Sababu Moja Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuwa Na Blog, Hata Kama Hutaki Kipato Mtandaoni (NA ZAWADI YA KITABU BURE.)

Ushauri wangu siku zote umekuwa ni huu, katika zama tunazoishi sasa, kila mtu, nisisitize, KILA MTU anapaswa kuwa na blog. Siyo tu kama sehemu ya kutengeneza kipato, bali pia kama sehemu ya kutoa mchango wake kwa jamii inayomzunguka, kwa upande wa maarifa, na pia kuifanya kama jarida binafsi ambapo unaweza kuandika mambo yako na maisha yako yanavyoenda.

Wacha nikupe mfano, moja ya vitabu ambavyo vimesomwa sana na kuwasaidia wengi katika uongozi, biashara na hata kuwa imara kupambana na changamoto, ni kitabu kinachoitwa MEDITATIONS ambacho kimeandikwa na Marcus Aurelius, wakati wa uhai wake miaka ya 180, baada ya kuzaliwa Kristo. Ni kitabu kizuri mno, na kinakujenga sana, kama pia hujakisoma, fanya hima ukisome. Kama huna wasiliana nami kwa wasap 0717396253 na nitakupa kitabu hicho.

Sasa ninachotaka kukuambia ni kwamba, Marcus hakuandika kitabu hicho kama kitabu. Yaani hakukaa chini na kusema naandika kitabu. Bali kitabu hichi kilikuja kupatikana miaka mingi baada ya yeye kufa. Maandiko hayo yalikuwa ni jarida lake binafsi, ambapo kila siku alijipa muda mchache wa kuyatafakari maisha yake na kuandika.

Lakini miaka karibu elfu mbili sasa watu wamesoma kitabu hichi na wamenufaika sana. Na kitaendelea kuwanufaisha wengi, japo yeye hajui kama kimekuja kuwa kitabu.

Marcus Aurelius alikuwa mtawala wa Roma na pia mwanafalsafa wa ustoa. Aliweza kuiongoza Roma vizuri, akashinda vita kali na kuwa kipenzi cha wengi.

Sasa tukija kwako wewe, unaweza kuwa na blog ambapo unaandika mawazo yako. Kwa sababu kila mmoja wetu huwa ana mawazo mengi kwenye akili yake. Kila siku tunakutana na mambo mengi, tunajifunza mambo mengi, kwenye maisha, kazi, biashara na hata mahusiano yetu na wengine.

Unaweza kujitengenezea utaratibu wa kuwa unakaa chini na kuandika haya yote unayojifunza na unayofikiri. Na uzuri siyo lazima dunia ione, unaweza kuifanya blogu yako kuwa ya siri, ambayo unaiona wewe mwenyewe tu. Au ukawapa ruhusa watu fulani pekee waisome.

SOMA;Jinsi Unavyoweza Kupata Wasomaji Wa Kudumu Kwenye Blogu Yako.

Huwezi kujua huenda blogu hii ikaja kuwa msaada kwa wengine wengi. Huenda ikaja kuwasaidia watoto na wajukuu zako siku zijazo, wewe ukiwa haupo wakawa wanapata ushauri mzuri kupitia blog yako.

Ndiyo maana nimekuwa nakushauri sana kuwa na blog, siyo kwa sababu itakusaidia wewe tu, bali kwa sababu itavisaidia vizazi vijavyo, kama utakuwa na ndoto ya aina hiyo.

Kama bado huna blog na ungependa kuwa nayo, au kama unataka ushauri kuhusu blogu, tuwasiliane kwa njia ya wasap kwa namba 0717396253. Pia kama ungependa kupata kitabu cha MEDITATIONS cha Marcus Aurelius, nitumie ujumbe kwa njia hiyo ya wasap na nitakutumia.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Sababu Moja Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuwa Na Blog, Hata Kama Hutaki Kipato Mtandaoni (NA ZAWADI YA KITABU BURE.)

  1. Pingback: Jambo Pekee La Kiungwana Unaloweza Kufanya Kwenye Mtandao Wa Intaneti Ni Hili, Na Ukalipwa Pia. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Andika Kitabu Ambacho Ungependa Kukisoma, Lakini Bado Hujakipata. | MTAALAMU Network

Leave a Reply