Unasubiri Nani Akuchague Kuwa Mwandishi? Huyu Ndiye Anayekuchelewesha.

Kitu kimoja ambacho nimekuwa nawasisitiza watu ni hichi, hakuna mtu wa kukuzuia zama hizi, hasa pale unapofikiria kufanya kile unachopenda kufanya.

Zamani ilikuwa kuwa mwandishi mpaka wachapaji wakuchague, mpaka wamiliki wa magazeti na majarida wakukubali.

Kama ulitaka kuwa msanii basi wenye kurekodi wakukubali, vituo vya redio na tv vikukubali ndiyo wananchi wakusikia na wakujue.

Lakini zama hizi, hakuna kikwazo chochote, ni wewe mwenyewe uchague kubaki nyuma.

tofauti uandishi

Kuna fursa iliyopo wazi kwa kila mtu kufanya kile anachopenda kufanya na kuwafikia wengi, bila kusubiri mpaka akubaliwe na watu fulani au wamchague.

Mtandao wa intaneti umefanya rahisi kwa kila mtu kuweza kuchukua hatua. Umetoa fursa ya wazi ya kila mwenye wazo, mwenye kuweza kufanya kitu kuchukua hatua hiyo na kuwafikia wanaotaka kitu hicho.

Lakini cha kushangaza, wapo watu katika zama hizi wanasubiri kuchaguliwa. Wapo watu wanasubiri mtu awaambie nini cha kufanya. Wapo watu wanasubiri mtu awaambie wanaweza kufanya ndiyo wafanye. Na wapo watu ambao wanasubiri watu wawaambie wanastahili kufanya, ndiyo waanze kufanya.

SOMA; Kitu Pekee Unachopaswa Kufanya Kama Mwandishi Ni Kuwa Bora Zaidi Kila Siku.

Huku ni mtu kuchagua kujichelewesha, kwa sababu hakuna anayepaswa kufanya hivyo ila wewe mwenyewe. Na mbaya zaidi, hakuna aliye tayari kufanya hivyo kama wewe mwenyewe hutachukua hatua. Na kwa dunia ya sasa ambayo kila mtu anapiga kelele, hakuna mwenye muda wa kukutafuta na kukupata wewe.

Jichague wewe mwenyewe, ona unastahili na tumia teknolojia kuweza kutoa kile ulichonacho, kufanya unachopenda na kuwafikia wengi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Unasubiri Nani Akuchague Kuwa Mwandishi? Huyu Ndiye Anayekuchelewesha.

Leave a Reply