Kama Unasema Huna Muda Wa Kuandika, Nihakikishie Kwanza Hufanyi Vitu Hivi Vitano, Nitakuelewa.

Ushauri wangu kwa mtu yeyote ambaye anataka kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii huwa ni huu; ANDIKA KILA SIKU.

Huo ndiyo msingi wa kwanza na muhimu sana ambao kila mtu anapaswa kuuishi, kwa sababu tupo zama za taarifa, na moja ya njia kuu za kutoa taarifa na maarifa ni kuandika. Andika kwenye blog yako (ambayo lazima uwe nayo), andika kwenye mitandao yako ya kijamii, na andika kwenye email list yako. Hivi ni vitu vitatu ambavyo hupaswi kuvikosa.

Sasa wengi wakishasikia ushauri wangu huo, wanakuja na sababu moja kubwa kwao ambayo ni HAWANA MUDA WA KUANDIKA. Wengi watakuambia ni namna gani muda umewabana, kazi ni nyingi na hawapati muda wa kuweza kukaa chini na kuandika. Wengine watakuambia namna hawana mtandao wa kuweza kuandika na kuweka kwenye mtandao kila siku.

Mimi nimekuwa sipokei sababu hizo kirahisi, na nimekuwa nawahoji zaidi na kugundua, wanaosema hawana muda wa kuandika, wanaona tu aibu kusema ukweli kwamba ni wavivu kuandika. Kwa sababu ninapojaribu kupitia nao siku yao, naona namna gani wana muda mwingi kwenye siku wanaupoteza, lakini hawaoni aibu kusema hawana muda.

Sasa leo nataka nikuamie na wewe wazi, kama unasema huna muda wa KUANDIKA KILA SIKU, nihakikishie kwanza kwamba hufanyi yafuatayo, na nitakiri kwamba huna muda na kukuacha ufanye yako;

SOMA;Jinsi Unavyoweza Kupata Mawazo Ya Kuandika Makala Kila Siku Kwenye Blog Yako.

  1. Nihakikishie kwamba hutembelei mtandao wowote wa ijamii hata dakika moja ya siku yako. Yaani facebook, instagram, wasap, yote hupati hata muda wa kuchungulia na kuona nini kinaendelea. Kama unapata fursa hiyo, basi una muda wa kutosha wa kuandika, acha sababu.
  2. Nihakikishie kwamba wewe hufuatilii habari yoyote ile kwenye siku yako, yaani husomi gazeti, husikilizi redio na wala huangalii tv, ukinihakikishia hilo, nakuacha kabisa. Ila kama unapata muda wa habari, una muda wa kutosha wa kuandika.
  3. Nihakikishie ya kwamba wewe siyo shabiki wa mchezo wowote ule, kwamba huwa huangalii mchezo wowote ule iwe ni moja kwa moja au kwenye luninga. Kama jibu ni hapana, hebu anza kuandika, usiendelee kujidanganya.
  4. Nihakikishie kwamba kila siku hupati muda wa kutosha wa kulala, unalala chini ya masaa sita, na nje ya hapo upo kwenye kazi au majukumu mengine muhimu zaidi ambayo ukiyaacha tu kuna mambo mabaya sana yatatokea na watu watadhurika. Kumbuka hiyo ni kila siku, siku 7 za wiki. Kama haupo kwenye hali hiyo, kubali tu wewe ni mzembe na huaki kuandika.
  5. Nihakikishie kwamba siku yako mwanzo mwisho ni kazi, ukiamka hapo hapo ni kazi, hakuna mapumziko, chakula unakula ukiwa kwenye kazi, na ukitoka kwenye kazi ni kwenda kulala. Kama siku yako ipo tofauti na hapo, halafu huandiki kila siku, umeamua tu kujidanganya kwa sababu hutaki kuuona ukweli.

Kwa kifupi, ninachotaka kukukumbusha hapa ni kwamba muda upo, swala ni wewe kuweka vipaumbele. Badala ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kuzurura humo, hebu kaa na uandike kwanza. Badala ya kuanza kufuatilia habari na kushabikia mambo, kaa chini uandike kwanza. Na muhimu zaidi, unapoamka, kabla hujaanza mambo mengine, kaa chini na uandike kwanza. Fanya hivyo, na utaona namna itakavyokusukuma kufanya kazi bora na kuweza kujijenga vizuri kwenye mtandao wa intaneti.

Mwisho kabisa, kama unasumbuka na kudhibiti muda wako, nina kitabu kizuri sana ambacho kitakusaidia kwenye hilo. Kitabu kinaitwa PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU. Nakuambia ukisoma kitabu hichi, utaweza kutenga masaa mawili, ambayo ukiyawekeza kwenye blog au uandishi wako, utafika mbali mno muda siyo mrefu. Kupata kitabu hichi tuma fedha tsh 5,000/= kwa namba za simu 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu hichi moja kwa moja kwenye email yako.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

1 thought on “Kama Unasema Huna Muda Wa Kuandika, Nihakikishie Kwanza Hufanyi Vitu Hivi Vitano, Nitakuelewa.

  1. Pingback: Kila Wazo Linahitaji Kuboreshwa Zaidi, Hivyo Anzia Popote Na Endelea Kuwa Bora. | MTAALAMU Network

Leave a Reply