Unawezaje Kuandika Pale Unapokuwa Hujisikii Kuandika?

Mwandishi mmoja mashuhuri, aliulizwa tofauti ya mwandishi aliyebobea na mwandishi mchanga. Na bila ya kusita alisema mwandishi mchanga anaandika pale anapojisikia, ila mwandishi aliyebobea anaandika wakati wote, iwe anajisikia au hajisikii.

Nimekuwa nakusisitiza mara nyingi ya kwamba, kuweza kufikisha uandishi wako kwenye ngazi kubwa ya kuweza kupelekea kulipwa, kwanza uandike kila siku, KILA SIKU.

Ila sasa changamoto inakuja unawezaje kuandika kila siku iwapo kuna siku hujisikii kuandika?
Hapa sina muujiza wowote wa kukupa, zaidi ya kukuambia unahitaji kujijengea nidhamu ya kuandika kila siku. Inabidi upange ratiba yako ya uandishi, muda unaoandika na kila siku andika, ndani ya muda ule.

Ni vyema muda huo ukawa asubuhi, kabla hujafanya jambo jingine lolote. Amka kaa chini na andika. Iwapo hujisikii kuandika, kaa na andika. Kaa pale mpaka uandike kitu.

Usikimbilie kujisumbua, maana wengi wanapokuwa hawajisikii kuandika, husema labda wachungulie facebook kuna nini, au instagram, au wasap. Kote huko ni usumbufu na kunazidi kukuondoa kwenye kuandika.

SOMA;Ukitaka Kuandika Vizuri, Ondokana Kwanza Na Huu Usumbufu.

Dawa ya kutokujisikia kuandika ni kuandika. Hivyo tu. Kaa chini na andika.

Andika chochote, anza kuandika, bila ya kujihukumu au kujikosoa. Anza kuandika neno moja na nenda neno jingine linalofuatia. Kaa hapo mpaka uandike kitu chenye kuweza kumsaidia mtu. Halafu ukumbuke una uwezo wa kufuta chochote ulichoandika, hivyo kama mwanzo ulianza kwa kuandika kitu cha hovyo, usiwe na wasi wasi, unaweza kufuta wakati wowote.

Kuwa mwandishi mbobezi, andika siyo kwa sababu unajisikia kuandika, ila andika kwa sababu unataka kuandika, ndiyo jukumu lako, ndiyo wajibu wako, kila siku.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Unawezaje Kuandika Pale Unapokuwa Hujisikii Kuandika?

  1. Pingback: Hapo Ulipo Tayari Umekamilika Kama Mwandishi, Anza Kuandika Utaendelea Kuwa Bora Zaidi. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Tengeneza Hamasa Ya Kuandika, Na Siyo Kusubiri Mpaka Upate Hamasa. | MTAALAMU Network

Leave a Reply