Kitu Pekee Unachopaswa Kufanya Kama Mwandishi Ni Kuwa Bora Zaidi Kila Siku.

Kwenye uandishi, epuka sana vitu hivi viwili, kuiga wengine na kushindana na wengine. Vitu hivyo viwili havitakusaidia kupiga hatua na mbaya zaidi vitakuondoka kwenye njia ya mafanikio kiuandishi. Nilishakuandikia hilo kwa kina kwenye makala hii, lakini nakukumbusha tena, kwa sababu ni muhimu zaidi.

Kitu pekee muhimu sana unachopaswa kufanya wewe mwandishi ni kuwa bora zaidi kila siku.

Kila siku mpya, kazana kuwa bora kuliko siku iliyopita. Jiangalie wewe wa jana na leo amua kuwa bora zaidi.

Na njia pekee ya kuwa bora zaidi kila siku inahusisha vitu viwili, kujifunza na kuandika, kila siku.

Writing4

Jifunze kwa kusoma sana, soma vitabu vingi, soma machapisho mbalimbali. Pia jifunze kutokana na uzoefu wako wa maisha na kile unachokifanya. Jifunze kutoka kwa kila unayekutana naye, kwa mazuri au mabaya anayofanya. Jifunze kutokana na asili, uangalie mti na jifunze mti ule unawezaje kuendesha maisha yake, kadhalika viumbe wengine wanavyoishi.

Unahitaji kuandika kila siku, andika kwa wingi na andika kwa ubora. Sitaeleza hilo sana kwa sababu nimelieleza kwenye makala hii.

Muhimu sana ambacho nataka uondoke nacho hapa ni hichi;

Kazana kuwa bora kila siku, siyo kuwa bora zaidi ya wengine, bali kuwa bora leo kuliko ulivyokuwa jana.

Unavyozidi kuwa bora ndivyo unavyowafikia wengi zaidi na ndivyo kipato chako kinaongezeka zaidi.

Nimalize kwa kukupa tahadhari, wapo watakaokupinga na kukukatisha tamaa, katika harakati zako za kuwa bora. Achana nao na kazana kuwa bora zaidi. Hilo pekee ndiyo litakuwezesha kupiga hatua, kwenye uandishi na hata chochote kile unachofanya.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Kitu Pekee Unachopaswa Kufanya Kama Mwandishi Ni Kuwa Bora Zaidi Kila Siku.

  1. Pingback: Unasubiri Nani Akuchague Kuwa Mwandishi? Huyu Ndiye Anayekuchelewesha. | MTAALAMU Network

Leave a Reply