Author Archives: mtaalamu

Kila Wazo Linahitaji Kuboreshwa Zaidi, Hivyo Anzia Popote Na Endelea Kuwa Bora.

Moja ya vitu ambavyo vinawazuia watu kuchukua hatua, ni kutaka ukamilifu. Watu wengi wamekuwa wanajiona hawajakamilika hivyo kutokuanza, wanasubiri mpaka waone wapo tayari. Kitu ambacho huwa hakitokei.

Kitu kikubwa ambacho kinawafanya wengi kusubiri, ni kuamini kwamba bado hawajapata wazo bora kabisa kwao kufanyia kazi. Ni kawaida kwenye biashara, na hata kwenye uandishi na sanaa pia.

Mtu anakuwa anataka kuandika, iwe ni kitabu au makala, lakini hafanyi hivyo kwa kuona bado hajapata wazo zuri kabisa la kuandikia. Hivyo anasubiri mpaka apate wazo zuri kabisa ndiyo aandike. Kitu ambacho huwa hakitokei kabisa.

WriteYourStory

Kuondokana na hali hii, ili mtu uweze kuanza mara moja ni kujipa ruhusa.

Jipe ruhusa ya kuanza na wazo la kawaida sana, anza na kitu cha kawaida, lakini kazi yako kubwa ni moja, kuendelea kuwa bora zaidi.

Unaanza na wazo la kawaida, lakini unaendelea kukazana kuwa bora zaidi. Unakazana kuangalia maeneo ya kuboresha na kuchukua hatua.

Faida ya kutumia njia hii ni kujifunza kwa vitendo. Kwa mfano unapoanza na wazo la kawaida na kuendelea kujiboresha, utajifunza moja kwa moja kutoka kwa wale wanaopokea unachofanya.

SOMA; Kama Unasema Huna Muda Wa Kuandika, Nihakikishie Kwanza Hufanyi Vitu Hivi Vitano, Nitakuelewa.

Huenda mwanzoni ulifikiri watu wanataka kitu fulani, lakini unapokuja kufanya unagundua wanachotaka ni tofauti kabisa na ulichofikiri wewe, hivyo unahitajika kuboresha zaidi.

Ukisema usubiri mpaka upate wazo bora kabisa, utasubiri sana, na hata ukipata wazo hilo bado utahitaji kuliboresha pale unapoanza na kugundua watu wanahitaji tofauti na ulivyofikiri.

Kwa wale ambao wanaandika kitabu na hawajapata wazo zuri la kuandika, nimekuwa nawashauri kuanza na blog kwanza, kaundika kila siku kwa angalau siku 100 kisha kufanya tathmini, kwao wenyewe na kwa wasomaji wa makala zao. hapo wataona kipi ambacho wanaweza kufanya kwa ubora zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kuuza Kwa Uhaba Na Kuuza Kwa Mapenzi, Njia Bora Ya Kutumia Kupata Wanunuzi Wa Kazi Zako.

Uandishi kama zilivyo kazi nyingine, unahitaji wanunuzi, yaani watu ambao wanakubali kazi ya uandishi na kuwa tayari kulipia gharama ili kuipata.

Ubora wa kazi unachangia sana kwenye uuzaji, lakini kitu kingine muhimu kinachochangia ni uwezo wa uuzaji wa mwandishi. Kadiri mwandishi anavyoweza kuwafikia na kuwashawishi wapenzi wa kazi zake kununua, ndivyo anavyoweza kuuza zaidi.

buy books

Katika hili la ushawishi, zipo njia mbili ambazo zinaweza kutumika.

Njia ya kwanza ni hofu, hapa mwandishi anawashawishi wasomaji wa kazi zake kuchukua hatua ili kupata kazi ile kwa sababu wasipochukua hatua wataikosa. Hapa mwandishi anaweza kuweka ukomo wa muda wa kupata kazi zake hizo. Pia anaweza kutoa punguzo la bei ambalo ni la muda maalumu, ambapo watu wanapaswa kuchukua hatua katika muda huo.

Njia ya pili ni mapenzi, hapa mwandishi anatengeneza wasomaji ambao wanapenda sana kazi zake. Wasomaji ambao wanasubiri kwa hamu kila kazi ambayo mwandishi anaitoa. Wanakuwa tayari kulipia na  kupata kazi hiyo. Wasomaji wengine wanaweza kulipia kazi ambayo hata hawaihitaji sana, ila mapenzi yao kwa mwandishi yanawasukuma wao kufanya hivyo.

SOMA; Anza Kumwandikia Mtu Huyu Mmoja, Na Itakuwa Rahisi Kuwafikia Watu 1000.

Njia ya kwanza ni rahisi kutumia, inaweza kuleta wanunuzi wengi ndani ya muda mfupi kununua, lakini haiwezi kutengeneza wafuasi wazuri wa kazi zako za uandishi, au kazi zozote unazotaka kuwa na wanunuaji wa uhakika.

Njia ya pili ni ngumu, inahitaji muda na kazi kuweza kutengeneza wasomaji ambao wanapenda kazi zako na walio na kiu ya kupata kazi zako.

Njia ipi utumie wewe? Tumia njia zote mbili mwanzoni, ila mkazo weka kwenye kutengeneza wasomaji wanaopenda kile unachofanya. Hii itawafanya watu kukufuatilia na pia kuchukua hatua. Kwa sababu tabia zetu binadamu ni kutokuchukua hatua kwa haraka, mpaka tuone kuna kitu tunapoteza. Kadiri unavyokua, unaweza kuegemea upande wa mapenzi zaidi.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Ubora Na Wingi Katika Uandishi, Kipi Cha Kuzingatia?

Katika uandishi, kuna njia mbili ambazo wengi hutumia kupima kazi zao.

Njia ya kwanza ni kuangalia wingi wa kazi, hapa unaangalia zile kazi unazotoa kwa namba. Kama ni makala basi unaangalia makala ngapi umeandika. Kama ni vitabu unaangalia vitabu vingapi. Kikubwa hapo ni wingi wa kazi ambazo mtu unatoa.

Njia ya pili ni kuangalia ubora wa kazi unazotoa. Hapa unaangalia kile ulichoandika kina ubora kiasi gani, watu wamekipokeaje, kimekuwa maarufu kiasi gani na vigezo vingine vya ubora.

Wingi na ubora vinaonekana kama kwenda kinyume. Yaani kaka kazi zikiwa nyingi basi ubora wake unashuka, na kama kazi zikiwa bora basi siyo nyingi.

wingi na ubora

Hii imekuwa inawafanya waandishi wengi kuamua kutoa kazi chache lakini bora.

Lakini tafiti na hata historia zinaenda kinyume kabisa na hilo. Ukiangalia waandishi ambao wametoa kazi bora kabisa tunazozikubali, walikuwa na kazi nyingi sana ambazo hazikuwa bora.

Hii ina maana kwamba, mwandishi anayeangalia kwenye wingi, katika kazi nyingi anazotoa, chache zitakuwa bora. lakini yule anayeangalia kwenye ubora pekee, anatoa kazi chache, na kwa bahati mbaya zinaweza zisiwe bora.

SOMA; Sababu Nyingine Kwa Nini Unapaswa Kuzalisha Kazi Nyingi Na Bora Zaidi.

Waandishi wengi wenye mafanikio wanakubaliana na dhana kwamba ni vigumu sana wewe mwandishi kupima ubora wa kazi kama ambavyo wasomaji au soko litapokea. Unaweza kuona kazi yako ni bora sana kwa vigezo vyako, lakini soko likapokea tofauti. Unaweza kuona kazi yako ni ya kawaida, lakini soko likaiona ni bora kabisa.

Hivyo ushauri kwa waandishi wote, badala ya kukazana na ubora na kuachana na wingi, tukazane na wingi huku tukizingatia ubora pia.

Kwa maana kwamba, kipaumbele chetu cha kwanza kiwe kutoa kazi nyingi tuwezavyo, na kwenye kila kazi tukazane kuweka ubora kadiri ya uwezo wetu. Halafu tuliachie soko lichague ipi kazi bora kwao.

Hii pia inakwenda kwa kila aina ya sanaa, kazi na hata biashara. Zalisha kwa wingi kwa ubora unaoweza kuzalisha, kisha soko litachagua kile kilicho bora kabisa.

Ukikazana kuangalia ubora pekee, utaacha kazi nyingi na itakuwa vigumu kwako kufikia ubora unaotaka kufikia.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kujitofautisha Na Wengine, Andika Na Kushauri Kile Unachofanyia Kazi Wewe Mwenyewe.

Kadiri mitandao inavyofanya uandishi kuwa rahisi, ndivyo waandishi wanavyokuwa wengi. Hili limekuwa linawapa baadhi wa waandishi wasiwasi kwamba je ipo nafasi ya kusikika iwapo waandishi ni wengi kiasi hichi?

Na jibu ni kwamba nafasi ipo kubwa sana, kama tu utaandika kile ambacho unafanyia kazi wewe mwenyewe.

Hata kama wapo waandishi wengi wanaoandika kuhusu fedha, bado na wewe unaweza kuandika kuhusu fedha, kwa kuwashirikisha wasomaji wako yale unayofanyia kazi kwenye fedha.

Unaweza kuwashirikisha mbinu unazotumia kuweka akiba, kubana matumizi, wapi unawekeza na jinsi gani unaongeza kipato chako.

WriteYourStory

Kwa njia hiyo utakuwa na wasomaji wengi ambao wanakufuatilia kwa sababu wanajua kuna kitu halisi wanajifunza kutoka kwako. Hilo litakutofautisha kabisa na waandishi wengine, kwa sababu unachofanya wewe ni cha kipekee.

Hivyo kujitofautisha kwenye uandishi, kujiepusha na ushindani, andika kile unachofanyia kazi wewe.

Kama unachoandikia hakifai kufanyia kazi wewe moja kwa moja, basi kuwa na mifano hai ya wale wanaokifanyia kazi na maisha yao yakawa bora.

SOMA; Je Unawezaje Kuandika Kuhusu Mafanikio Iwapo Wewe Hujafanikiwa?

Hata kama unajifunza kile unachoandikia, basi jifunze kwa vitendo, washirikishe wasomaji wako kile unachojifunza na jinsi unavyofanyia kazi, pamoja na matokeo unayopata.

Hata kama unashindwa, washirikishe wasomaji wako, watajifunza zaidi kupitia kushindwa kwako na wala hawatakudharau au kuacha kukusoma.

Kwenye ulimwengu ambao kila mtu anapiga kelele, kila mtu anasema na mimi pia, kujitofautisha ni muhimu sana.

Na huwezi kujitofautisha kwa kupiga kelele zaidi ya wengine, bali unajitofautisha kwa kufanya kile ambacho wengine hawawezi kufanya, kwa kuwa wewe, kwa sababu hakuna mwingine anayeweza kuwa wewe.

Kila mtu ni hadithi inayotembea, ipe dunia hadithi yako, na wapo ambao wataona hadithi yako inaendana nao, na watakuwa wasomaji na wafuasi wako wazuri kwenye kazi zako za uandishi na ushauri.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Njia Tano(05) Za Uhakika Za Kuongeza Wasomaji Kwenye Blogu Yako Na Kuwafikia Watu Wengi Zaidi.

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia, zama tunazoishi sasa, kila mtu anapaswa kuwa na blogu. Tunaishi zama za taarifa ambapo taarifa sahihi zina thamani kubwa sana katika maisha, kazi na hata biashara.

Unapokuwa na blogu, unaweza kuitumia kukuza jina lako, kuendeleza kazi zako, kukuza biashara yako na hata kuwawezesha wengi kujua ulipo na unafanya nini. Blogu pia inaweza kuwa nafasi yako ya kutoa mchango kwa wengine hapa duniani.

Lakini watu wengi wamekuwa wanakata tamaa pale wanapoanzisha blogu halafu hawapati wasomaji wa kutosha. Wanaona kama nguvu wanazoweka zinapotea bure.

Wengine wamekuwa wanatumia njia ambazo siyo sahihi za kukuza blogu zao. Njia hizo zimekuwa na madhara makubwa kwao na blogu zao na hivyo kuzidi kuwapoteza zaidi kuliko kuwasaidia.

Katika kipindi cha leo cha MTAALAMU, nimekushirikisha njia tano za uhakika za kuweza kuwafikia wasomaji wengi kwa kutumia blog yako.

Njia hizi ni rahisi na za uhakika, ambazo ukiweza kuzitumia utaweza kuwafikia wasomaji wengi, na wakawa wasomaji wa kudumu wa blogu yako.

Kwa kifupi nikushirikishe njia mbili kati ya hizo tano;

Moja ni kuandika makala bora kabisa, makala ambazo zina majawabu kwa changamoto za watu, zinawawezesha kuchukua hatua na kuboresha maisha yao. Kwa kuwa na makala bora, watu watazisoma na watawashirikisha wengine ili nao wajifunze. Ukiangalia kipindi hichi nimeeleza kwa kina jinsi ya kuboresha makala zako.

Mbili ni kuwa na msimamo kwenye uandishi, kuwa na ratiba ya kuandika na kuweka makala kwenye blogu ambayo unaifuata. Changamoto kubwa kwa wengi ni kuandika pale wanapojisikia kuandika, hili limekuwa linawafanya wasomaji washindwe kuwafuatilia vizuri. Kwenye kipindi hichi nimekushirikisha ratiba nzuri ya uandishi ambayo itawafanya wasomaji wako waweze kukutegemea kulingana na uandishi wako.

Kujifunza njia hizi kwa kina na njia nyingine tatu za kukuza blogu yao kwa kuwafikia wasomaji wengi, angalia kipindi hichi cha leo.

Kuangalia kipindi hichi, bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu kuona moja kwa moja.

Usikubaki kuishi zama hizi bila ya kutumia vyema mtandao wa intaneti katika kujinufaisha wewe na wengine kwa maarifa na taarifa muhimu unazoweza kutoa na kupokea kupitia mtandao huu.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Usitafute Fedha Za Haraka Mtandaoni, Utapoteza Muda Wako Na Kuharibu Uaminifu Wako.

Msingi mkuu wa kutengeneza fedha ni mmoja, na unafanya kazi iwe ni unapata fedha hizo shambani, kwenye ajira, kwenye biashara na hata kwenye mtandao; fedha ni zao la thamani unayozalisha kwa wengine.

Kama kuna kitu chochote unachoambiwa kinalipa, swali la kwanza kujiuliza je ni thamani gani unazalisha kwa wengine mpaka wakulipe? Ukijiuliza swali hili moja, kamwe hutatapeliwa wala kupoteza muda wako kwa mambo yasiyo sahihi.

Kutokana na ugeni wa mitandao na njia zake za kutengeneza kipato, watu wengi wamedanganywa na kuhadaiwa. Wanaambiwa wabonyeze link fulani au watume ujumbe fulani kwa watu wengi na watalipwa fedha.

getpaid_scam

Huo ni uongo mkubwa, unakupotezea muda na kusababisha usumbufu kwa wengine.

Ukweli ni kwamba unaweza kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, lakini siyo zoezi rahisi kama wengi wanavyofikiri.

Hutakaa tu na kubonyeza link halafu ukapata fedha. Wala hutawatumia wengine link wabonyeze halafu wewe ukapata fedha.

Unahitaji kuweka kazi kubwa, kazi ya kuandaa na kutoa maarifa na taarifa ambazo zinawawezesha watu kuchukua hatua na kuboresha maisha yao. Waone thamani kubwa kupitia kile unachofanya, kisha wawe tayari kulipia huduma na bidhaa unazotoa.

SOMA; Jambo Pekee La Kiungwana Unaloweza Kufanya Kwenye Mtandao Wa Intaneti Ni Hili, Na Ukalipwa Pia.

Unahitaji kujifunza sana na kuwa tayari kuwafundisha wengine maarifa sahihi. Unahitaji kuyajua matatizo na mahitaji ya watu, kujua changamoto zao na kuweza kuwasaidia kuzitatua. Na wao kwa kuridhika na hilo, wawe tayari kukupa fedha zao, ili kupata zaidi.

Hivyo rafiki, unapoambiwa kuhusu njia mpya ya kutengeneza fedha kwenye mtandao, swali lako la kwanza liwe; ni thamani gani napaswa kutoa mpaka nilipwe?

Kama hakuna thamani unayopaswa kutoa, kama hakuna kazi unayopaswa kuweka, kimbia haraka sana, kuna watu wanataka kukutapeli.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Waandishi Hawa Watakufanya Wewe Ushindwe Vibaya Kwenye Uandishi.

Wapo watu wanaoingia kwenye uandishi lakini hawachukui muda, wanashindwa na kuacha haraka sana.

Na hili linakuwa linachangiwa na waandishi wengine.

Wanachofanya watu hawa, ni kujilinganisha na waandishi wengine. Wanajaribu kuwaiga au kuwaangalia wanafanya nini, na kuwaiga.

Sasa unapoanza kuiga waandishi wengine, unakuwa umeingia kwenye mbio ambazo huwezi kushinda kamwe.

Kwa sababu yule unayemuiga yeye ana mpango ambao anaufanyia kazi. Lakini wewe unayeiga, huna mpango, unasubiri akifanya na wewe ndiyo ufanye.

tofauti uandishi

Hivyo kama unataka kufanikiwa kwenye uandishi acha kabisa kushindana na waandishi wengi. Acha mara moja kuwaiga waandishi wengine.

Andika kile ambacho kinatoka ndani yako, andika vile unavyoona itawasaidia watu.

SOMA; Hapo Ulipo Tayari Umekamilika Kama Mwandishi, Anza Kuandika Utaendelea Kuwa Bora Zaidi.

Kuna wakati unaweza kuona kama wengine wanafanya vizuri kuliko wewe, na hivyo kutamani kuiga kile wanachofanya. Usiingie kwenye mtego huo. Chagua namna utakavyoandika na andika. Hilo ndiyo muhimu sana kwako kama mwandishi.

Kujilinganisha na waandishi wengine kutakufanya ujidharau, hasa pale wale wengine wanapokuwa wamekutangulia katika uandishi.

Kuwaiga wengine ni kupoteza kile kilichopo ndani yako.

Dunia inataka kukusikia wewe, dunia inataka kusikia sauti yako, sauti ya kipekee ambayo dunia haijawahi kusikia kabisa.

Usikubali waandishi wengine wawe kikwazo kwako kufanikiwa kwenye uandishi.

Jifunze kupitia waandishi wengine, lakini usijilinganishe nao wala kuwaiga.