Monthly Archives: October 2016

Umuhimu Na Matumizi Ya Email List Kwenye Blog Yako.

Mara zote nimekuwa nasema kwamba ili kutengeneza kipato kwenye mtandao basi unahitaji vitu vitatu.

Kitu cha kwanza ni blog, hapa ndiyo nyumbani kwako kwenye mtandao, hapa ndipo watu wakikutafuta wanakupata. Ndipo unapoweka kazi zako kwenye mtandao.

Kitu cha pili ni mfumo wa email (EMAIL LIST) kupitia mfumo huu unakusanya taarifa za wasomaji wa blog yako, hasa majina email na namba za simu, kisha unakuwa unawatumia maarifa kwenye email zao moja kwa moja. Hii ni njia nzuri ya kujenga uhusiano bora na wasomaji wako ambao utakuwezesha kufanya biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Kitu cha tatu ni mitandao ya kijamii, ambapo unahitaji kuwa na kurasa za blog yako kwenye mitandao ya kijamii unayotumia. Mitandao kama facebook, instagram, twitter na linked in ina watumiaji wengi. Unahitaji kuwa kwenye mitandao hii ili kupata wasomaji wa blog yako.

tengeneza-fedha-kwa-blog

Aina za email list.

Kuna aina nyingi za kuweza kutengeneza email list yako. Mimi nashauri utengeneze kwa aina moja kati ya hizi mbili.

Mailchimp ni moja ya aina unazoweza kutumia kutengeneza email list. Mailchimp unakuwezesha kuwa na watu 2000 bure na kuweza kutuma email mpaka 12,000 kwa mwezi. Ni rahisi kutumia na inakubali hata kwa blog za bure ambapo huna jina lako kamili (domain name).

Kutengeneza email list yako kwenye mailchimp tembelea www.mailchimp.com

Mailerlite ni aina nyingine ya kutengeneza email list, hii haina tofauti sana na mailchimp ila ni rahisi zaidi. Unapata nafasi ya kuwa na watu 1000 bure na hakuna ukomo wa email unazoweza kutuma kwa mwezi.

Mailerlite huwezi kutumia kama unatumia blog ya bure, unahitaji kuwa na jina la blog yako (domain name) na email inayoendana na jina hilo. Hivyo unahitaji uwe umehifadhi blog yako mwenyewe (Hosting).

Kutumia mailerlite tembelea www.mailerlite.com

Matumizi ya email list kwenye blog yako.

Ukishakuwa na email list yako kwanza unahitaji kuwashawishi wasomaji wako kujiunga na list hiyo. Unafanya hivyo kwa kuwaahidi kuwatumia maarifa zaidi kwenye email zao. Pia unaweza kuwapa kitabu pale wanapojiunga kwenye email list yako. Unafanya hivi kwa kuweka fomu ya kujiunga na email list yako kwenye blog yako. Weka fomu maeneo ambapo msomaji anaweza kuiona kwa urahisi. Mfano kila mwisho wa makala unaweka fomu. Au unaweka fomu inayotokea juu ya makala kabla msomaji hajasoma au anapomaliza kusoma.

Ukishapata watu kwenye email list yako sasa unaweza kuitumia ifuatavyo;

 1. Tengeneza utaratibu wa kuwa unawatumia maarifa zaidi watu kwenye email zao. Unafanya hivyo kwa kuingia kwenye list yako kisha kutengeneza na kutuma kampeni ya email (email campaign).
 2. Waulize wasomaji iwapo wana changamoto zozote kwa maswali unayoweza kuwa unawatumia kwenye email zao, na hapo unaweza kuwashauri moja kwa moja au kupata makala za kuandika.
 3. Wapatie wasomaji wako ofa mbalimbali kwa kuwatumia taarifa kwenye email zao, hili fanya baada ya muda na wasomaji wako kuwa wameshakuzoea.
 4. Unganisha email list yako na blog yako kiasi kwamba unapoweka makala mpya kwenye blog inakwenda mara moja kwenye email za wasomaji wako. Hii haiji moja kwa moja, badala yake ni lazima utengeneze hivyo. Kutengeneza hili unahitaji kwenda kwenye email list yako, nenda kwneye kuandaa email campaign na chagua RSS feed au campaign, utafuata maelekezo baada ya hapo.
 5. Endesha mafunzo au semina kupitia email list yako, hii pia ni njia nzuri ya kukuza list yako.

Hivyo ndivyo unavyoweza kuwa na email list na jinsi unavyoweza kuitumia.

Kupokea maarifa zaidi kuhusu kutengeneza fedha kwenye mtandao weka taarifa zako kwenye email hapo chini.

[mailerlite_form form_id=1]

Kama una swali lolote kuhusu kutengeneza fedha kwenye mtandao au blog uliza kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Makirita Amani,

Kocha, Mwandishi na Mjasiriamali,

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kupata blog ya kitaalamu kwa tsh elfu kumi (10,000/=) bonyeza maandishi haya.

Kupata kitabu cha kutengeneza blog yako mwenyewe bonyeza maandishi haya.

Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Jinsi Ya Kutumia Lugha Ya Kiswahili Kwenye Uandishi Na Uhariri Wa Makala.

Moja ya changamoto kubwa zinazowakumba waandishi wa vitabu na makala ni uhariri. Unapoandika kuna maneno utayakosea na hata unapohariri unaweza usione maneno yote uliyokosea.

Wengi huishia kuweka kazi ambayo haijafanyiwa uhariri wa kutosha hivyo kuwa na makosa madogo mengi.

Madhara ya makosa haya ni msomaji kuona mwandishi amekosa umakini au hajali kuhusu kazi yake. Na kama wewe mwenyewe hujali kuhusu kazi yako kwa nini msomaji ajali? Hivyo unakuwa unapoteza wasomaji wengi kwa makosa yako ya uandishi.

Kwenye makala ya leo nitakuelekeza namna ya kutumia lugha ya Kiswahili kwenye kuandika na kuhariri makala. Nitakupa maelekezo kwa picha na kazi itakuwa kwako kuchukua hatua.

Kwa mfano angalia hii picha hapo chini, neno hili ina mstari mwekundu chini yake kuonesha kwamba nimekosea kuandika, hivyo unakuwa rahisi kwangu kufanya uhariri, nisingekuwa na programu hiyo ya Kiswahili isingekuwa rahisi kuona makosa hayo.

blog-kiswahili

Mambo unayohitaji.

Kabla hatujaanza kwanza nikuambie kitu gani unahitaji.

Unahitaji kuwa na programu ya microsoft word kwenye kompyuta yako, kuanzia toleo la 2010 na kwenda mbele.

Utahitaji kupakua program maalumu ya lugha ya kiswahili.

Hatua za kuwezesha lugha ya Kiswahili kwenye kompyuta yako;

 1. Pata microsoft 2013.

Kupata programu ya microsoft word 2013 ipakue kupitia kiungo hiki; https://word-2013.jaleco.com/ au bonyeza maandishi haya hili ni toleo la majaribio, TRIAL VERSION, watakuambia uweke key, usiweke kwanza, wewe endelea kutumia.

Pakua programu hiyo na iweke kwenye kompyuta yako.

 1. Pata programu ya Kiswahili.

Nenda kwenye tovuti ya microsoft ili kupata ana za Kiswahili, tumia kiungo hiki; https://www.microsoft.com/sw-KE/download/details.aspx?id=35400 au bonyeza maandishi haya.

Pakua namba moja na namba mbili kama inavyoonekana kwenye picha.

blog-kiswahili-1

Install programu hizo kwenye kompyuta yako, hakikisha tayari umeinstall microsoft word 2013.

 1. Kuiwezesha program kufanya kazi.

Fuata maelekezo hapo kwenye picha angalia nilipozungushia duara nyekundu.

blog-kiswahili-2

Fungua microsoft word, bonyeza sehemu ya FILE.

blog-kiswahili-3

Bonyeza sehemu ya option.

blog-kiswahili-4

Ikishafunguka bonyeza sehemu ya LANGUAGE.

blog-kiswahili-5

Ikishafunguka bonyeza Kiswahili, bonyeza SET AS Default. Kisha bonyeza OK.

blog-kiswahili-6

Ukimaliza bonyeza sehemu ya PROOFING, hakikisha umeweka yafanane na hapo juu kwenye picha. Kisha bonyeza OK.

Kwa hatua hizo utakuwa umemaliza kuweka lugha ya Kiswahili, unapoandika pale chini kwenye lugha pataonekana KISWAHILI. Kama haionekani andika makala kwenye microsoft word, kisha highlight makala yote kisha nenda sehemu ya lugha pale chini na chagua kiswahili.

Kwa kutumia program hii utaweza kuhariri kazi zako vizuri.

Hongera kwa kujifunza, kupata mafunzo zaidi kuhusu blog moja kwa moja kwenye blog yako jaza fomu hapo chini.

[mailerlite_form form_id=1]

Nakutakia kila la kheri.

Makirita Amani,

Kocha, Mwandishi na Mjasiriamali,

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kupata blog ya kitaalamu kwa tsh elfu kumi (10,000/=) bonyeza maandishi haya.

Kupata kitabu cha kutengeneza blog yako mwenyewe bonyeza maandishi haya.

Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Vitu Viwili Unavyohitaji Ili Uweze Kutengeneza Fedha Kupitia FACEBOOK.

Je umekuwa unatumia mtandao wa facebook kila siku ya maisha yako? Kama unasoma hapa, basi najua jibu lako ni ndiyo. Na ninajua bila ya shaka kwamba kila siku lazima uingie kwenye mtandao huu wa kijamii namba moja duniani. Ikitokea siku hujaingia kwenye mtandao huu unajiona kama kuna kitu umekosa.

Swali muhimu nataka kukuuliza na wewe mwenyewe ujiulize ni je ungependa kutengeneza fedha kwa kutumia mtandao huu wa facebook? Yaani ungependa kwa kuingia kwako kwenye mtandao wa facebook uweze kuingiza kipato? Kama jibu ni ndiyo basi endelea kusoma na nitakuonesha namna unaweza kufanya hivyo. Kama jibu ni hapana, hutaki kuingiza kipato kila unapoingia kwenye facebook, basi unaweza kuishia hapa, kwa leo.

facebook-money

Nilijiunga na mtandao wa Facebook mwaka 2009, lakini sikuwa najua kama naweza kuutumia kuingiza kipato. Nilikuwa nauchukulia kama mtandao wa kukutana na marafiki, kuoneshana picha na kubishana kuhusu siasa, michezo na kingine kinachoweza kuleta ubishi baina ya wengi.

Ni mpaka ilipofika mwaka 2013 ndipo nilijua kwamba naweza kutengeneza kipato kwa kutumia facebook. Ni kwa mara ya kwanza mwaka huo niliweza kupata fedha kwa kupitia facebook. Na tangu kipindi hicho, mpaka sasa nimekuwa natengeneza kipato kwa kutumia mtandao huu wa facebook.

Leo nataka nikushirikishe hatua unazoweza kutumia kutengeneza kipato kwa kutumia Facebook, kwa sababu, kama mpaka sasa unasoma hapa, jibu lako ni kwamba unataka kutengeneza kipato kwa kutumia facebook.

Facebook ni nini?

Kabla hatujaangalia jinsi unaweza kuingiza kipato kwa kutumia mtandao huu wa facebook, kwanza tuangalie facebook ni nini.

Wote tunajua kwamba facebook ni mtandao wa kijamii. Ni sehemu ambayo watu tunakutana kupeana habari mbalimbali na pia kushirikishana yale ambayo yanaendelea kwenye maisha yetu.

Wapo watu ambao wanaingia kwenye facebook kila siku ili kupata habari mbalimbali, wapo wanaoingia ili kujua wengine wanafanya nini kwenye maisha yao.

Unaingizaje kipato kwa kutumia facebook?

Njia ya uhakika ambayo wewe hapo ulipo unaweza kuitumia kuingiza kipato kwa kutumia mtandao wa facebook ni kutoa maarifa na taarifa ambazo watu wanazihitaji ili kuwa na maisha bora. Maarifa hayo unaweza kuwa nayo wewe kwa kusomea, kujifunza mwenyewe au kwa uzoefu.

Maarifa na taarifa hizi inaweza kuwa kuhusu afya, kuhusu biashara, kuhusu uchumi, kuhusu fedha, michezo, dini na chochote kile ambacho unakijua na watu wanaweza kukitumia kuwa na maisha bora.

Kwa maana hii, hapo ulipo wewe, tayari una maarifa na taarifa za kuweza kukuingizia kipato kupitia mtandao wa facebook.

Vitu viwili unavyohitaji ili kuingiza kipato kwa kutumia facebook.

Ili uweze kutengeneza kipato kwa kutumia mtandoa wa facebook, kuna vitu viwili muhimu sana unavyohitaji. Iko hivi, siyo rahisi sana (sisemi haiwezekani) kutengeneza kipato moja kwa moja ndani ya mtandao wa facebook. Ila kuna vitu viwili ambavyo utavitumia pamoja na facebook kuweza kutengeneza kipato.

Kitu cha kwanza; unahitaji kuwa na BLOG.

Iko hivi, kama facebook ni sehemu ambayo unakutana na watu mbalimbali, tunaweza kuchukulia kama kijiweni, basi blog ndiyo nyumbani kwako. Hii ina maana kwamba baada ya kukutana na watu kijiweni, unaweza kuwakaribisha nyumbani kwako.

Hivyo ndivyo ilivyo pia, ukishakutana na watu kwenye facebook, unahitaji kuwakaribisha kwenye blog yako, ili wapate mengi zaidi kutoka kwako. Kama wewe ambavyo umefika kwenye blog yangu kwa kutokea facebook.

Blog ni sehemu ambayo unaweka taarifa na maarifa unayotoa kwa wengine. Ni sehemu nzuri ambapo mtu akifika anakutana na taarifa zako zote na hivyo kuweza kujifunza vizuri. Ni muhimu sana uwe na blog, kwa sababu kupitia blog yako ndiyo unaweza kuwa na watu wanaokufuatilia kwa karibu.

Kitu cha pili; MFUMO WA EMAIL (EMAIL LIST)

Ukishakuwa na blog, ambayo ni nyumbani, unahitaji kuwa na mfumo wa kukusanya mawasiliano ya wasomaji wako, ambao unaitwa email list. Kama facebook ni kijiweni, blog ni nyumbani, basi email list ni chumbani. Ni watu gani unawaruhusu waingie chumbani kwako? Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba siyo kila mtu unampeleka chumbani, ila wale marafiki zako wa karibu unawaruhusu kuingia chumbani kwako.

Hivyo basi ni muhimu sana uwe na email list, wasomaji wanapofika kwenye blog yako, na kusoma maarifa unayotoa, kuna ambao watahitaji kupata zaidi kutoka kwako. Hawa unawakaribisha chumbani, kwa kuwaruhusu wakupe taarifa zako kwenye mfumo wako wa email.

Hawa wasomaji ambao wanakupa taarifa zao, ndiyo wanakuwa wa kwanza kabisa kununua chochote ambacho utaamua kuwauzia.

Kwa kukamilisha nikukumbushe haya muhimu;

 1. Unaweza kutengeneza fedha kwa kutumia mtandao wa facebook.
 2. Facebook ni kama kijiwe ambapo unakutana na watu.
 3. Blog ni nyumbani kwako kwenye mtandao wa intaneti, ni lazima uwe na blog ili kutengeneza fedha.
 4. Email list ni chumbani kwako, ambapo unawakaribisha marafiki zako wa kweli. Hawa ndiyo ambao wanakuamini na watakuwa tayari kununua kile unachouza.

Kwenye makala zijazo nitakushirikisha vitu gani unaweza kuuza kwenye facebook na mtandao wa intaneti kwa ujumla.

Kama unahitaji kupata blog na email list fuata maelekezo hapo chini.

Kujiunga na email list na upokee makala kama hizi jaza fomu hiyo hapo chini.

[mailerlite_form form_id=1]

Asante na karibu sana.

Makirita Amani,

Kocha, Mwandishi na Mjasiriamali,

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kupata blog ya kitaalamu kwa tsh elfu kumi (10,000/=) bonyeza maandishi haya.

Kupata kitabu cha kutengeneza blog yako mwenyewe bonyeza maandishi haya.

Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.