Category Archives: UJASIRIAMALI MAARIFA

Kuandika Ni Mapenzi Kwanza Kabla Ya Kufikiria Kulipwa.

Watu wengi wamekuwa wakiuliza je unaweza kujiajiri kwa kuwa mwandishi na ukaweza kuendesha maisha yako vizuri?

Jibu ni ndiyo, lakini kabla ya kufikiria kulipwa unahitaji kuweka mapenzi yako kwanza.

Ndiyo maana nimekuwa nasema kuandika ni mapenzi kwanza kabla ya kufikiria kulipwa.

Hii ni kwa sababu, hakuna mtu atakayekimbilia kukulipa kwa uandishi wako kabla hajakujua wewe mwenyewe vizuri.

Hata kama utaandika kitabu kizuri, watu wanahitaji kuwa wanakujua kwanza wewe kabla hawajawa tayari kununua kitabu chako.

Hivyo lazima uanze kuandika kama mapenzi, uandike kwa sababu unapenda, uandike kwa sababu una kitu cha kuwasaidia watu, una maarifa ya kuwashirikisha wengine.

Uandike kwa sababu una uzoefu ambao wengine wakiutumia maisha yao yatakuwa bora.

Au pia uandike kwa sababu unajifunza na ungependa wengine wajifunze kama wewe pia.

Hayo yote unayafanya bure, ukiweka thamani kubwa kwenye kazi zako, bila ya kutegemea kulipwa hapo hapo moja kwa moja.

andika kwa mapenzi

Lakini wakati unafanya hayo, unakuwa unatengeneza imani yako kwa watu, unakuwa unatengeneza wafuasi ambao wanategemea kazi zako. Ambao watakuwa tayari kununua kwako, kwa sababu wameshapata vingi kutoka kwako.

Hivi ndivyo unavyopaswa kuanza kama unataka kufanya uandishi kuwa kazi yako ya kukuingizia kipato. Unatanguliza mapenzi mbele, na unatengeneza mazingira ya watu kuwa tayari kununua kutoka kwako.

SOMA; Tengeneza Hamasa Ya Kuandika, Na Siyo Kusubiri Mpaka Upate Hamasa.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Fanya Uandishi Kama Sehemu Ya Maisha Yako, Na Hutasumbuka Kuandika.

Kila siku unapumua, hujawahi kusema na leo tena inabidi nipumue.

Kadhalika kwenye kula, kila siku unakula, hata kama utabanwa na shughuli zako kiasi gani, lazima utatenga muda wa kula, hata kama ni mara moja kwa siku. Huanzi kulalamika sasa inabidi tena nile.

Sasa inapokuja kwenye uandishi, kwa nini ujiulize na kuanza kutafuta sababu za kuacha kuandika?

Unaonaje uandishi ungekuwa sehemu ya maisha yako? Labda ukiamka tu cha kwanza ni kuandika. Au baada ya kufanya kitu fulani kinachofuata ni kuandika.

Je huoni kwamba uandishi utakuwa rahisi kwako?

Writing4

Lengo langu leo ni kukuambia kwamba, kama umechagua kuwa mwandishi, au kufanya ujasiriamali maarifa, basi ni muhimu kufanya uandishi kuwa sehemu ya maisha yako.

Uandishi usiwe kitu ambacho unafikiria ufanye au usifanye, bali iwe ni kitu ambacho lazima ufanye, kila siku.

SOMA; Tengeneza Hamasa Ya Kuandika, Na Siyo Kusubiri Mpaka Upate Hamasa.

Lakini wakati mwingine watu wanakwama kwa sababu wanaona hawana wazo bora la kuandika, au hawataandika kitu kizuri.

Na mimi ninachokuambia ni andika, siamini kama unaweza kufika mahali akili yako ikawa tupu kabisa, huna wazo lolote, huna chochote ulichojifunza, huna chochote cha kumshauri mtu. Ni ngumu sana hiyo.

Kila siku andika, siyo lazima uandike kitu kikubwa, siyo lazima uandike kitu kilichokamilika. Lakini pia, siyo lazima uandike kitu na kuwaonesha watu. Siku nyingine unaweza kuandika na ukabaki na ulichoandika. Au ukaboresha zaidi na kupata kilicho bora.

Kwa vyovyote vile, andika kila siku, hivyo ndivyo unavyokuwa mwandishi bora.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Jinsi Ya Kuendesha Blog Kwa Mafanikio Hata Kama Huna Muda Kabisa.

Nimekuwa nashauri jambo moja mara zote, kwamba kwa ulimwengu tunaoishi sasa, ni muhimu sana kila mtu kuwa na blog. Yaani kila mtu anapaswa kuwa na blog, hata kama haitumii kibiashara.

Yapo mambo mengi utapitia na kujifunza kwenye maisha, ambayo unaweza kuwashirikisha wengine nao pia wakanufaika. Ukiwa na blog itakuwa njia nzuri kabisa ya kufanya hivyo.

Pia kama una utaalamu, uzoefu, elimu, kazi au biashara yoyote, blog itakuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi na kwa gharama nafuu kabisa.

Lakini changamoto ya wengi katika kuendesha blog imekuwa ni muda. Wengi wamekuwa wanasema wanapenda sana kuwa na blog, ila hawana muda wa kuweza kuiendesha.

Kwenye somo la leo, nakwenda kukuonesha ni jinsi gani unaweza kuendesha blog yako, hata kama huna muda kabisa. ndiyo, namaanisha hata kama muda wako wote unafanya kazi, bado unaweza kupata muda wa kuendesha blog.

Teknolojia imekua sana kwa sasa, unaweza kufanya kila kitu kwa muda mfupi, unaweza kuonekana unapost kwenye blog na mitandao ya kijamii kumbe muda huo haupo hewani kabisa.

Yaani hata kama unasafiri kwenda vijijini ambapo huna mtandao wala umeme, unaweza kupanga na makala zinawa zinaenda hewani muda wote, huku wewe ukiwa haupo kwenye mtandao kabisa.

Kwenye kipindi hichi nimekushirikisha vitu vitatu muhimu unavyohitaji kutumia kuendesha blog na mitandao ya kijamii pale unapokuwa huna muda kabisa. pia nimekushirikisha mbinu ya kuonekana upo kwenye mitandao ya kijamii siku nzima hata kama haupo kabisa.

Angalia kipindi hichi ujifunze na uweze kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kwa faida.

Kuangalia kipindi hichi, bonyeza maandishi haya, au kama kifaa chako kinaruhusu, angalia moja kwa moja hapo chini.

Kwa ushauri na elimu zaidi kuhusu blog na matumizi sahihi ya mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii, tuwasiliane kwa wasap 0717396253.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Fanya Uandishi Kuwa Kazi Yako Kuu, Na Siyo Kitu Cha Pembeni.

Watu wengi wanaoanza kuandika, hasa uandishi wa kujitegemea kama uandishi wa vitabu na makala, huwa wanafanya uandishi kuwa kitu cha pembeni au cha ziada kufanya. Wanakuwa na kazi au shughuli nyingine wanazofanya, na uandishi unakuwa kitu cha ziada.

Siyo jambo baya, hasa unapoanza, kwa sababu unahitaji maisha yaendelee, uwe na kipato cha uhakika na kuendelea kujijenga kiuandishi.

Lakini hili lina changamoto kubwa moja, ukifanya uandishi kama kitu cha ziada, au kitu cha pembeni, unajizuia kukua kiuandishi. Hii ni kwa sababu unakuwa huupi uandishi uzito wa kutosha, unaufanya pale unapopata muda.

Kwa kuwa muda una ukomo, na kila siku yapo mambo mengi ya kufanya kuliko muda tulionao, uandishi unakosa muda. Unajikuta ukisema utaandika kesho au utafanya kesho. Hili ndiyo linasababisha wengi wanashindwa kukuza uandishi wao na hatimaye kuwa kazi ya kudumu kwao.

andika kila siku

Ninachotaka kukuambia hapa ni ufanye uandishi kuwa kazi yako kuu. Hapa simaanishi uache kazi nyingine zote, bali utoe kipaumbele cha kwanza kwenye uandishi. Uhakikishe unafanya uandishi kwanza kabla ya shughuli nyingine zozote.

Hapa huhitaji kufanya mabadiliko yoyote makubwa, bali unachohitaji kufanya ni kutenga muda wako wa uandishi na kuutumia kila siku kwa lengo hilo la uandishi. Kwa mfano unaweza kutenga saa moja kwa siku kwa ajili ya kuandika. Kisha ukapanga kuamka asubuhi na mapema na kuandika, kabla hujafanya kitu kingine chochote.

Ukishaweka mipango hiyo, kila siku asubuhi unaamka mapema na kuandika. Iwe unaandika makala na kuweka kwenye blog, au unaandika kipengele au sura ya kitabu, kwa kufanya hivi kila siku, unapiga hatua kubwa kiuandishi.

SOMA; Tengeneza Hamasa Ya Kuandika, Na Siyo Kusubiri Mpaka Upate Hamasa.

Muhimu ni kutenga muda na kujijengea nidhamu ya kufuata muda ule ambao umeutenga kufanya kile ulichopanga kufanya. Kwa njia hii uandishi unakuwa kazi yako kuu, bila ya kuathiri kazi zako nyigine.

Uandishi ni njia nzuri ya kuja kununua uhuru wako wa baadaye, njia unayoweza kuitumia sasa wakati unaendelea na shughuli zako nyingine na isiathiri chochote.

Tumia fursa hii nzuri, hasa kwa zama hizi za taarifa, ili kuweza kujitengenezea uhuru mkubwa baadaye. Kama umekuwa unapanga kuandika kitabu, anza sasa na andika kila siku. Kama huna blog, fungua sasa na anza kuandika kila siku. Kama huna blog na unahitaji, tuwasiliane 0717396253, karibu sana.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kiuandishi Kabla Ya Kuandika Kitabu.

Waandishi wengi ambao wamekuwa wanaandika vitabu vyao vya kwanza, yapo makosa mengi ambayo wamekuwa wanayafanya, ambayo yanapelekea vitabu wanavyotoa visiwe bora sana.

Japokuwa ni kawaida kukosea kwenye kitu cha kwanza, lakini vipo vitu ambavyo unapaswa kuepuka kuvikosea kwa sababu ni vya kawaida sana katika uandishi.

Uandishi wa vitabu una mambo mengi, kuanzia kuja na wazo, uandishi wenyewe, upangaji wa bei, usambazaji na uuzaji. Leo nataka nikushirikishe machache kwenye hatua ya uandishi, ili uweze kuandika kitabu kizuri, kinachosomekana na chenye mwonekano mzuri.

q

Kwanza kabisa ni ukubwa au urefu wa kitabu.

Wapo watu ambao wanaandika maneno elfu tano au elfu kumi na kusema wameandika kitabu. Hicho siyo kitabu, bali ni makala ndefu au ripoti kama unaweza kuiita hivyo.

Kitabu hasa kinapaswa kuwa na maneno elfu sitini na kijitabu kinakuwa na maneno elfu thelathini.

Hivyo unapopanga kuandika kitabu, hakikisha unaandika siyo chini ya maneno elfu 30.

Elewa hapo nimetumia idadi ya maneno na siyo idadi ya kurasa. Kwa sababu wengi huangalia kurasa ngapi za kitabu, sasa kurasa zinadanganya kwa sababu ukiweka maandishi makubwa, kurasa zinaweza kuonekana nyingi. Tumia idadi ya maneno, haidanganyi.

Jambo la pili ni uchaguzi wa aina ya maneno (fonts) unayopaswa kutumia. Zipo aina nyingi za maneno unaweza kutumia kwenye uandishi, lakini kwa mwonekano mzuri na kwa kila mtu kwa kila kifaa anachotumia, TIMES NEW ROMAN au CALIBRI (BODY) Ni nzuri katika uandishi wa vitabu.

SOMA; Makundi Matatu Ya Wasomaji Wa Kazi Zako Ambayo Unapaswa Kuyajua Ili Kufanikiwa Kwenye Uandishi.

Jambo la tatu ni ukubwa wa maneno unayotumia. Na huu huwa ni kwa namba. Wapo ambao wamekuwa wanatumia maneno makubwa ili kuonekana vizuri, lakini wakati mwingine hayo huharibu mwonekano wa kitabu. Hivyo namba nzuri kutumia ni namba 12 kwa aya za kawaida, 16 kwa kichwa cha habari na namba 14 kwa kichwa kidogo cha habari au kipengele.

Jambo la nne ni idadi ya sura za kitabu. Hata kama kitabu ni kirefu kiasi gani, jitahidi kisiwe na sura nyingi, kuwa na kitabu chenye sura 30 inaweza kumfanya msomaji aone ni kirefu sana na hatamaliza. Badala yake jitahidi kuweka pamoja vile vinavyoendana. Kuwa na sura zisizozidi kumi na kwenye kila sura kuwa na vipengele viwili mpaka vitatu. Kwa mpango huu unampa msomaji mtiririko mzuri.

Zingatia mambo hayo katika hatua ya uandishi wa kitabu na utaweza kuandika kitabu kizuri, kinachovutia kusoma na hata kueleweka na wasomaji wako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Dunia Ya Sasa, Kila Kitu Kinaanza Na Maudhui, Kisha Kuwafikia Wengi Zaidi.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, kama unataka kuwafikia watu wengi, unahitaji kutengeneza maudhui na kuyasambaza kwa njia ambayo yatawafikia wale ambao unawalenga.

Iwe ni kiongozi, mfanyabiashara au msanii, kitakachokufikisha kwa watu ni aina ya maudhui ambayo unayatengeneza na kuyatoa.

Dunia ya sasa, ambapo mitandao ya kujamii ni sehemu kubwa ya maisha ya watu wengi, kitakachowafanya watu waanze kukuangalia na hata wakufikirie ni aina ya maudhui unayoyatoa na kuwashirikisha.

toa maudhui

Unapotoa maudhui yoyote, wapo watu ambao watakubaliana nayo, watu hao wana watu wanaowajua ambao watakubaliana nayo hivyo wanawasambazia. Inakwenda hivyo mpaka unawafikia wengi zaidi.

Kabla hata hujafikiria kuwaambiwa watu wanunue unachotaka kuwauzia, wape maudhui kwanza.

Kabla hujawaomba watu wafanye kile unachotaka wafanye, hata kama ni kukupigia kura, wape maudhui.

Maudhui haya yanaweza kuwa ya mafunzo fulani, maarifa na hata hadithi ambayo ina funzo kubwa kwa mtu.

Maudhui unaweza kuyatoa kwa njia ya maandishi, kama makala, ripoti au maoni. Unaweza kuyatoa kwa njia ya sauti kama hotuba, maongezi, mahojiano au kuimba. Na pia unaweza kuyatoa kwa njia ya picha na video.

Hii Ndiyo Njia Bora Kabisa Ya Kutangaza Biashara Yako Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Chochote unachoweza kufanya, ambacho kitafikisha ujumbe ulionao kwa wale ambao wanauhitaji, kitumie. Lengo lako kuu ni watu wajue uwepo wako, wajue kwa namna gani unaweza kuwasaidia na wahitaji zaidi kile unachofanya.

Ni baada ya kutoa maudhui, ndipo sasa unaweza kuwauliza watu wakusaidie au wafanye kile ambacho unataka wafanye.

Lakini cha kwanza maudhui, hata kama biashara unayofanya ni ya kawaida. Maudhui ndiyo yanawafanya watu wajue uwepo wako, waone kama unawafaa au la.

Weka jitihada kwenye kutengeneza maudhui mazuri, ambayo yataendana na aina ya watu unaowalenga.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Kuna Watu Kamwe Hawatanunua Unachouza, Elewa Hilo Na Songa Mbele.

Ujasiriamali wa taarifa ni moja ya aina ngumu sana za ujasiriamali kuliko wengi wanavyofikiri.

Hii ni kwa sababu, kabla hujamuuzia mtu maarifa na taarifa ulizonazo, unahitaji kwanza kumpa maarifa na taarifa nyingi za bure. Hata kama wewe ni mwandishi wa vitabu, na unategemea kuchapa na kuweka kwenye maduka ya vitabu, kama unataka wanunuzi wengi, basi unahitaji njia ya kuwafikia wengi zaidi kwa kutoa maarifa ya bure.

Sasa hapo ndipo mtego ulipo, kwa sababu wengi wanapotoa maarifa hayo ya bure, na watu wakayapokea vizuri na kuyafurahia, hufikiri kwamba watu wote hao lazima watanunua kile ambacho mtu anauza. Hii siyo kweli.

Wapo watu watafurahia maarifa ya bure unayotoa, lakini kamwe hawatanunua chochote unachouza. Tena wengine watakuwa wa kwanza kulalamika pale wanapokosa maarifa unayotoa bure, lakini ukiwaambia wanunue, hawatanunua.

buy books

Lazima uelewe hili ili uweze kusonga mbele. Lazima ujue wapo watu hawatanunua, hata kama ungeamua kuwapa unachouza kwa bei ndogo sawa na bure kabisa.

Unakuta wengi ndivyo tu walivyo, hawana mpango wowote wa kununua. Wengine wanaona hawana haja ya kulipia kwa kuwa tayari wanapata bure.

SOMA; Unachojua Wewe, Wapo Wengi Hawakijui, Washirikishe Utengeneze Kipato.

Ni muhimu sana ukawajua wale wanaonunua ni wapi, na hao kuwapatia thamani kubwa sana kulingana na gharama wanazolipa.

Lakini pia usiwatelekeze wale ambao hawanunui, ni sehemu ya wafuasi na wasomaji wako, endelea kuwapa maarifa na taarifa zaidi.