Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuandika.

Kitu kikubwa ambacho kinawazuia watu kuchukua hatua kwenye maisha yao ni hofu. Hofu ndiyo inayowatofautisha wale wanaojaribu mambo makubwa na kufanikiwa, na wale wanaoshindwa na kuendelea kuwa na maisha magumu.

Tofauti hii haitokani na hofu kuwa tofauti kwa watu, bali hutokana na namna watu wanavyoichukulia hofu. Wale ambao wanaweza kufanya licha ya kuwepo kwa hofu, siyo kwamba wanakuwa na hofu ndogo au ujasiri mkubwa. Ila tu wanakuwa wamechagua kufanya licha ya uwepo wa hofu. Yaani wao wanakuwa na hofu lakini wanaendelea kufanya.

Kwa upande wa pili, wale wanaoshindwa kufanya, huwa wanaipata hofu na kuruhusu hofu iwatawale, wasiweze kuchukua hatua kabisa.

Kwenye uandishi, hali ni hiyo hiyo, wengi hushindwa kuandika kwa sababu ya hofu. Hofu kwamba watu watawachukuliaje, hofu kwamba watu watawapinga na kuwakosoa. Hofu kwamba wataandika kitu ambacho kitawafanya wengine wawashangae na hata kuwahukumu. Na kubwa zaidi, hofu kwamba bado hawajawa tayari na hivyo kuendelea kusubiri.

Lakini hata mtu achukua muda kiasi gani wa kusubiri, hizo hofu huwa hazipungui, badala yake zinaongezeka zaidi. Kadiri muda unavyokwenda ndivyo hofu hizo zinavyokua na kuzidi kumzuia mtu kuchukua hatua.

SOMA;Naweza Kumsaidia Nani? Naweza Kumsaidia Nini? Njia Ya Kupata Mawazo Ya Kuandika.

Hivyo dawa pekee ya hofu ya kuandika, ni kuanza kuandika. Hivyo tu. Yaani pale unapofikiria kuandika halafu unapata hofu, basi hapo ndiyo unapaswa kuandika. Andika kile kinachokupa hofu na kiweke kwa wale unaohofia kama kikiwafikia itakuwaje.

Kwa kufanya hivi, utagundua kumbe mambo siyo mabaya kama ulivyokuwa unafikiria awali. Picha uliyokuwa umejijengea kwenye mawazo yako kwamba watu watakupinga na kukukosoa, inakuwa kubwa kuliko uhalisia.

Hii ni njia nzuri na ya uhakika ya kuondokana na hofu ya kuandika, ambayo ni kuandika. Pale unapopata hofu ya kuandika, ndiyo unapaswa kuchukua hatua na kaundika. Pale unapata hofu ya kuandika, anza kuandika na utaona hofu hiyo ikipotea yenyewe. Na unapoiweka kazi yako mbele ya wale uliokuwa unawahofia, utagundua mambo siyo mabaya kama ulivyokuwa unadhania.

Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia MTAALAMU NETWORK. Kupata ushauri wa blog na jinsi ya kutengeneza kipato tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253.

Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu na kuweza kutengeneza fedha kwenye mtandao, BONYEZA MAANDISHI HAYA.

Kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, bonyeza maandishi haya.

KUPOKEA MAKALA NA MAARIFA YA KUTENGENEZA FEDHA KWA BLOG KWENYE EMAIL YAKO BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UJAZE FOMU.

2 thoughts on “Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuandika.

  1. Pingback: Andika Kama Unavyoongea, Na Siyo Kama Unavyojibu Mtihani. | MTAALAMU Network

  2. Pingback: Je Unawezaje Kuandika Kuhusu Mafanikio Iwapo Wewe Hujafanikiwa? | MTAALAMU Network

Leave a Reply