Kama Huandiki Hukitendei Haki Kizazi Kinachokuja.

Moja ya maeneo ambayo wenzetu wa nchi zilizoendelea wametuzidi kwa mbali sana, ni kwenye maandiko. Wenzetu wanaandika sana, na wanaandika kwa ajili ya vizazi vinavyokuja.

Uandishi wao siyo lazima uwe wa kitaalamu au wa kiuvumbuzi, bali uandishi wao ni wa uzoefu wao wa kila siku, namna walivyoweza kuondoka kwenye nyakati ngumu na kufika nyakati nzuri.

Kila mtu ambaye anafanikiwa kufanya kitu fulani, anaandika kitabu au majarida ambayo yanaelezea jinsi alivyoweza kufanya.

Maandiko hayo husomwa na vizazi vinavyofuata na kujifunza jinsi vizazi vilivyowatangulia vilivyofanya mambo yao.

Kwa njia hii wanakuwa tayari wana mahali pa kuanzia na kuweza kuboresha zaidi.

uandishi kwa vizazi vijavyo

Lakini kwa huku kwetu, mtu akishaondoka hapa duniani, basi uzoefu wake na hata kile alichojifunza na kufanyia kazi kinapotea. Zinabaki hadithi pekee ambazo kadiri muda unavyokwenda zinapoteza uhalisia na kupotea kabisa.

Lakini mtu anapokuwa ameandika, watu wanakuwa na sehemu ya kufanya rejea kila wakati wanapotaka kujifunza.

Hivyo basi, kama wewe huandiki sasa, maana yake unadhulumu vizazi vinavyokuja. Maana yake yote uliyoyapitia na kuweza kushinda, yote uliyopambana nayo yanakuja kupotea pale unapoondoka hapa duniani.

Hii siyo sahihi kabisa, na siyo sawa kwa vizazi vijavyo.

Hii ndiyo sababu nimekuwa nasisitiza sana tuandike, tuandike uzoefu wetu, tuandike yale tunayokutana nayo na tukajifunza.

SOMA; Soma Maandiko Ya Miaka Mia Tano Iliyopita, Na Utajifunza Kitu Hiki Kikubwa Sana.

Kama huwezi kuandika kitabu na ukakichapa usiwe na wasiwasi, unaweza kuwa na blogu ambayo unaandika kila siku au kila mara kadiri unavyojifunza na kufanyia kazi. Baadaye unaweza kugeuza blogu hiyo kuwa kitabu. Au kama siyo wewe utakayefanya hivyo, basi vizazi vinavyokuja, vitafanya hivyo.

Muhimu ni wewe uandike, andika kushirikisha uzoefu wako, changamoto unazokutana nazo na yale unayojifunza ambayo yanaboresha maisha yako.

Kama mpaka sasa hujaanza kuandika, tuwasiliane kwa wasap 0717396253 nikupe utaratibu mzuri wa kuwa na blog utakayoweza kuitumia kuandika.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Leave a Reply