Category Archives: Ujasiriamali Wa Taarifa

Saikolojia Ya Mitandao Ya Kijamii Inayowazuia Wengi Kuwa Na Blogu.

Jambo moja ambalo nimekuwa nasisitiza sana kwa mtu yeyote ambaye anafanya ujasiriamali wa taarifa ni kuwa na blogu. Lakini bado wengi wamekuwa hawaelewi hilo, kwa sababu wanashindwa kuivuka saikolojia ya mitandao ya kijamii.

Huwa nafananisha maisha yetu kwenye mtandao na maisha yetu ya uhalisia. Huwa nasema mitandao ya kijamii ni sawa na kijiweni ambapo watu wanakutana kupiga hadithi za hapa na pale. Na blogu yako ndiyo nyumbani kwako, ambapo watu wana uhakika wa kukupata pale.

Unapokuwa na shida na mtu, sehemu ya uhakika ya kumpata ni nyumbani kwake na siyo kwenye kijiwe ambacho huwa unamwona mara kwa mara.

like za facebook

Kadhalika kwenye mtandao, uwepo wako kwenye mitandao ya kijamii ni sawa na kuwepo kijiweni. Kwa sababu siyo muda wote watu wanakuona pale, wanakuoa kwa muda mchache wakati wao wanapita na mambo yao.

Unapokuwa na blogu, hapo sasa ndiyo nyumbani kwako. Muda wowote mtu anapokuja kwenye blogu yako, anakutana na kazi zako. Mtu anapokuwa kwenye blogu yako, anakuwa na wewe moja kwa moja na hana usumbufu mwingine kama anaokutana nao kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa watu wengi wamekuwa wakipenda kutumia mitandao ya kijamii na hata wakianzisha blogu huwa wanaziacha ndani ya muda mfupi. Hii inatokana na saikolojia ya mitandao ya kijamii. Mitandao hii imetengenezwa kisaikolojia, ambapo unapoweka kitu chenye hisia fulani, unawavutia watu ‘kulike’ na ‘kukomenti’.

Hivyo unapoandika kitu au kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii, utapata wengi wanaolike na kukomenti, tofauti na ukifanya hivyo kwenye blogu. Hili linawafanya wengi kukimbilia kwenye likes na comments na kuacha kujenga jukwaa muhimu zaidi kwenye blogu.

Kuweza kuishinda saikolojia hii, unahitaji kufikiria mbali zaidi ya likes na comments. Kwenye mitandao ya kijamii unaweza kupata hizo likes na comments, lakini kujenga mahusiano mazuri baina yako na wasomaji wako huwa ni vigumu. Kwa sababu usumbufu ni mkubwa na mambo ni mengi.

SOMA; Usiangalie Umepata Likes Ngapi, Angalia Umegusa Watu Wangapi.

Lakini unapokuwa na blogu yako, unapata nafasi ya kujenga mahusiano bora sana, unapata nafasi ya kuwageuza wasomaji wako kuwa mashabiki wako na baadaye kuwa wateja wako.

Lakini kama bado unataka likes na comments kwa sababu ndiyo zinakufanya uone kweli wewe ni wa muhimu, basi fanya yote. Andika kwenye blog na andika kwenye mitandao ya kijamii. Kwa kufanya yote kwa pamoja, itakupa nafasi ya kujenga jukwaa lako ambalo ni blogu yako.

Usipotezwe na vitu ambavyo siyo muhimu ukaacha kujenga kitu muhimu. Unapochagua kufanya ujasiriamali wa taarifa, jua kujenga wafuasi na wateja ni zaidi ya likes na comments kwenye mitandao ya kijamii. Lazima uweke kazi ya kutosha kwenye blogu yako, ili watu waweze kuitembelea mara kwa mara na kuwa tayari kununua chochote unachouza.

Ni mara chache sana watu wananunua moja kwa moja kutoka kwenye mitandao ya kijamii. Lakini kwenye blogu yako, wengi watanunua kwa sababu tayari wanakujua kiundani na kazi zako wanazijua vizuri.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Sema Kitu Kimoja Kwa Wakati, Kusema Mengi Kunawachanganya Watu.

Changamoto kubwa kwenye uandishi wa aina yoyote ile, hasa kwa wale wanaoanza, ni kwenye kupangilia vizuri mtiririko wa mawazo ambayo mtu anaandikia.

Watu wengi ni kama wanatapika kwenye ukurasa wanaoandika. Wao kila kinachokuja kwenye mawazo yao wanakiweka pale.

Wengine wanakuwa na vitu vingi vya kusema, na hivyo kutaka vyote vionekane pale wanapoandika. Hii ipo sana kwenye uandishi wa matangazo na nakala za kuuza kitu. Mtu anakuwa na mengi ambayo anataka yote yaonekane.

Sasa iko hivi, kadiri unavyokazana kusema vitu vingi kwa wakati mmoja, ndivyo inavyokuwa vigumu kwa watu kukusikia na kukufuatilia. Unapokazana kusema mengi kwa wakati mmoja, watu wanashindwa kujua wafuatilie lipi na hivyo kukata tamaa moja kwa moja.

abc

Unapokuwa na mengi ya kusema au kuandika, angalia lipi lenye umuhimu kwa wakati huo, kisha sema hilo. Lieleze kwa kina na hakikisha anayesoma au kukusikiliza anakuelewa vizuri. Hayo mengine yaseme kwa wakati wake.

Andika makala inayobeba wazo kuu moja, ambalo utalielezea vizuri na kumpa mtu hatua ambazo atachukua. Kwa njia hii wengi wataweza kukufuatilia na kujifunza na hatimaye kuchukua hatua. Lakini unapokazana kuandika mambo mengi kwa pamoja, mtu anachanganyikiwa, asijue afanye lipi na kuacha lipi.

Kama unatoa tangazo, basi elezea kitu kikuu kimoja, ambacho kitakuwa na ushawishi kwa wale ambao unawalenga. Eleza kile muhimu kabisa na hatua za mtu kuchukua ili kupata kile ambacho unataka apate. Na kama yapo mengine mengi anayapata, angalia namna ya kumwambia mtu yapo bila ya kuharibu na kuchafua tangazo lako.

SOMA; Jinsi Unavyoweza Kupata Mawazo Ya Kuandika Makala Kila Siku Kwenye Blog Yako.

Unaweza pia kufikiria kwenye maelekezo, kitu chochote ambacho unakitolea maelekezo, kadiri unavyokazana kueleza mambo mengi kwa wakati mmoja, ndivyo unavyowachanganya zaidi watu badala ya kuwaelekeza. Kama unatoa maelekezo, angalia mwisho mtu anapaswa kufika wapi, kisha angalia njia moja rahisi ya kumfikisha pale na mpe hiyo.

Uandishi wa makala, matangazo, maelekezo, mchakato na vingine vingi, kadiri unavyokazana kuweka mambo machache, ndivyo watu wanakuelewa na kuweza kuchukua hatua.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

Muda Wa Kuandika Upo Wa Kutosha, Ni Wewe Kusema NDIYO Na HAPANA.

Kwenye ujasiriamali wa taarifa, kazi kubwa sana unazopaswa kufanya ni mbili, kuandika na kusoma sana. Ninaposema sana namaanisha kweli SANA. unahitaji kuandika kila siku, wakati mwingine kuandika mara nyingi kwa siku moja. Lakini pia unahitaji kusoma ili kujifunza na kupata uelewa mkubwa kwenye kile unachoandika.

Hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu huona hawawezi kufanya hivyo, kutokana na kukosa muda kwa majukumu mengine ambayo tayari wanayo.

Huhitaji muda mwingi wa siku yako kuweza kufanya majukumu hayo mawili muhimu. Bali unahitaji angalau masaa mawili kwa siku. Saa moja ya kuandika na saa moja ya kusoma. Kadiri unavyokwenda unaweza kuongeza muda zaidi.

Sasa ukweli ni kwamba, muda huwa upo, kinachofanya muda ukosekane ni vipaumbele ambavyo tunaweka kwenye muda tulionao. Vile ambavyo umevipa kipaumbele kikubwa, ndiyo vinachukua muda wako mwingi.

time to write

Hii ina maana kwamba iwapo utaweka kuandika na kusoma kama kipaumbele kikubwa kwako, basi utapata muda wa kufanya hayo. Kwa sababu ukishaweka hayo kama kipaumbele, kuna ambayo unafanya sasa utahitaji kuacha kuyafanya.

Ni swala la kusema NDIYO kwenye kuandika na kusoma na kusema HAPANA kwenye mambo mengine unayofanya sasa ambayo siyo muhimu mno.

Hivyo ukiangalia kwa upande huo wa vipaumbele, swali siyo napata wapi muda wa kuandika na kusoma, swali linakuwa kipi muhimu kwangu zaidi ya kusoma na kuandika na kipi ambacho siyo muhimu.

Kinachowaponza wengi ni wanataka maisha waliyonayo sasa yaendelee hivyo hivyo bila ya kubadilika, halafu pia waweze kusoma na kuandika, kitu ambacho hakiwezi kutokea kabisa. Lazima uache baadhi ya vitu unavyofanya sasa, ili kuweza kupata muda wa kuandika na kusoma.

Hivyo basi, kuanzia sasa usiseme huna muda, bali sema wazi kabisa kile ambacho unajiambia huna muda wa kukifanya, ni siyo cha muhimu kwako kufanya. Kikishakuwa muhimu, muda upo na utakifanya.

Weka ujasiriamali wa taarifa kama kitu muhimu kwako na kila siku utapata muda wa kukuza ujasiriamali wako huo.

SOMA; Tenga Muda Wa Kutosha Kutangaza Kazi Yako Ya Uandishi, Hakuna Atakayekufanyia Hilo.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.