Category Archives: Blog

Njia Tano(05) Za Uhakika Za Kuongeza Wasomaji Kwenye Blogu Yako Na Kuwafikia Watu Wengi Zaidi.

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia, zama tunazoishi sasa, kila mtu anapaswa kuwa na blogu. Tunaishi zama za taarifa ambapo taarifa sahihi zina thamani kubwa sana katika maisha, kazi na hata biashara.

Unapokuwa na blogu, unaweza kuitumia kukuza jina lako, kuendeleza kazi zako, kukuza biashara yako na hata kuwawezesha wengi kujua ulipo na unafanya nini. Blogu pia inaweza kuwa nafasi yako ya kutoa mchango kwa wengine hapa duniani.

Lakini watu wengi wamekuwa wanakata tamaa pale wanapoanzisha blogu halafu hawapati wasomaji wa kutosha. Wanaona kama nguvu wanazoweka zinapotea bure.

Wengine wamekuwa wanatumia njia ambazo siyo sahihi za kukuza blogu zao. Njia hizo zimekuwa na madhara makubwa kwao na blogu zao na hivyo kuzidi kuwapoteza zaidi kuliko kuwasaidia.

Katika kipindi cha leo cha MTAALAMU, nimekushirikisha njia tano za uhakika za kuweza kuwafikia wasomaji wengi kwa kutumia blog yako.

Njia hizi ni rahisi na za uhakika, ambazo ukiweza kuzitumia utaweza kuwafikia wasomaji wengi, na wakawa wasomaji wa kudumu wa blogu yako.

Kwa kifupi nikushirikishe njia mbili kati ya hizo tano;

Moja ni kuandika makala bora kabisa, makala ambazo zina majawabu kwa changamoto za watu, zinawawezesha kuchukua hatua na kuboresha maisha yao. Kwa kuwa na makala bora, watu watazisoma na watawashirikisha wengine ili nao wajifunze. Ukiangalia kipindi hichi nimeeleza kwa kina jinsi ya kuboresha makala zako.

Mbili ni kuwa na msimamo kwenye uandishi, kuwa na ratiba ya kuandika na kuweka makala kwenye blogu ambayo unaifuata. Changamoto kubwa kwa wengi ni kuandika pale wanapojisikia kuandika, hili limekuwa linawafanya wasomaji washindwe kuwafuatilia vizuri. Kwenye kipindi hichi nimekushirikisha ratiba nzuri ya uandishi ambayo itawafanya wasomaji wako waweze kukutegemea kulingana na uandishi wako.

Kujifunza njia hizi kwa kina na njia nyingine tatu za kukuza blogu yao kwa kuwafikia wasomaji wengi, angalia kipindi hichi cha leo.

Kuangalia kipindi hichi, bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu kuona moja kwa moja.

Usikubaki kuishi zama hizi bila ya kutumia vyema mtandao wa intaneti katika kujinufaisha wewe na wengine kwa maarifa na taarifa muhimu unazoweza kutoa na kupokea kupitia mtandao huu.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Mitandao Ya Kijamii Siyo Jukwaa, Tengeneza Jukwaa Lako Kwa Njia Hizi Mbili.

Kama wewe ni mwandishi, mwimbaji, mchoraji au msanii wa aina yoyote ile, unalenga kuwafikia watu wengi zaidi. Kazi yako haijakamilika kama haijafika kwa wengine. Na kadiri kazi yako inavyowafikia wengi, ndivyo unavyozidi kuwa na ushawishi mkubwa na hata kuwasaidia wengi zaidi.

Kama unaishi zama hizi, basi lazima utakuwa unatumia mitandao ya kijamii. Na hapa ndipo wengi wameweka tegemeo lao kubwa katika kusambaza kazi zako.

Msanii yeyote yule, anahitaji kitu kimoja muhimu sana. kitu hicho ni jukwaa. Jukwaa ndiyo linatumika kufikisha kazi ya msanii kwa wale ambao wamewalenga.

kutangaza mitandaoni

Mitandao ya kijamii inaweza kuonekana ni jukwaa zuri, kutokana na wingi wa watu waliopo kwenye mitandao hiyo. Lakini ukweli ni kwamba, mitandao ya kijamii siyo jukwaa zuri kwa wasanii au waandishi. Ni sehemu ya kuwaeleza watu jukwaa lako lilipo, lakini yenyewe kama yenyewe siyo jukwaa.

Hii ni kwa sababu watu kwenye mitandao ya kijamii wanakutana na taarifa nyingi sana kwa muda mfupi. Hivyo kelele ni nyingi, siyo rahisi kwao kukufikia wewe na kazi zako.

Hivyo jukwaa sahihi ni kwa msanii na mwandishi, linapaswa kuwa na kazi zake tu. Sehemu ambayo msomaji au mfuatiliaji akienda, anakutana na kazi za msanii pekee na siyo kelele nyingi.

SOMA; Itumie Blogu Yako Kama Jukwaa Lako.

Jukwaa sahihi kwa waandishi na wasanii ni kuwa na blog. Unapokuwa na blog unaweka kazi zako pekee, hivyo msomaji au shabiki anapotembelea blog yako, anakutana na kazi zako pekee.

Hii ndiyo sababu nimekuwa nawashauri sana waandishi na wasanii wengine, kuwa na blog zao ambapo wanaweka kazi zao. Hata kama kazi hizo wanaziweka kwenye mitandao ya kijamii, bado wanapaswa kuziweka kwenye blogu zao pia.

Njia ya pili ya kuwa na jukwaa ni kuwa na email list. Huu ni mfumo ambao wasomaji na washabiki wako wanapata taarifa kutoka kwako moja kwa moja kwenye email zao. Hapo unatengeneza ukaribu na wasomaji au washabiki wako ambapo unaweza kuwapa zaidi na hata wao kununua zaidi kutoka kwako.

Hivyo kama unatumia mitandao ya kijamii ni njia nzuri, lakini kumbuka hilo siyo jukwaa, hiyo ni njia ya kuwafikisha watu kwenye jukwaa. Tengeneza jukwaa, kuza jukwaa lako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Usiandike Kitabu Kama Hakuna Anayekujua, Itakukatisha Tamaa.

Watu wengi wamekuwa wakiniandikia kuomba ushauri kuhusu uandishi wa vitabu. Wapo ambao tayari wanakuwa na vitabu wakati wengine ndiyo wanafikiria kuandika kitabu kwa mara ya kwanza.

Swali langu la kwanza kwa watu hawa huwa ni nani anayekufahamu? Kwa sababu kama hakuna anayekufahamu, kitabu unamwandikia nani?

Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi mno, kuna maarifa na taarifa za kila aina. Wapo waandishi wengi wanaotoa vitabu kila siku. Kipi kitamfanya mtu ajue kitabu chako na kukinunua?

abc

Unahitaji kuwa na watu wanaokujua tayari, ambao watakuwa wateja wa kwanza wa vitabu vyako. Na ninaposema kujua simaanishi kukujua wewe kwa jina na unapoishi, bali wanaokujua kupitia kazi zako za uandishi.

Mtu anapokujua wewe, kwa kujua kazi zako za uandishi, ambazo kwa kiasi fulani zinakuwa zimemsaidia, inakuwa rahisi kwake kununua kitabu chako. Hata unapotoa kitabu na kumwambia hapa nina kitabu kinaweza kukufaa, atachukua hatua mara moja.

Tofauti na mtu ambaye hajawahi kukusikia kabisa, anaweza kukutana na kitabu chako, lakini asiwe na msukumo wa kukinunua.

Swali muhimu ni je watu wanakujuaje?
Na hili ni swali muhimu na rahisi sana kujibu kwa zama hizi tunazoishi. Watu wanakujua kupitia intaneti na mitandao ya kijamii.

Kwa intaneti unahitaji kuwa na blog ambayo inaandika mambo yanayoendana na kile kitabu ulichoandika au unachopanga kuandika. Kupitia blog yako utatengeneza wasomaji ambao watakuwa wanakutegemea na kusikiliza kile unachosema. Hawa wanakuwa rahisi sana kununua kutoka kwako.

SOMA; Vitu Viwili Unavyohitaji Ili Uweze Kutengeneza Fedha Kupitia FACEBOOK.

Kupitia mitandao ya kijamii unahitaji kuwa na kurasa ambazo unazitumia kuwaelimisha watu kwa kile ambacho unaandika au umeandikia kitabu. Kupitia kurasa hizi watu wanakufuatilia na kujifunza, unapokuwa na kitabu na kuwaambia hichi hapa ni kitabu kinachoweza kukusaidia, watakuwa tayari kununua kutoka kwako.

Haya mawili ni muhimu sana kwako katika uandishi na uuzaji wa vitabu kwa zama tunazoishi sasa. Hata kama vitabu vyako unapeleka kwenye maduka ya vitabu, kukaa pale haimaanishi vitanunuliwa. Lakini unapowaambia wanaokufahamu kupitia kazi zako kwamba kitabu kipo duka fulani, wataenda pale na kununua.

Ni muhimu sana uwe na wasomaji kabla hata hujaandika kitabu, hili litakusaidia kuwafikia watu wengi kupitia kitabu ulichoandika au unachopanga kuandika.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kama Wewe Una Taaluma Au Uzoefu Wowote Ambao Watu Wanauhitaji, Unafanya Kosa Kubwa Sana Kama Huna Blog.

Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo taarifa ndiyo sarafu ya zama hizi. Watu wanathamini taarifa kuliko kitu kingine chochote. Kwa sababu taarifa sahihi zinawawezesha watu kufanya maamuzi sahihi na maamuzi sahihi yanawapelekea watu kupata mafanikio.

Katika zama hizi, mtu anapotaka kujua jambo lolote, kwanza anaingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake. Kupitia mtandao anakutana na wale wanaotoa taarifa kisha kutaka kujifunza zaidi kutoka kwao. Na pale unapobidi, wanakuwa tayari kugharamia ili kupata taarifa sahihi zinazowawezesha wao kufanya maamuzi sahihi.

Hivyo basi, kama wewe una taaluma au uzoefu wowote, ambao unaweza kuwasaidia watu kufanya maamuzi, iwapo huna njia ya kuweka taaluma na uzoefu wako kwenye mtandao wa intaneti, unafanya makosa makubwa. Hii ni kwa sababu unawakosa wale ambao wana shida na uhitaji wa taaluma au uzoefu ulionao wewe.

Chochote kile ambacho unajua, kinaweza kumsaidia mtu mwingine. Unaweza kuona unachojua ni cha kawaida sana, lakini nataka kukuambia kuna mtu amekwama mahali kwa sababu hajui unachojua wewe. Anaingia kwenye mtandao na kutafuta hatua zipi achukue, na huenda hajakutana na ushauri unaoweza kumsaidia.

Unahitaji kuwa na njia ya kuwafikia watu kwenye mtandao wa intaneti. Pale mtu anapoingia kwenye mtandao wa google na kutafuta kitu kinachoendana na unachojua wewe, basi waletwe kwako moja kwa moja.

SOMA;Njia Tano Za Kuanza Kukuza Email List Yako Kupitia Blog Na Mitandao Ya Kijamii.

Zipo njia nyingi za kufanya hivyo, rahisi kabisa na inayopendwa na wengi ni MITANDAO YA KIJAMII. Hii wengi huitumia kwa kuweka taarifa fupi fupi na hata matangazo ya kile ambacho wanafanya.

Njia nzuri kabisa ambayo nimekuwa nawashauri watu waitumie ni kuwa na blog. Hii inakuwa kama nyumba yako kwenye mtandao wa intaneti. Ni kona ambayo unakuwa umejitengenezea, ambapo mtu akitaka kitu fulani kutoka kwako, basi anajua akija pale atakipata.

Unapokuwa na blog kwa sehemu kubwa unakuwa unaimiliki mwenyewe na hivyo kuweza kuitumia kutunza kazi zako, kujenga wafuasi wako na kuuza huduma au bidhaa ambazo unazo.

Blog ni njia bora kabisa ya watu kukufikia, hasa pale wanapotafuta kitu kinachoendana na kazi zako kupitia mitandao kama google.

Ndiyo maana napenda kukushauri, kama utaalamu wako au uzoefu wako ni wa kufanya kazi na watu moja kwa moja, basi anzisha blog yako.

Na wala huhitaji kuwa na gharama kubwa ili kuanzisha blog, huhitaji hata kuwa na utaalamu mkubwa. Unachohitaji ni kuwa tayari kuwapa watu maarifa na taarifa sahihi, ili waweze kufanya maamuzi sahihi.

Kama mimi ninavyokupa taarifa sahihi hapa kuhusu kuwafikia watu kupitia mtandao wa intaneti kwa kuwa na blog. Na kama mpaka sasa huna blog, naweza kukusaidia ukawa na blog bora kabisa ya kuanzia kufikisha taarifa zako kwa watu ambao wana uhitaji nazo. Tuwasiliane kwa wasap 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Jinsi Unavyoweza Kupata Wasomaji Wa Kudumu Kwenye Blogu Yako.

Tofauti kati ya blogu za kuhabarisha na blogu za kufundisha au kutoa maarifa, ni hatua mtu anayochukua baada ya kusoma kile kilichoandikwa.

Nikupe mifano miwili kabla hatujaendelea;

Mfano wa kwanza kwenye blogu ya habari; Huyu ni mtu aliyefanya mauaji ya kutisha.

Mfano wa pili kwenye blogu ya mafunzo; hatua tatu za kuboresha wazo lako la biashara.

Katika makala hizo mbili, kwanza itakayofunguliwa sana ni ile ya mauaji ya kutisha. Kwa sababu gani? Kwa sababu inashika eneo muhimu la watu ambalo ni hofu. Lakini sasa twende, kama wameifungua watu 1000, unafikiri wanachofanya ni nini baada ya kusoma habari hiyo? Hakuna kikubwa, watakuwa na hofu na kuendelea na maisha yao. Hawatajali hata ni nani ameandika habari hiyo. Wao wameshajua mwenye kufanya mauaji, na wanaendelea na maisha.

Kwenye habari ya pili, ya hatua tatu za kuboresha wazo lako la biashara, tuseme imefunguliwa na watu 50. Kati ya hao 50, huenda 10 wanakazana kupata wazo bora la biashara. Hawa moja kwa moja watachukua hatua, watafanyia kazi zile hatua tatu, watataka kumjua mwandishi zaidi na hivyo kusoma makala zake nyingine, na ataendelea kumfuatilia kuanzia hapo. Anaweza asimtafute wakati huo, lakini kadiri siku zinavyokwenda ataendelea kujifunza zaidi. Na iwapo mwandishi ataendelea kutoa makala zinazomsaidia, anakuwa mshabiki wake na kuwa tayari kununua chochote kutoaka kwake.

Kama ulivyoona hapo, kinachomfanya mtu kuwa msomaji wa kudumu wa blogu yako, siyo kuvutiwa na kile unachoandika, bali kitu gani anaondoka nacho cha kuweza kufanyia kazi. Hivyo ni muhimu sana unapoandika makala zako, hakikisha unampa mtu kitu cha kufanyia kazi, hakikisha kuna hatua ya yeye kuchukua ili kuweza kuboresha maisha yake zaidi.

Usiumizwe na namba, hasa mwanzoni. Maana watu wengi wamekuwa wanaangalia idadi ya wasomaji, wanavyoona ndogo wanakata tamaa na kuacha. Hata kama unao wasomaji 50, hao ni wazuri sana kuanza nao. Waandikie hao, wape hatua za kuchukua na mtaendelea kuwa pamoja.

Hivi ndivyo unavyojenga wasomaji wanaokufuatilia kupitia kazi zako. Siyo kwa kutaka kuwavutia wengi, ambao hawana wanachofanyia kazi. Bali kwa kuwavutia wachache ambao watachukua hatua na kuendelea kuwa pamoja.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Idadi Sahihi Ya Wasomaji Unaohitaji Ili Kutengeneza Kipato Cha Uhakika Kwenye Intaneti.

Intaneti imeleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yetu ya kila siku. Watu walifikiri ni kitu cha muda na cha kupita, lakini kadiri siku zinavyokwenda, watu wanakubali kwamba intaneti ipo na itaendelea kuwepo.

Mitandao ya kijamii kama facebook, instagram na wasap imezidi kuchochea matumizi ya intaneti kwa kila mtu. Mitandao hii imekuwa sehemu kubwa ya mawasiliano na kupashana habari kwa watu walio wengi.

Kizuri zaidi ni kwamba, intaneti na mitandao ya kijamii, imekuwa fursa ya watu kuweza kujiajiri kupitia mitandao hii na kutengeneza kipato cha kuendesha maisha yao. Watu wanaweza kujiajiri kwa kufanya biashara moja kwa moja kwenye intaneti au kutumia intaneti kukuza zaidi biashara zao ambazo wamekuwa wanafanya.

Pamoja na fursa hii kubwa ya kutengeneza kipato kwenye intaneti, bado watu wengi hawana uelewa wa kutosha, na hivyo wamekuwa wanafanya makosa ambayo yanawagharimu.

Moja ya makosa hayo ni kutojua idadi sahihi ya wasomaji ambayo mtu unapaswa kuwa nayo kwenye intaneti ili kuweza kutengeneza kipato cha uhakika. Kwa kutokujua idadi hii sahihi, watu wamekuwa wakipoteza nguvu nyingi kutaka kumfikia kila mtu, na kujikuta hawapati watu wengi wa kuweza kufanya nao biashara.

Ipo sheria inaitwa MASHABIKI WA UKWELI 1,000.

Sheria hii inasema kwamba, ili uweze kutengeneza kipato cha kutosha kama msanii, yaani uwe mwandishi, mwimbaji, mchoraji na kadhalika, unahitaji kuwa na mashabiki wa ukweli 1,000. Ndiyo ni mashabiki wa ukweli elfu moja tu unaohitaji ili uweze kutengeneza kipato cha kutosha kuendesha maisha yako kwa kufanya kile unachotaka kufanya.

Na hapa ni muhimu kwanza tuwajue mashabiki wa ukweli ni wapi?

Hawa ni wale watu wanaoikubali kweli kazi yako. Wapo tayari kununua chochote unachotoa. Watu hawa wanasubiri kwa hamu chochote unachotoa na kukinunua haraka. Siyo watu wanaouliza bei au kutaka kupunguziwa au kupata bure. Ni watu ambao wapo tayari hata kukuchangia ili kazi zako ziweze kwenda. Watanunua hata tisheti au kikombe chenye jina lako. Watasafiri umbali mrefu kuja kwenye onesho lako au mafunzo yako. Hawa ndiyo mashabiki wa ukweli, ambao unawahitaji ili kuweza kuendesha vizuri kile unachofanya.

Kitu cha pili kwa nini elfu moja?

Kama una mashabiki wa ukweli, ambao wapo tayari kununua chochote unachotoa. Unaweza kuwapa wastani wa kukupa kiasi cha shilingi elfu kumi kila mwezi. Hivyo tsh 10,000/= kwa watu 1,000 unapata tsh 10,000,000/= hiyo ni shilingi milioni kumi kila mwezi. Hicho ni kipato kinachokuwezesha kuwa na maisha inayoyataka. Na kama hutaki kuanzia mbali kiasi hicho, basi unaweza kuweka wastani wa shilingi elfu 5 kila mwezi, na ukapata milioni tano kila mwezi. Au kama unaanzia chini kabisa, basi fanya shilingi elfu moja kila mwezi, na utapata milioni moja kwa mwezi.

Unaona sasa tunachokwenda kutengeneza hapa?

Huhitaji kila mtu ili kuweza kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti. Huhitaji kukazana kumfikia kila mtu, bali unachohitaji kufanya ni kutengeneza mashabiki elfu moja tu, ambao wanakukubali sana  wewe, wanaenda sambamba na wewe kwenye kila unachofanya. Utakuwa na uhuru mkubwa wa kufanya kile unachofanya.

Tukirudi kwenye mpango wetu ambao ni kutengeneza kipato kupitia intaneti na mitandao ya kijamii, hapa sasa unahitaji kuwa na blog ambayo utaitumia kuwapata mashabiki wako 1000. Unahitaji kuwa na mitandao ya kijamii ambayo utaitumia kuwafikia mashabiki wako hao elfu moja. Na muhimu zaidi, unahitaji kuwa na mfumo wa email, ambao utautumia kuwa karibu na mashabiki wako hao elfu moja.

Vitu hivyo vitatu; 1. BLOG 2. MITANDAO YA KIJAMII 3. EMAIL LIST, ni lazima uwe navyo kama unataka kutengeneza kipato kupitia intaneti.

Kama huwezi 1,000 basi anza na 100 au anza na 10.

Upo usemi wa Martin Luther King kwamba kama huwezi kuruka basi kimbia, kama huwezi kukimbia basi tembea na kama huwezi kutembea basi tambaa, fanya chochote ila tu usonge mbele.

Najua elfu moja inaweza kuwa namba kubwa, hasa kama ndiyo unaanza. Na mimi nakuambia usiwe na wasiwasi, kama elfu moja ni kubwa, basi anza na 100 na kama 100 ni kubwa, basi anza na kumi. Anza kwa kutafuta mashabiki kumi wa ukweli, ambao watanunua chochote unachowauzia, na hata wapo tayari kukuchangia huduma yako iendelee, na ukishawapata hao kumi, endelea kuwakuza zaidi.

Je una mashabiki wangapi wa ukweli kwenye kazi zako?

Kama bado hujaweza kutengeneza mashabiki, au huna mashabiki wa kutosha, tuwasiliane kwa wasap namba 0717 396 253. Karibu sana.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kama Unataka Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao, Jukumu Lako Kubwa Ni Hili.

Swali siyo kama inawezekana au la kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, hilo linafahamika kwamba mtandao wa intaneti ni njia moja na ambayo ipo wazi kwa kila mtu kuweza kutengeneza kipato.

Swali ni unawezaje kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti kwa kuanzia pale ulipo sasa, kwa utaalamu, ujuzi, uzoefu au chochote ambacho wewe binafsi unapenda kufanya.

Na hapa ndipo mimi nimekuwa nakupa maarifa mbalimbali ya kufanya hivyo kuputia mtandao wa www.mtaalamu.net/pesablog Kusudi langu ni wewe uweze kutumia mtandao wa intaneti kwa faida, uache kushabikia tu wengine na wewe unufaike. Uache kushangilia wamiliki wa mitandao hii kuwa mabilionea wakiwa vijana wadogo, na wewe uanze kunufaika na sehemu ya mabilioni hayo ya mtandao wa intaneti.

Ambacho nimekuwa nakuambia mara zote, huhitaji kitu kikubwa sana ambacho huna sasa ili kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti. Unahitaji kuanzia hapo ulipo sasa, ukiwa unafanya kile ambacho umekuwa unafanya, ila sasa ukiwa na mtazamo tofauti kidogo.

Iwapo unataka kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, basi jukumu lako kubwa ni hili; KUFANYA MAISHA YA WENGINE KUWA BORA ZAIDI. Tunaweza kuishia hapo na ukaanze kuweka kazi, kwa sababu hakuna la ziada zaidi ya hilo. Fanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi. Mara zote kuwa wa msaada kwa wengine, kupitia kile ambacho unafanya sasa.

Sasa hizi maisha ya watu yamehamia kwenye mtandao wa intaneti. Watu wengi wanatumia mtandao kwa muda mwingi zaidi kwenye maisha yao. Sasa hivi mtu kukaa nusu saa hajashika simu yake na kuingia kwenye mtandao, ni vita kubwa sana ambayo wachache ndiyo wanaweza kuishinda.

Kwa maisha kuhamia kwenye mtandao, hii ina maana hata mahitaji ya watu wanayatafuta kwenye mtandao, chochote wanachotaka kujifunza wanaanzia kwenye mtandao. Na hapo ndipo wewe una nafasi ya kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kwa kuwapa maarifa na taarifa zinazowawezesha kufanya maamuzi bora kwa maisha yao.

Unahitaji kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuwa shirikisha watu maarifa yanayoendana na kile ambacho unafanya au unafuatilia, yatakayowawezesha kufanya maamuzi bora zaidi. Ukishafanya hivyo, unahitaji kujua namna ya kuwafikia wale wanaojali kile unachofanya.

Writing Message On Smartphone

Ili kufanya hili, unahitaji kuiweka vizuri mitandao yako ya kijamii unayotumia, ili watu wanapotembelea wajue pale wanapata kitu fulani. Na muhimu zaidi unahitaji kuwa na BLOG ambayo hii ndiyo itakuwa nyumbani kwako kwenye mtandao wa intaneti. Watu wanapokuwa wanatafuta kitu chochote kinachohusiana na yale unayowashirikisha watu wewe, ataletwa moja kwa moja kwenye blog yako. Kwenye blog atajifunza zaidi na atapenda kupata mengi kutoka kwako, ikiwa ni pamoja na kupata huduma muhimu unazotoa.

Hivyo rafiki yangu, chochote unachofanya kwenye mitandao ya kijamii na mtandao wa intaneti kwa ujumla, hakikisha unakuwa wa msaada kwa wengine. Unafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi na wao watakuwa tayari kukufuatilia na pia kununua kutoka kwako chochote unachouza.

Usisahau kuweka vizuri mitandao yako ya kijamii na pia kuwa na blog itakayokuwa nyumba yako. Kama unahitaji ushauri wa kina kwenye hili, pamoja na kupata blog, tuwasiliane kwa simu 0717396253, wasap itakuwa njia bora zaidi.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.