwenye mitandao kama wasap na telegram. Hapa muhimu sana ni ule ukaribu uliopo kati yako wewe na wasomaji na wafuatiliaji wako. Ukaribu ambao siyo rahisi kupatikana kwenye itandao ya kijamii.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao.

Kazana sana kutengeneza ukaribu, wa kuwapa taarifa na maarifa wasomaji na wafuatiliaji wako moja kwa moja. Wape taarifa na maarifa ambayo yanawasaidia kuchukua hatua, kisha wauzie kile ambacho kinawasaidia zaidi.

Wanunuaji kwenye mtandao wa intaneti wapo kwenye mtandao wako binafsi unaoweza kuutengeneza ndani ya mtandao wa intaneti. Weka nguvu zako katika kutengeneza blog, email list, makundi ya wasap na/au telegram kabla hujafikiria kuwauzia watu vitu.

Kama unahitaji blog au email list na namna ya kutumia kuuza kwenye mtandao wa intaneti, tuwasiliane kwa wasap namba 0717 396 253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Saikolojia Ya Mitandao Ya Kijamii Inayowazuia Wengi Kuwa Na Blogu.

Jambo moja ambalo nimekuwa nasisitiza sana kwa mtu yeyote ambaye anafanya ujasiriamali wa taarifa ni kuwa na blogu. Lakini bado wengi wamekuwa hawaelewi hilo, kwa sababu wanashindwa kuivuka saikolojia ya mitandao ya kijamii.

Huwa nafananisha maisha yetu kwenye mtandao na maisha yetu ya uhalisia. Huwa nasema mitandao ya kijamii ni sawa na kijiweni ambapo watu wanakutana kupiga hadithi za hapa na pale. Na blogu yako ndiyo nyumbani kwako, ambapo watu wana uhakika wa kukupata pale.

Unapokuwa na shida na mtu, sehemu ya uhakika ya kumpata ni nyumbani kwake na siyo kwenye kijiwe ambacho huwa unamwona mara kwa mara.

like za facebook

Kadhalika kwenye mtandao, uwepo wako kwenye mitandao ya kijamii ni sawa na kuwepo kijiweni. Kwa sababu siyo muda wote watu wanakuona pale, wanakuoa kwa muda mchache wakati wao wanapita na mambo yao.

Unapokuwa na blogu, hapo sasa ndiyo nyumbani kwako. Muda wowote mtu anapokuja kwenye blogu yako, anakutana na kazi zako. Mtu anapokuwa kwenye blogu yako, anakuwa na wewe moja kwa moja na hana usumbufu mwingine kama anaokutana nao kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa watu wengi wamekuwa wakipenda kutumia mitandao ya kijamii na hata wakianzisha blogu huwa wanaziacha ndani ya muda mfupi. Hii inatokana na saikolojia ya mitandao ya kijamii. Mitandao hii imetengenezwa kisaikolojia, ambapo unapoweka kitu chenye hisia fulani, unawavutia watu ‘kulike’ na ‘kukomenti’.

Hivyo unapoandika kitu au kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii, utapata wengi wanaolike na kukomenti, tofauti na ukifanya hivyo kwenye blogu. Hili linawafanya wengi kukimbilia kwenye likes na comments na kuacha kujenga jukwaa muhimu zaidi kwenye blogu.

Kuweza kuishinda saikolojia hii, unahitaji kufikiria mbali zaidi ya likes na comments. Kwenye mitandao ya kijamii unaweza kupata hizo likes na comments, lakini kujenga mahusiano mazuri baina yako na wasomaji wako huwa ni vigumu. Kwa sababu usumbufu ni mkubwa na mambo ni mengi.

SOMA; Usiangalie Umepata Likes Ngapi, Angalia Umegusa Watu Wangapi.

Lakini unapokuwa na blogu yako, unapata nafasi ya kujenga mahusiano bora sana, unapata nafasi ya kuwageuza wasomaji wako kuwa mashabiki wako na baadaye kuwa wateja wako.

Lakini kama bado unataka likes na comments kwa sababu ndiyo zinakufanya uone kweli wewe ni wa muhimu, basi fanya yote. Andika kwenye blog na andika kwenye mitandao ya kijamii. Kwa kufanya yote kwa pamoja, itakupa nafasi ya kujenga jukwaa lako ambalo ni blogu yako.

Usipotezwe na vitu ambavyo siyo muhimu ukaacha kujenga kitu muhimu. Unapochagua kufanya ujasiriamali wa taarifa, jua kujenga wafuasi na wateja ni zaidi ya likes na comments kwenye mitandao ya kijamii. Lazima uweke kazi ya kutosha kwenye blogu yako, ili watu waweze kuitembelea mara kwa mara na kuwa tayari kununua chochote unachouza.

Ni mara chache sana watu wananunua moja kwa moja kutoka kwenye mitandao ya kijamii. Lakini kwenye blogu yako, wengi watanunua kwa sababu tayari wanakujua kiundani na kazi zako wanazijua vizuri.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Sema Kitu Kimoja Kwa Wakati, Kusema Mengi Kunawachanganya Watu.

Changamoto kubwa kwenye uandishi wa aina yoyote ile, hasa kwa wale wanaoanza, ni kwenye kupangilia vizuri mtiririko wa mawazo ambayo mtu anaandikia.

Watu wengi ni kama wanatapika kwenye ukurasa wanaoandika. Wao kila kinachokuja kwenye mawazo yao wanakiweka pale.

Wengine wanakuwa na vitu vingi vya kusema, na hivyo kutaka vyote vionekane pale wanapoandika. Hii ipo sana kwenye uandishi wa matangazo na nakala za kuuza kitu. Mtu anakuwa na mengi ambayo anataka yote yaonekane.

Sasa iko hivi, kadiri unavyokazana kusema vitu vingi kwa wakati mmoja, ndivyo inavyokuwa vigumu kwa watu kukusikia na kukufuatilia. Unapokazana kusema mengi kwa wakati mmoja, watu wanashindwa kujua wafuatilie lipi na hivyo kukata tamaa moja kwa moja.

abc

Unapokuwa na mengi ya kusema au kuandika, angalia lipi lenye umuhimu kwa wakati huo, kisha sema hilo. Lieleze kwa kina na hakikisha anayesoma au kukusikiliza anakuelewa vizuri. Hayo mengine yaseme kwa wakati wake.

Andika makala inayobeba wazo kuu moja, ambalo utalielezea vizuri na kumpa mtu hatua ambazo atachukua. Kwa njia hii wengi wataweza kukufuatilia na kujifunza na hatimaye kuchukua hatua. Lakini unapokazana kuandika mambo mengi kwa pamoja, mtu anachanganyikiwa, asijue afanye lipi na kuacha lipi.

Kama unatoa tangazo, basi elezea kitu kikuu kimoja, ambacho kitakuwa na ushawishi kwa wale ambao unawalenga. Eleza kile muhimu kabisa na hatua za mtu kuchukua ili kupata kile ambacho unataka apate. Na kama yapo mengine mengi anayapata, angalia namna ya kumwambia mtu yapo bila ya kuharibu na kuchafua tangazo lako.

SOMA; Jinsi Unavyoweza Kupata Mawazo Ya Kuandika Makala Kila Siku Kwenye Blog Yako.

Unaweza pia kufikiria kwenye maelekezo, kitu chochote ambacho unakitolea maelekezo, kadiri unavyokazana kueleza mambo mengi kwa wakati mmoja, ndivyo unavyowachanganya zaidi watu badala ya kuwaelekeza. Kama unatoa maelekezo, angalia mwisho mtu anapaswa kufika wapi, kisha angalia njia moja rahisi ya kumfikisha pale na mpe hiyo.

Uandishi wa makala, matangazo, maelekezo, mchakato na vingine vingi, kadiri unavyokazana kuweka mambo machache, ndivyo watu wanakuelewa na kuweza kuchukua hatua.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Umuhimu Wa Kutangaza Kazi Zako Kwenye Mtandao Wa Intaneti.

Upo usemi kwamba kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, huu ni usemi ambao umekuwa unatumiwa na wengi kama sababu ya kutotangaza kazi zao kwa nguvu.

Katika zama tunazoishi sasa, zama za mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, unahitaji kutenga muda wa kutosha wa kutangaza kazi zako.

Iwe unafanya biashara au una kipaji kama cha uandishi, uimbaji, uchoraji na kadhalika, unahitaji kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia watu wengi zaidi.

Hii ni kwa sababu kuna kelele nyingi mno, wapo watu wengi wanaosambaza maarifa mengi ambayo yanawazuia wale unaowalenga kujua kile unachowapatia. Hivyo tenga muda kutangaza kazi zako na itakulipa.

Zipo njia mbili za kutangaza kazi zako kwenye mitandao ya kijamii, moja ni ya kulipia na nyingine ni ya bure. Jinsi ya kutumia njia hizi nimeeleza kwa kina kwenye somo letu la leo.

Karibu ujifunze umuhimu wa kutangaza kazi zako na jinsi ya kufanya hivyo kwa kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Angalia somo hili la leo kwa kubonyeza maandishi haya au kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya kosa kubwa sana wanapotangaza biashara zao kwenye mitandao ya kijamii. Wanachofanya ni kuwasukumia watu picha za bidhaa zao. Wanakazana kutuma picha nyingi kupitia mitandao ya kijamii na wakati mwingine hata kuwatumia watu moja kwa moja kwenye mitandao kama wasap.

Njia hii inaweza kuonekana kuleta matokeo kiasi mwanzoni, lakini baadaye inakuwa usumbufu na haileti matokeo. Kwa sababu ni usumbufu na wengi wanaokuwa wanatumiwa picha zile hawajali kabisa kuhusu hizo picha wanazotumiwa.

Kama wewe ni mfanyabiashara, ambaye unatumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako, basi acha mara moja kuwasukumia watu picha kila wakati. Watu watajifunza kupuuza picha zako na haijalishi utatuma nyingi kiasi gani, haitakuongezea mauzo.

kutangaza mitandaoni

Njia bora kabisa ya kutangaza bidhaa zako kwenye mitandao ya kijamii ni kuwafikia wale ambao wanajali. Badala ya kumsukumia kila mtu picha nyingi, unachagua wale wanaojali, ambao wao wenyewe watakutafuta wakitaka bidhaa zako ambazo zitawasaidia.

Kwa njia hii, kwanza unahitaji kuwajua wateja wa biashara yako ni watu wa aina gani. Ukishawajua, jua changamoto zao kwenye kile unachouza ni nini? Vitu hivi viwili vitakuwezesha wewe kuwatengenezea sababu ya kukutafuta na kununua kwako.

Baada ya kujua vitu hivyo viwili, unahitaji kutengeneza maudhui ambayo yanawasaidia wateja wako kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye eneo la maisha yao linalohusisha biashara yako. Hapa unawaandalia taarifa na maarifa muhimu kwao, ambayo yatawawezesha kufanya maamuzi sahihi kwao.

SOMA; Chagua Tatizo Unaloweza Kuwasaidia Watu Kutatua Kupitia Maarifa Sahihi.

Kwa njia hii, utatengeneza watu wanaokuamini wewe kama mshauri na mwalimu wao, na hivyo utakapowaambia kuna bidhaa unauza, hawatasita kununua. Hii inawafanya wao wakuulize kama kuna bidhaa unayouza, kabla hata hujawaambia kama unauza. Huwezi kuwachosha watu kwenye hili, kwa sababu wao ndiyo wanakutafuta wewe kupata maarifa na taarifa badala ya wewe kuwasukumia matangazo.

Swali ni je unawezaje kufanya hivyo?

Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwaelimisha watu kuhusiana na biashara unayofanya. Pia unaweza kuwa na blogu ambayo itakuwa inatoa elimu inayohusiana na biashara yako. Hapo utaweza kuwapa watu maarifa na taarifa na pia kuwaeleza juu ya kile unachouza.

Watu wanathamini sana elimu yoyote wanayoipata, na kadiri unavyowapa elimu, ndivyo wanavyojenga imani kwako na kuwa tayari kukusikiliza. Pia hutatumia nguvu nyingi kuuza, kwa sababu tayari wateja wako wanakujua.

ANGALIZO; Njia hii inahitaji muda mpaka uanze kuona matokeo yake. Wafanyabiashara wengi wanakosa subira, wanataka wafanye kitu leo na majibu yawe kesho, kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Lakini uzuri wa njia hii ni kwamba ikishaanza kukupa matokeo mazuri, matokeo hayo yanaendelea kukua kwa kasi kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Watu wakishakuelewa na kukuamini, wakishaanza kuwa tayari kununua kwako, wanaendelea kununua kwako na hao watakusaidia kuwapata wateja wengi zaidi.

Kwa ushauri zaidi jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii na blogu katika kutangaza biashara yako tuwasiliane kwa wasap namba 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Muda Wa Kuandika Upo Wa Kutosha, Ni Wewe Kusema NDIYO Na HAPANA.

Kwenye ujasiriamali wa taarifa, kazi kubwa sana unazopaswa kufanya ni mbili, kuandika na kusoma sana. Ninaposema sana namaanisha kweli SANA. unahitaji kuandika kila siku, wakati mwingine kuandika mara nyingi kwa siku moja. Lakini pia unahitaji kusoma ili kujifunza na kupata uelewa mkubwa kwenye kile unachoandika.

Hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu huona hawawezi kufanya hivyo, kutokana na kukosa muda kwa majukumu mengine ambayo tayari wanayo.

Huhitaji muda mwingi wa siku yako kuweza kufanya majukumu hayo mawili muhimu. Bali unahitaji angalau masaa mawili kwa siku. Saa moja ya kuandika na saa moja ya kusoma. Kadiri unavyokwenda unaweza kuongeza muda zaidi.

Sasa ukweli ni kwamba, muda huwa upo, kinachofanya muda ukosekane ni vipaumbele ambavyo tunaweka kwenye muda tulionao. Vile ambavyo umevipa kipaumbele kikubwa, ndiyo vinachukua muda wako mwingi.

time to write

Hii ina maana kwamba iwapo utaweka kuandika na kusoma kama kipaumbele kikubwa kwako, basi utapata muda wa kufanya hayo. Kwa sababu ukishaweka hayo kama kipaumbele, kuna ambayo unafanya sasa utahitaji kuacha kuyafanya.

Ni swala la kusema NDIYO kwenye kuandika na kusoma na kusema HAPANA kwenye mambo mengine unayofanya sasa ambayo siyo muhimu mno.

Hivyo ukiangalia kwa upande huo wa vipaumbele, swali siyo napata wapi muda wa kuandika na kusoma, swali linakuwa kipi muhimu kwangu zaidi ya kusoma na kuandika na kipi ambacho siyo muhimu.

Kinachowaponza wengi ni wanataka maisha waliyonayo sasa yaendelee hivyo hivyo bila ya kubadilika, halafu pia waweze kusoma na kuandika, kitu ambacho hakiwezi kutokea kabisa. Lazima uache baadhi ya vitu unavyofanya sasa, ili kuweza kupata muda wa kuandika na kusoma.

Hivyo basi, kuanzia sasa usiseme huna muda, bali sema wazi kabisa kile ambacho unajiambia huna muda wa kukifanya, ni siyo cha muhimu kwako kufanya. Kikishakuwa muhimu, muda upo na utakifanya.

Weka ujasiriamali wa taarifa kama kitu muhimu kwako na kila siku utapata muda wa kukuza ujasiriamali wako huo.

SOMA; Tenga Muda Wa Kutosha Kutangaza Kazi Yako Ya Uandishi, Hakuna Atakayekufanyia Hilo.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Watu Huwa Hawathamini Sana Vitu Vya Bure, Jifunze Kuweka Thamani Zaidi Na Kutoza Gharama.

Unapoanza kuingia kwenye ujasiriamali wa maarifa, kwa kutoa taarifa na maarifa kwa njia ya mtandao wa intaneti, vitu vingi utakuwa unatoa bure. Utaandika makala nyingi za bure, na huenda ukaandika vitabu na kuvitoa bure kwa wasomaji wako.

Hii ni njia nzuri ya kuwafanya watu wakujue na wajue kazi zako, kwa sababu ni vigumu kuanza kuwauzia watu ambao bado hawajakujua.

Lakini baada ya muda, unahitaji kujifunza kuweka thamani kubwa zaidi kwenye maarifa unayotoa na kisha kutoza gharama. Hii siyo kwa sababu tu unataka kutengeneza kipato, bali utawasaidia wengi zaidi.

paid-content-big1

Watu huwa hawathamini sana vitu vya bure. Kwa mfano kama umeandika kitabu na ukakitoa bure, ni wachache sana watakaokisoma mpaka mwisho. Wengi watakichukua na kukaa nacho, wakiamini siku wakipata muda watakisoma. Lakini muda huwa haupatikani.

Lakini iwapo utatoza gharama kwenye kitabu hicho, wengi watakaokinunua watalazimika kukisoma ili kupata thamani ya fedha walizolipia. Hii inawafanya wapate maarifa uliyotoa na kuweza kuyafanyia kazi.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuuza Maarifa Yanayopatikana Bure Kabisa Kwenye Mtandao.

Hili ni jambo muhimu sana unalopaswa kulifanyia kazi kwenye biashara yako ya kuuza maarifa, kwa sababu wengi wamekuwa wakivutiwa na kutoa vitu vingi vya bure na kushangaa mbona watu wanauliza maswali ambayo walipaswa kuwa wanayajua iwapo wangekuwa wamesoma ulichowaandikia.

Kuna tofauti kubwa kwenye kitu cha bure na cha kulipia. Toa maarifa mengi bure ili watu wakujue na kujua unawezaje kuwasaidia, lakini pia toa maarifa mengine ya thamani kubwa mno na toza gharama.